Mapendekezo ya bajeti Mwanza.
Serikali mkoani Mwanza imewasilisha mapendekezo ya mpango wa bajeti inayofikia kiasi cha Bil. 451, 948,254,000 kwa ajili ya mwaka wa fedha 2017/2018 hii ikiwa ni ongezeko la asilimia thelathini na tisa kutoka katika bajeti ya mwaka 2016/2017 iliyokuwa Bil. 324,577,344,000.
Akisoma mapendekezo hayo mbele ya kikao cha kamati ya ushauri cha Mkoa wa Mwanza, Mchumi katika Sekretarieti ya mkoa huo Bw. Michael Nyanda, alisema mapendekezo hayo nikwaajili ya fedha za matumizi ya kawaida na zile za maendeleo.
Nyanda amesema kuwa, katika mapendekezo hayo, katika ngazi ya sekretarieti ya mkoa umependekeza kiasi cha Bil. 16,025,134,000 kwaajili ya fedha za mishahara, maendeleo na matumizi ya kawaida na halmashauri zote nane za mkoa wa Mwanza mapendekezo yake ni Bil. 435,923,120,000, ambazo nazo zitaelekezwa katika miradi mbali mbali ya maendeleo na matumizi ya kawaida ikiwepo mishahara ya watumishi.
Katika mapendekezo hayo, Nyanda amesema, endapo mkoa utaidhinishiwa na Bunge, fedha hizo zitawezesha miaradi mbali mbali ya maendeleo kuanza na mingine kukamilika ikiwepo miradi ya jamii na ile ya serikali, ameitaja miradi ambayo itatekelezwa inatoka katika sekta za Afya, Maji, Elimu, Miundombinu, kilimo na Ushirika.
Ametaja Fedha hizo pia zitaelekezwa katika sekta za fedha kwa ajili ya kuimarisha miundombinu ya ukusanya wa mapato, ikiwepo kutilia mkazo ukusanyaji mapato kwa njia ya Kieletroniki.
Maeneo mengine ni Utawala, maendeleo na ustawi wa jamii, UKIMWI na Virusi vya Ukimwi, ambapo mkoa unakusudia kuvijengea uwezo vikundi na asasi zilizo katika mapambano ya vita dhidi ya UKIMWI na Virusi vya UKIMWI, aidha pia Mpango huo umezingatia suala la upangaji miji na uimarishaji wa matumizi bora ya ardhi na kutatua migogoro iliyopo.
Kikao cha kamati cha ushauri cha mkoa kilikaa chini ya Mwenyekiti wake Mkuu wa mkoa wa Mwanza John Mongella na kuhudhuriwa na Viongozi wa dini, Vyama vya siasa, Wenyeviti na mameya, wakurugenzi wa Halmashauri, wataalam kutoka ngazi ya mkoa na Wilaya sambamba na asasi za kiraiya.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.