Wednesday 23rd, April 2025
@Tanzania
Hayati Baba wa Taifa , Mwalimu Julius Kambarage Nyerere alizaliwa Mwaka 1922 katika kijiji cha Butiama, wilaya ya Musoma, Mkoa wa Mara, Tanzania (wakati ule ilikuwa Tanganyika). Ifikapo tarehe 14/10/2020 atakuwa anafikisha miaka 21 tangu atangulie mbele za haki huku Taifa na vizazi vyake vikiendelea na kumbukumbu ya kifo chake na kumuenzi.
Kitaifa Maadhimisho hayo huambatana na sherehe za kilele cha Mbio za Mwenge wa Uhuru, Mgeni rasmi atakuwa Mh. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli.
Mwalimu Nyerere alikuwa na uwezo wa kuona mbali, hata alipopingwa baadaye waliompinga walikiri ukweli wa maono yake. Ni dhahiri kwamba Mwalimu Nyerere anakumbukwa kwa Mambo mengi ya msingi aliyoyapa kipaumbele wakati wa uongozi wake. jambo mojawapo alilolisema julai 29/07/1985, kwamba "kazi iliyokuwa muhimu kuliko zote kwangu Mimi , ilikuwa ni kujenga Taifa lenye umoja kwa msingi wa heshima na usawa wa Binadamu." Mwenyezi Mungu Mrehemu.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.