• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
Mwanza Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Mwanza

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia ya Mkoa
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti Mkoa
    • Seksheni
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Serikali za Mitaa
      • Afya
      • Elimu
      • Maji
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa Ndani
      • ununuzi na Ugavi
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Kitengo cha Sheria
  • Wilaya
    • Ilemela
    • Nyamagana
    • Magu
    • Misungwi
    • Kwimba
    • Sengerema
    • Ukerewe
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Jiji la Mwanza
    • Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
    • Hamashauri ya Wilaya ya Magu
    • Hamashauri ya Wilaya ya Sengerema
    • Hamashauri ya Wilaya ya Misungwi
    • Hamashauri ya Wilaya ya Kwimba
    • Hamashauri ya Wilaya ya Ukerewe
    • Hamashauri ya Wilaya ya Buchosa
  • Fursa za uwekezaji
    • Miundombinu ya Umwagiliaji na kilimo cha mkataba
    • Kilimo
    • Madini
    • Sekta ya Huduma
  • Huduma zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Watumishi
  • Machapisho
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa Kwa vyombo vya habari
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya video

“Wafichueni wahujumu wa ATCL”- Kamwelwe

Posted on: July 13th, 2018

  

“Nimekutana na bomu na maajabu hapa Mwanza” ndiyo kauli ya Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isack Kamwelwe aliyoitoa jana wakati akizungumza na waandishi wa habari na Wakuu wa idara zote zilizo chini yake katika kikao cha majumuisho ya ziara yake mkoani Mwanza.

Waziri Kamwelwe alisema licha ya mambo makubwa ya maendeleo kufanyika lakini bado baadhi ya maeneo yanatia shaka, uzembe na kuwa na dalili za uhujumu uchumi hususan katika Shirika la Ndege Tanzania (ATCL) na reli, kwanini wahujumu hawa wasifichuliwe hatua zikachukuliwa dhidi yao.

Mhe. Kamwelwe ameongeza kuwa, dreamline  ni ndege kubwa inatua viwanja vine tu hapa Tanzania kikiwamo cha Mwanza ingawa kuna mambo ya kurekebisha haraka kabla ya kutua hapa Julai 29, mwaka huu lakini nisema wazi nimekutana na maajabu katika ukataji wa tiketi, yaani ATCL haina dirisha maalum la kukata tiketi zake badala yake wanatumia mawakala.

“Mawakala wale hawana ofisi bali wana vibanda tu, haitoshi bei ya tiketi ya chini kabisa inakatwa zaidi ya 400,000 wakati sisi tulielekeza iwe Sh 190,000, vile vile mawakla wale inaelezwa wana mikataba ya ajira na kampuni nyingine, kwa hiyo hapo kuna hali ya kuhujumu ndege zetu na shirika likafa tena,”alisema Kamwelwe.

Alisema moja ya maeneo ambayo hakuridhika nayo ni namna ya ukataji wa tiketi za abiria unavyofanyika kwa kuwatumia mawakala ambao hawana ofisi maalum ispokuwa wanatumia vibanda huku bei elekezi ya chini kabisa kwa ndege za shirika hilo ni Sh 190,000 lakini wao huongeza na kufikia kiasi cha  Shilingi  400,000 na 450,000.

“Serikali ya awamu ya tano ilipoingia madarakani ilikuta shirika hili halipo hai lakini leo hii limefufuliwa na kuwa na ndege zake ambapo juzi tumeshuhudia tukipokea ndege kubwa ya dreamline yenye uwezo wa kubeba abiria zaidi ya 260, pia tunazo ndege za bombardier tatu.

Waziri Kamwelwe aliwataka viongozi wanaohusika kumpa maelezo ya kina juu ya bei hizo kabla ya kuchukua hatua zaidi ambapo ameelekeza kufanyika haraka mfumo wa uboreshaji na uthibiti wa ukataji tiketi.

“Kuna hali ya hujuma na hatuwezi kubembelezana katika suala hilo na sipo tayari kuona jitihada za Rais Dk. John Magufuli zinakwamishwa na watu wachache, naomba mfumo huo uanzishwe ndani ya wiki mbili, naweza kuchukua hatua muda huu baadaye mkanilaumu mimi ndiye nimewaingilia ndiyo maana nimesema nahitaji maelezo kwanza,”alisema Kamwelwe.

Matangazo

  • WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA KIDATO CHA KWANZA MKOA WA MWANZA MWAKA 2021 December 18, 2020
  • Matokeo ya Uchaguzi wa Wanafunzi Waliochaguliwa Kujiunga na Kidato cha Kwanza 2018 Shule za Sekondari za Serikali Mkoa wa Mwanza December 13, 2017
  • Ziara ya Mhe. Mkuu wa Mkoa kwa ajili ya kufanya ufuatiliaji katika shule za Msingi na Sekondari Mkoa wa Mwanza 2018 January 10, 2018
  • Ufunguzi wa Mashindano ya UMISSETA na UMITASHUMTA Kitaifa Mkoa wa Mwanza. June 07, 2018
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • AGA KHAN Yatoa Vifaa vya Bilioni 1.5 Kuepusha vifo vya mama na mtoto Mwanza

    December 22, 2020
  • Kikao cha bodi ya Barbara chapanga mikakati ya mafanikio Mwanza

    December 21, 2020
  • Mwanza Kwanza Toleo la pili kwa habari mbalimbali Mkoa wa Mwanza

    December 12, 2020
  • Elimu ya maadili yatolewa Mwanza kwa Viongozi

    December 10, 2020
  • Angalia zote

Video zinazotembea

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe.John Mongella akifungua Baraza la biashara katika kikao kilichofanyika kwenye ukumbi wa mkikutano uliopo katika ofisi ya Mkoa uliojumuisha wajumbe mbalimbali wa Baraza hilo wa Mkoa wa Mwanza.
video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Fomu ya Ugonjwa
  • FFARS User Guidelines
  • Miongozo ya mfumo wa bajeti na Mipango
  • Makusanyo ya Ndani ya Halmashauri za Mkoa wa Mwanza
  • PReM
  • Maswali Yaulizwayo Mara kwa Mara
  • Opras fomu
  • OFISI MTANDAO

Viunganishi Linganishi

  • Tovuti ya Ikulu
  • Utumishi
  • Tamisemi
  • Ofisi ya Taifa ya Takwimu Tanzania
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Kuu ya Serikali

Watembeleaji

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    Regional Drive Mkabala na Ofisi za TRA

    S.L.P: S.L.P. 119, Mwanza.

    Simu: 028-2501037

    Simu ya Mkononi: 028-2501037

    Barua Pepe: ras.mwanza@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.