Mei, 20 kila mwaka nchi nyingi duniani husherehekea siku ya vipimo duniani. Mwaka huu kauli mbiu ( theme) ya maadhimisho ni vipimo katika sekta ya usafirishaji (measurement for transport) .
Wakala wa Vipimo inalo jukumu la kumlinda mlaji na umma kwa ujumla kupitia uhakiki na uthibiti wa vipimo vinavyotumika katika biashara na huduma nyingine, kuhakikisha kuwa vipimo hivyo ni sahihi na vinatumika kwa usahihi kulingana na Sheria ya Vipimo Sura 340 mapitio ya mwaka 2002 na maboresho yake ya mwaka 2016 pamoja na kanuni zake.
KAZI ZA WAKALA
Kudhibiti ufungashaji wa bidhaa (Net quantity & lebelling)
Kuwa kiungo cha Taifa letu na taasisi za Kikanda na Kimataifa katika masuala ya vipimo (legal Metrology)
Kutoa ushauri wa kitaalamu kuhusu masuala ya vipimo kwa wadau
Kuhakikisha vifaa vyote vitumikavyo nchini vinakuwa na ulinganisho sahihi na ule wa Kimataifa.
FAIDA ZA KUTUMIA VIPIMO KATIKA SEKTA YA USAFIRISHAJI
A: Kuna faida mbalimbali zinazopatikana kwa kutumia vipimo vya uzito katika sekta ya usafirishaji, baadhi ya faida hizo ni pamoja na:-
B: Vipimo vya kupimia mafuta na gesi (Volume Measurements)
Vyombo vingi vya usafiri ili viweze kusafiri kutoka sehemu moja kwenda nyingine huhitaji nguvu yaani mafuta au gesi. Mafuta au gesi hutolewa kwa vipimo sahihi ili kuhakikisha chombo kinafika sehemu sahihi kulingana na kiasi cha mafuta/gesi iliyochukuliwa kituoni. Vipimo ambavyo vyombo vya usafiri (Ndege, Mabasi, Magari) huchukuwa mafuta/gesi ni Vituo vya mafuta (Dispensing pumps) na Flow meters.
Jaribu kufikiri kwa mfano ndege inaondoka ikiwa imepakia abiria pamoja na mizigo na imejaza mafuta yakiwa pungufu yaani haijazingatia matumizi sahihi ya vipimo ni dhahiri itakapokuwa angani itaishiwa mafuta, hivyo usalama wake na wa abiria utakuwa mashakani. Hivyo, Vipimo vina umuhimu mkubwa sana katika sekta ya usafiri.
C. Kipimo cha kupima mwendokasi (Speed Measuring Device)
Speed measuring device ni kifaa kinachotumika na Traffic kupima speed (Mwendo kasi) wa magari yanayo tembea barabarani. Kifaa hicho hupima na kurekodi mwendokasi wa gari linalokimbia barabarani. Faida ya kutumia vifaa hivi vya kudhibiti mwendokasi ni dhahiri, mojawapo ikiwa ni kudhibiti ajali barabarani.
D. Vipimo vingine katika sekta ya usafiri ambavyo Wakala wa Vipimo ipo kwenye mchakato wa kuvihakiki ni taximeter pamoja na tyre pressure gauge.
CHANGAMOTO
Upungufu wa watumishi na vitendea kazi katika kufanya shughuli za vipimo.
Uelewa mdogo wa sheria za vipimo kwa jamii ya wafanyabiashara na wananchi.
Kuwepo kwa mizani mingi batili na isiyokuwa na ubora sahihi inayoingizwa nchini kinyemela na baadhi ya wafanyabiashara wasio waaminifu. Changamoto hii inasababishwa na uhaba wa mizani nchini na hata ile michache inayopatikana/ kuagizwa toka nje ni ghali kwa wananchi wa kawaida kumudu.
Hivyo tukiwa tunaadhimisha Siku ya Vipimo Duniani ambayo mwaka huu imejikita katika Sekta ya Usafirishaji, ni vyema tukatambua kuwa umuhimu wa Vipimo sahihi uko katika kila sekta ya maisha yetu hapa nchini. Baadhi ya sekta hizo ni kama Biashara, Afya, Usalama, Mazingira na nyingine nyingi. Ni wajibu wetu pia kutambua kuwa Wakala wa Vipimo ndio iliyopewa majukumu haya muhimu ya kumlinda mwananchi katika harakati zake za kujenga uchumi.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.