Mamlaka ya hali ya Hewa nchini imetoa utabiri wa hali ya hewa kwa nchi nzima kwa kipindi cha Miezi mitatu, kwa mujibu wa utabiri huo mikoa ya kanda ya ziwa, ukiwemo mkoa wa Mwanza, inatarajiwa kupata mvua za wastani hadi juu ya wastani.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na mamlaka ya Hali ya hewa nchini kwa vyombo vya habari na kusainiwa na Mkurugenzi Mkuu Dkt. Agnes Kijazi inaonesha ukanda wa Ziwa Victoria mvua za kipindi cha Machi hadi Mei 2017 zinatarajiwa kuwa za wastani hadi juu ya wastani katika maeneo ya Ziwa Viktoria. Baadhi ya maeneo ya mikoa ya Mwanza, Mara, Shinyanga, Kagera, Geita na Simiyu mvua zinazoendelea kunyesha zikitarajiwa kuungana na mvua za msimu na kusambaa katika maeneo mengine ya nchi.
Kijazi amesema, uchambuzi wa mwenendo wa mifumo ya hali ya hewa na mwelekeo wa msimu wa mvua katika kipindi cha Machi hadi Mei 2017, umekwenda sambamba na ushauri pamoja na tahadhari kwa wadau wa sekta mbali mbali wanaohitaji taarifa za hali ya hewa katika utekelezaji wa majukumu yao kama vile kilimo na usalama wa chakula, mifugo na wanyamapori, maliasili na utalii, nishati na maji, mamlaka za miji, afya pamoja na menejimenti za maafa.
Ameongeza kuwa, Mwelekeo wa mvua uliotolewa umezingatia zaidi kipindi cha msimu (miezi mitatu mitatu) na hali ya mvua katika maeneo makubwa, amesema, viashiria vinavyochangia mwenendo wa mifumo ya hali ya hewa na mabadiliko ya muda mfupi katika maeneo madogo utazingatiwa katika uchambuzi wa utabiri wa muda wa mfupi na ule wa kati.
Sambamba na hilo taarifa hiyo pia imewashauri watumiaji wa taarifa za utabiri wa hali ya hewa wakiwapo wananchi kufuatilia tabiri zitolewazo na mamlaka kila baada ya saa 24, siku 10 pamoja na zile za kila mwezi.
NB.Juu yakujua Masuala ya hali ya hewa kwa Nchi nzima, ingia katika Eneo la Maktaba la Mtandao huu.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.