Mkoa wa Mwanza, umetenga jumla ya Bilioni 24. 6 kwa ajili ya matumizi ya kawaida, huku Halmashauri zikielekezwa kutenga asilimia arobaini ya makusanyo ya ndani kwa ajili ya kuongezea katika matumizi ya kawaida.
Akizungumza na tovuti ya mkoa, Katibu Tawala msaidizi wa mipango na uratibu Bibi Isabella Marick, amesema Bilion 1.6 zimetengwa kwa ajili ya ngazi ya mkoa na Bilioni 22.9 ni kwa ajili ya Halmashauri za Mkoa huo.
Marick amesema Mkoa hadi hivi sasa bado mkoa haujatengewa fedha za miradi huku akiahidi ukweli wa juu ya fedha za miradi kutambulika mara baada ya kikao cha bajeti cha tarehe 05/3/2016 kitakacho keti jijini Dar es salaam.
Marick amesema, fedha hizo kiasi cha fedha Bilioni 1.673,948,000, sawa na ongezeko la milioni 40 kutoka bajeti ya mwaka uliopita ambao ngazi ya Mkoa kwa maana ya (RS), ulitengewa mwaka uliopita ambazo ni Bilioni 1,635, 244,000 za matumizi ya kawaida (OC) zitawezesha kuendesha shughuli za ngazi ya Sekretarieti ya mkoa kufanyika kama zilivyopangwa.
Ameongeza kuwa, kwa upande wa Halmashauri za Wilaya za Mkoa wa Mwanza, ambazo zipo nane, zimetengewa Bilioni 22,928,078,000, kwa ujumla wake kama fedha za matumizi ya kawaida yaani (OC), hata hivyo pamoja na Wilaya kutengewa fedha hizo na hazina, vilevile zimeelekezwa kutengwa asilimia 40 ya mapato ya ndani yaani (own sources) kwa ajili ya kusaidia kuongezea katika matumizi ya kawaida ya bajeti za halmashauri.
Sambamba na suala la bajeti ya matumizi ya kawaida, Marick ameeleza pia Miradi ambayo Mkoa unatarajia kuitekeleza katika kipindi cha 2017/2018, kwaajili ya mkoa wa mwanza kwakusema, miradi hiyo inayotarajia kutekelezwa katika ngazi ya Mkoa, kuwa ni ujenzi wa Jengo la Ghorofa la Hospitali ya Rufaa ya Mkoa, Nyumba mpya ya Mkuu wa Wilaya Ilemela, ukarabati wa nyumba ya Mkuu wa Wilaya Ukerewe, miradi mingine ni ujenzi wa nyumba ya Mkuu wa Mkoa, na uendelezaji ujenzi katika Ofisi ya Wilaya ya Nyamagana.
Aidha kuhusu kikao cha kamati ya ushauri cha Mkoa, Marick amesema, maandalizi yote yapo tayari kwa ajili ya kikao hicho kitakacho fanyika siku tarehe 09 Machi 2017 katika Ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa mkoa na wajumbe wa kikao wote walisha pelekewa mialiko, pamoja na mambo mengine. Kikao hicho pia kitatumika kupitisha bajeti ya Mkoa wa Mwanza kwa mwaka 2017/2018.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.