Tanzania imezishauri Mataifa yanayounda Bonde la Ziwa Victoria kuunganisha pamoja nguvu ya rasilimali fedha na watu katika kuhifadhi, kulinda na kuendeleza Ziwa Victoria kwa matumizi endelevu.
Wito huo ulitolewa juma lililopita jijini Mwanza na Makamu wa Rais, Mhe. Samia Suluhu Hassan alipokuwa akizinduzi kongamano la utafiti wa kisayansi wa bonde la Ziwa Victoria unaohudhuriwa na wataalam kutoka Kenya, Uganda, Rwanda Burundi na wenyeji Tanzania.
Makamu amesema tafiti za kisayansi ndizo zitaleta mwanga wa namna ya kulinza na ziwa hilo linaloangamia kutokana na mabadiliko ya nchi.
Amezitaka nchi wanachama kushirikiana kwa pamoja ili kuondoa changamoto zinazolikabiili Ziwa hilo ambalo linachangia kwa kiasi kikubwa ongezeko la ajira kwa vijana pamoja na ongezeko la uchumi kwa mataifa husika.
“Kuwa na rasilimali kama hili la Ziwa Victoria ni kulifanya liwe endelevu kwa vizazi vijavyo, kwahiyo ndio maana wameshilikishwa wataalam kubaini changamoto hizo mfano suala la gugu maji linapunguza kwa kiasi kikubwa kina cha maji,”alinukuliwa makamu wa Rais.
Pia alisema changamoto nyingine ni uvuvi haramu pamoja na shughuli zinazofanywa pembezoni mwa Ziwa hilo zinachangia kupunguza kina cha maji, jambo la msingi ni kuwasaidia watu hao na kuwatafutia shughuli maeneo mengine yakufanyia shughuli hizo.
Kwa upande wake katibu Mtendaji wa kamisheni ya bonde la Ziwa Victoria, Ally Matano, amesema, lengo mahususi wa mkutano huo ni kuwaleta wanasayansi ambao wamefanya kazi kwa miaka mingi katika bonde hilo kujadiliana kwa pamoja na kujua changamoto zinazolikumba ziwa.
Ukweli ni kuwa changamoto za Ziwa hilo zinazidi kuongezeka hivyo wanasayansi hao wamefanya tafiti lakini hazijajadiliwa na wadau ambapo zaidi ya tafiti 47 zimefanyika katika vipindi tofauti lakini hajaweza kujadiliwa.
pamoja na changamoto hizo lakini bado kuna tatizo la ongezeko la magugu maji, uchafuzi wa maji, masuala ya rasilimali pia athari za mabadiliko ya anga katika maendeleo endelevu.
“Ukiangalia nchi zingine zinatenga asilimia moja au mbili za kufanya utafiti lakini kwa Tanzania suala hilo halijafikiwa, hivyo ni muda mwafaka kwa wadau kujadili suala hilo na kuona jambo la kufanya kabla hatujaanza mradi mwingine wa awamu ya tatu ya mradi wa utunzaji wa Mazingira,”alisema Matano
“Miaka iliyopita kumekuwa na gape kubwa sana baina ya wanasiasa na watafiti njia moja ya kuwaleta pamoja ni kuwaleta pamoja watu hao katika kutengeneza sera ili zisikizane,”aliongeza Matano.
Hata hivyo, Dk Matano alisema pamoja na changamoto hizo, zipo taasisi za kifedha zinazosaidia kufadhili mradi huo ili kuimarisha shughuli za ziwa huku akizitaja benki ya dunia,lakini pia benki ya serikali ya ujerumani, na benki ya Afrika katika kuimarisha wa maendeleo endelevu ambapo hivi sasa wanatarajia kufadhili zaidi ya Dolla 65,000kwa ajili ya safiri ziwani, usimamizi wa maji na uharamia wa majini.
Akizungumza katika mkutano huo waziri wa mambo ya nje na ushirikiano wa kimataifa, Dk Augustine Mahiga alisema ili kuweza kufikia azma yao ya kutunza mazingira, nchi wananchama wanatakaiwa kuwa na silaha tatu ambazo ni Siasa safi, Utifiti wa kisayansi na elimu ya utunzaji wa Mazingira.
Wakizungumzia mkutano huo baadhi ya washiriki waliwataka wananchi wanachama wa ziwa hilo kuwa na mrengo unao fanana katika kukabiliana na changamoto za Ziwa hilo.“Mfano wanawaze wakakubaliana kukomesha uvuvi haramu au kuondoa gugu maji lakini, Tanzania pekee ikafanya huku zingine zikashindwa kushiriki,”alisema Sami Abbath mshiriki kutoka Tanzania.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.