• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
Mwanza Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Mwanza

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia ya Mkoa
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti Mkoa
    • Seksheni
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Serikali za Mitaa
      • Afya
      • Elimu
      • Maji
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa Ndani
      • ununuzi na Ugavi
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Kitengo cha Sheria
  • Wilaya
    • Ilemela
    • Nyamagana
    • Magu
    • Misungwi
    • Kwimba
    • Sengerema
    • Ukerewe
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Jiji la Mwanza
    • Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
    • Hamashauri ya Wilaya ya Magu
    • Hamashauri ya Wilaya ya Sengerema
    • Hamashauri ya Wilaya ya Misungwi
    • Hamashauri ya Wilaya ya Kwimba
    • Hamashauri ya Wilaya ya Ukerewe
    • Hamashauri ya Wilaya ya Buchosa
  • Fursa za uwekezaji
    • Miundombinu ya Umwagiliaji na kilimo cha mkataba
    • Kilimo
    • Madini
    • Sekta ya Huduma
  • Huduma zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Watumishi
  • Machapisho
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa Kwa vyombo vya habari
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya video

Hakikisheni utoro unadhibitiwa - Ligola

Posted on: April 5th, 2019


Wakuu wa Shule za Sekondari Mkoani Mwanza (TAHOSSA) wamefanya kikao katika ukumbi wa Shule ya Sekondari ya Wasichana Bwiru wakiwa na lengo la kuleta umoja na kujadili kuhusu maendeleo ya taaluma Mkoani hapo.

Akiongea katika kikao hicho Mgeni rasmi ambaye ni Afisa Elimu Mkoa wa Mwanza Michael Ligola amesema, ili kukuza taaluma ni lazima kila mmoja wetu kutimiza wajibu wake ikiwa ni pamoja na kuaminiana  na kuwa na nidhamu katika kazi kwa kuepuka udanganyifu na kutokujihusisha na siasa.

"Lugha nzuri kwa wasaidizi na wazazi wanaokuja kufuatilia maendeleo ya watoto huleta amani na ushirikiano katika kazi,hii huleta picha nzuri kwani hujenga uaminifu,"alisema Ligola.

Aidha aliongeza kuwa nidhamu ya wanafunzi imeshuka sana na hii ndiyo inayopelekea baadhi ya shule kuto faulu vizuri katika masomo, na kuwaasa wakuu hao kuhakikisha wanasimamia nidhamu ya wanafunzi na walimu pia.

"Hatupo katika kuhakikisha watoto wanafukuzwa shule, walimu wa malezi kwa namna moja ama nyingine, wajitahidi kurudisha nidhamu ya wanafunzi na kuhakikisha kuwa utoro unadhibitiwa pia walimu wanaokiuka taratibu wachukuliwe hatua.

Ligola amewataka wakuu wa shule kuwaamini na kuwaandaa   wasaidizi wao kuwa wakuu wa shule na viongozi wazuri wa baadaye katika Nchi hii.

Hata hivyo ameongeza kuwa ili kuendelea kufanya vizuri katika taaluma ni vema kufanya majaribio mara kwa mara, na amewahakikishia kuwa Serikali inafahamu changamoto wanazokumbana nazo walimu na inaendelea kuzifanyia kazi.

"Naye Mkuu wa Shule ya Sekondari  Nyampulukano Christine E. Zegela amesema mara nyingi wao wamefanikiwa kwa sababu pale mwanafunzi anaposhindwa kufaulu wanakaa naye kujua tatizo ni nini pia wanawaita wazazi ili kushauliana namna ya kuboresha elimu, hata hivyo walianzisha chakula shuleni hii imeboresha ufaulu kwa kiasi kikubwa.

Kwa upande wake Mkuu wa Shule ya Sekondari ya wasichana Nganza Yasinta Lyimo amesema kuwa nidhamu  kwa walimu na wanafunzi ndiyo msingi wa ufaulu katika shule yao.

Matangazo

  • WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA KIDATO CHA KWANZA MKOA WA MWANZA MWAKA 2021 December 18, 2020
  • Matokeo ya Uchaguzi wa Wanafunzi Waliochaguliwa Kujiunga na Kidato cha Kwanza 2018 Shule za Sekondari za Serikali Mkoa wa Mwanza December 13, 2017
  • Ziara ya Mhe. Mkuu wa Mkoa kwa ajili ya kufanya ufuatiliaji katika shule za Msingi na Sekondari Mkoa wa Mwanza 2018 January 10, 2018
  • Ufunguzi wa Mashindano ya UMISSETA na UMITASHUMTA Kitaifa Mkoa wa Mwanza. June 07, 2018
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • AGA KHAN Yatoa Vifaa vya Bilioni 1.5 Kuepusha vifo vya mama na mtoto Mwanza

    December 22, 2020
  • Kikao cha bodi ya Barbara chapanga mikakati ya mafanikio Mwanza

    December 21, 2020
  • Mwanza Kwanza Toleo la pili kwa habari mbalimbali Mkoa wa Mwanza

    December 12, 2020
  • Elimu ya maadili yatolewa Mwanza kwa Viongozi

    December 10, 2020
  • Angalia zote

Video zinazotembea

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe.John Mongella akifungua Baraza la biashara katika kikao kilichofanyika kwenye ukumbi wa mkikutano uliopo katika ofisi ya Mkoa uliojumuisha wajumbe mbalimbali wa Baraza hilo wa Mkoa wa Mwanza.
video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Fomu ya Ugonjwa
  • FFARS User Guidelines
  • Miongozo ya mfumo wa bajeti na Mipango
  • Makusanyo ya Ndani ya Halmashauri za Mkoa wa Mwanza
  • PReM
  • Maswali Yaulizwayo Mara kwa Mara
  • Opras fomu
  • OFISI MTANDAO

Viunganishi Linganishi

  • Tovuti ya Ikulu
  • Utumishi
  • Tamisemi
  • Ofisi ya Taifa ya Takwimu Tanzania
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Kuu ya Serikali

Watembeleaji

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    Regional Drive Mkabala na Ofisi za TRA

    S.L.P: S.L.P. 119, Mwanza.

    Simu: 028-2501037

    Simu ya Mkononi: 028-2501037

    Barua Pepe: ras.mwanza@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.