• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
Mwanza Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Mwanza

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia ya Mkoa
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti Mkoa
    • Seksheni
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Serikali za Mitaa
      • Afya
      • Elimu
      • Maji
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa Ndani
      • ununuzi na Ugavi
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Kitengo cha Sheria
  • Wilaya
    • Ilemela
    • Nyamagana
    • Magu
    • Misungwi
    • Kwimba
    • Sengerema
    • Ukerewe
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Jiji la Mwanza
    • Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
    • Hamashauri ya Wilaya ya Magu
    • Hamashauri ya Wilaya ya Sengerema
    • Hamashauri ya Wilaya ya Misungwi
    • Hamashauri ya Wilaya ya Kwimba
    • Hamashauri ya Wilaya ya Ukerewe
    • Hamashauri ya Wilaya ya Buchosa
  • Fursa za uwekezaji
    • Miundombinu ya Umwagiliaji na kilimo cha mkataba
    • Kilimo
    • Madini
    • Sekta ya Huduma
  • Huduma zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Watumishi
  • Machapisho
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa Kwa vyombo vya habari
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya video

Waziri Jaffo asisitiza ukusanyaji wa mapato

Posted on: October 22nd, 2018

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI)Mhe. Suleiman Jaffo amewataka watendaji kuongeza  kasi ya ukusanyaji wa mapato wa Manispaa ya Ilemela, ambayo ni miongoni mwa manispaa zenye vyanzo vingi vya mapato.

Jaffo ameyasema hayo wakati alipokuwa akizungumza na watendaji na wafanyakazi wa Manispaa ya Ilemela ambapo alipata fursa ya kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo ujenzi wa miundombinu ya afya na barabara ambayo inatekelezwa chini ya Wizara yake,  wakati wa ziara yake ya kikazi ya siku moja katika manispaa hiyo.


Kwenye mkutano wake na watumishi wa manispaa hiyo, Jaffo aliwasimamisha Mchumi wa Manispaa hiyo Amosy Zephania na Mtunza Hazina wa Manispaa hiyo Jamea Dalasia ili  kueleza mikakati waliyoweka kuhakikisha nakusanya mapato na kufikia malengo waliyoweka kama Manispaa.

“ Kwenye suala la ukusanyaji wa mapato, nilichokigundua kwa baadhi ya maeneo mengi ni uzembe wa baadhi ya watumishi na msikubali mtu mmoja akawaharibia kazi”, alisema Mhe.Jaffo.

Alimtaka Mkurugenzi Mtendaji wa manispaa ya Ilemela John Wanga kuwa mkali na kuhakikisha kuwa anawachukulia hatua kali baadhi ya watumishi walio chini yake wenye malengo ya kukwamisha juhudi za ukusanyaji wa mapato.

“ Kamati ya fedha na mipango simamieni vizuri  ukusanyaji wa mapato ya manispaa yenu, makosa ya mtu mmoja yanaweza kusababisha manispaa yenu kusemwa vibaya,"alisema Mhe.Jaffo.

“ Unapoona manispaa yenu inasemwa vibaya, maana yake unaharibu jina la Mkuu wa Mkoa, Mkuu wenu wa wilaya na kamati nzima ya fedha,tubadilike na tuache kufanya kazi kwa mazoea."


Katika hatua nyingine Jaffo alimpongeza Mkurugenzi Mtendaji wa manispaa hiyo John Wanga kwa kufanya maboresho ya ukusanyaji wa mapato kwenye Soko la Kimataifa la Mwaloni ambapo makusanyo yamepanda kutoka Sh milioni 34 hadi kufikia Sh. milioni 54  katika kipindi cha kuanzia Oktoba mosi hadi Oktoba 21 mwaka huu.

 Kwa mujibu wa Wanga, ufanisi huo wa ukusanyaji wa mapato katika soko hilo, umetokana na manispaa hiyo kununua mizani ya kisasa ya kupimia mazao ya samaki, hali ambayo imeongeza mapato hayo maradufu.

Matangazo

  • WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA KIDATO CHA KWANZA MKOA WA MWANZA MWAKA 2021 December 18, 2020
  • Matokeo ya Uchaguzi wa Wanafunzi Waliochaguliwa Kujiunga na Kidato cha Kwanza 2018 Shule za Sekondari za Serikali Mkoa wa Mwanza December 13, 2017
  • Ziara ya Mhe. Mkuu wa Mkoa kwa ajili ya kufanya ufuatiliaji katika shule za Msingi na Sekondari Mkoa wa Mwanza 2018 January 10, 2018
  • Ufunguzi wa Mashindano ya UMISSETA na UMITASHUMTA Kitaifa Mkoa wa Mwanza. June 07, 2018
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • AGA KHAN Yatoa Vifaa vya Bilioni 1.5 Kuepusha vifo vya mama na mtoto Mwanza

    December 22, 2020
  • Kikao cha bodi ya Barbara chapanga mikakati ya mafanikio Mwanza

    December 21, 2020
  • Mwanza Kwanza Toleo la pili kwa habari mbalimbali Mkoa wa Mwanza

    December 12, 2020
  • Elimu ya maadili yatolewa Mwanza kwa Viongozi

    December 10, 2020
  • Angalia zote

Video zinazotembea

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe.John Mongella akifungua Baraza la biashara katika kikao kilichofanyika kwenye ukumbi wa mkikutano uliopo katika ofisi ya Mkoa uliojumuisha wajumbe mbalimbali wa Baraza hilo wa Mkoa wa Mwanza.
video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Fomu ya Ugonjwa
  • FFARS User Guidelines
  • Miongozo ya mfumo wa bajeti na Mipango
  • Makusanyo ya Ndani ya Halmashauri za Mkoa wa Mwanza
  • PReM
  • Maswali Yaulizwayo Mara kwa Mara
  • Opras fomu
  • OFISI MTANDAO

Viunganishi Linganishi

  • Tovuti ya Ikulu
  • Utumishi
  • Tamisemi
  • Ofisi ya Taifa ya Takwimu Tanzania
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Kuu ya Serikali

Watembeleaji

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    Regional Drive Mkabala na Ofisi za TRA

    S.L.P: S.L.P. 119, Mwanza.

    Simu: 028-2501037

    Simu ya Mkononi: 028-2501037

    Barua Pepe: ras.mwanza@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.