Wauguzi katika Mkoa wa Mwanza wametakiwa kuwa mstari wa mbele katika kuwahudumia wanachi, ili taifa liwe na Nguvu kazi itakayosaidia kukuza uchumi wan chi.
Akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa mkoa wa Mwanza mkoani hapa, Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana, Mhe. Mary Tesha Onesmo, amesema wauguzi ni jeshi kubwa katika suala zima la afya za Watanzania,
“Rai yangu kwenu, ni kuongeza kasi na ufanisi wa kazi ili kuboresha afya za watanzania. Ninaamini wauguzi ndio jeshi pekee lenye watu wengi walio mstari wa mbele katika sekta ya afya, (takribani asilimia 60 ya watumishi wote wa afya) ni wauguzi” amesema Tesha na Kuongeza.
“Kwa mantiki hiyo naamini mna uwezo wa kufikia azma hii, hivyo tuungane na sekta zingine nchini ili taifa liweze kufikia shabaha iliyokusudiwa kwa kuwaweka watu wetu kwenye afya bora”.
Kwa upande wao wauguzi katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mwanza Sekouture, wao wameahidi kufanya kazi kwakuzingatia viapo ambavyo ndio msingi mkubwa wa taaluma yao. Bibi Frida Mwaipopo ambaye ni Katibu wa Chama cha Wauguzi mkoani hapa, amesema wanajisikia fahari katika siku hiyo ambayo iliasisiwa na Frolence Nightingale, aliyewahudumia Majeruhi wa vita kwakutimia Kandili wakati wa vita huko Ujerumani.
Akizungumza kabla ya Maadhimisho hayo Mganga mfawidhi wa Hospitali hiyo, Onesmo Rwakyendera, tofauti na ilipokuwa hapo kabla, huduma katika hospitali hiyo zimeimarika sana. “Miaka saba iliyopita wakati nafika hapa ulikuwa ukiangalia utadhani kituo cha afya, tulikuwa na daktari kamili mmoja na Daktari Bingwa mmoja, hadi hivi sasa wenyewe mnaona kuna mabadiliko makubwa sana, hatuna budi kuipongeza Serikali katika kujali watu wake”, alisema Rwakyendera.
Katika hatuanyingine Katibu wa Hospitali hiyo, Danny Temba, amesema suala la Upungufu wa dawa kwenye hospitali hiyo ya Mkoa kwa sasa limeisha,“Tuna zaidi ya Milioni tisa kwa wenzetu wa MSD ambazo zinangoja kwenda kuchukua tu dawa hii nitofauti na huko nyuma” amesema Temba na kusema Wanamshukuru sana Mhe. Rais kwakujali afya za Watanzania.
Naye kaimu Mganga mkuu, awali akimkaribisha Mgeni rasmi kuzungumza alisema kila mmoja ajitathmini juu ya utendaji wake “Niwaombe kiapo tulichokula leo kila mmoja kwa nafsi yake ajihoji yeye mwenyewe”.
Siku ya wauguzi kwa mwaka 2017 ilibebwa na Kaulimbiu. Wauguzi: Mbiu ya Kuyafikia Malengo Endelevu ya Milenia).
Ambayo inawahimiza wauguzi kutenda kwa umahili na kuweza kufikia malengo ya millennia na masuala mazima ya uchumi wa Viwanda.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 33180, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras.mwanza@tamisemi.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.