• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
Mwanza Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Mwanza

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia ya Mkoa
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti Mkoa
    • Seksheni
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Serikali za Mitaa
      • Afya
      • Elimu
      • Maji
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa Ndani
      • ununuzi na Ugavi
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Kitengo cha Sheria
  • Wilaya
    • Ilemela
    • Nyamagana
    • Magu
    • Misungwi
    • Kwimba
    • Sengerema
    • Ukerewe
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Jiji la Mwanza
    • Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
    • Hamashauri ya Wilaya ya Magu
    • Hamashauri ya Wilaya ya Sengerema
    • Hamashauri ya Wilaya ya Misungwi
    • Hamashauri ya Wilaya ya Kwimba
    • Hamashauri ya Wilaya ya Ukerewe
    • Hamashauri ya Wilaya ya Buchosa
  • Fursa za uwekezaji
    • Miundombinu ya Umwagiliaji na kilimo cha mkataba
    • Kilimo
    • Madini
    • Sekta ya Huduma
  • Huduma zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Watumishi
  • Machapisho
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa Kwa vyombo vya habari
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya video

Historia ya Mkoa

Ndugu Msomaji karibu katika Tovuti rasmi ya Mkoa wa Mwanza. Historia ya mkoa wa Mwanza ilianza wakati ukiwa chini ya tawala za kitemi za wasukuma, wazinza, walongo, wakara na wakerewe kabla ya ukoloni.  Wajerumani walipotawala Tanganyika eneo la Mwanza likawa mojawapo ya wilaya katika himaya ya utawala wa Kijerumani.

 Utawala wa kikoloni wa Mwingereza ulipokabidhiwa uangalizi wa Koloni la Afrika Mashariki baada ya vita kuu ya Dunia, ulianzisha utawala wa majimbo yaani Provinces. Tanganyika ilikuwa na majimbo ya kiutawala manane (8)  na mojawapo likiwa ni Lake Province. 

 Lake Province liliundwa kwa kujumuisha maeneo ya wilaya za Mwanza, Biharamulo, Bukoba, Maswa, shinyanga, Musoma na Kwimba. Baadaye Lake Province liligawanywa na kuunda majimbo mawili la Lake Province (Sukuma Land) na Western Province). Utawala wa Mwingereza ulimalizika na Tanganyika kupata uhuru mwaka 1961.

 Baada ya uhuru Mwanza iliendelea kuwa sehemu ya Jimbo la Lake Province chini ya mtawala wake kwanza wa jimbo (Provincial Commissioner) aliyeitwa Provincial Commissioner Bw. Walden, ambaye alikabidhi madaraka kwa Richard Wambura. 

Mkoa wa Mwanza ulianzishwa rasmi mwaka 1963 ukiwa na wilaya nne za Ukerewe, Geita, Mwanza na Kwimba. Mwaka 1972 baada ya sera ya madaraka mikoani wilaya zaidi zilianzishwa kwa kuanza na Magu mwaka 1974. Wilaya ya Sengerema ilianzishwa mwaka 1975 ambapo awali ilikuwa ni tarafa mojawapo ya wilaya ya Geita.

Misungwi ilianzishwa mwaka 1995 ambapo awali ilikuwa ni eneo la tarafa za wilaya ya Kwimba, Ilemela na Nyamagana zilianzishwa mwaka 2002 ambazo zilikuwa zinaunda wilaya ya Mwanza. Mwaka 2010 mikoa mipya ya Geita na Simiyu ilitangazwa kuanzishwa. Wilaya mpya pia za Busega na Nyanghwale nazo zilitangazwa kuanzishwa 2010 na utekelezaji wake utaanza rasmi wakati wowote katika mwaka wa fedha 2011/12.

Mkoa wa Mwanza ni kati ya mikoa 30 ya Tanzania.Mipaka ya Mkoa, Mkoa wa Mwanza unapakana  na Geita upande wa magharibi, Shinyanga na Simiyu upande wa kusini na Mara upande wa mashariki. Ziwa la Viktoria Nyanza liko kaskazini.


Idadi ya watu, kabla ya kumegwa na kuzaa mkoa mpya wa Geita, mkoa wa Mwanza ulikuwa na wakazi 2,942,148 (sensa ya mwaka  2002) katika wilaya 8 ukiwa na eneo la 19,592 km2. Wilaya ndizo Ukerewe,Magu, Sengerema,Geita,Misungwi,Kwimba,Nyamagana na Ilemela.  Jiji la Mwanza  ndani  yake lina  wilaya za Nyamagana na Ilemela.


Majimbo ya bunge
Wakati wa uchaguzi mkuu wa Tanzania mwaka 2015 mkoa huu ulikuwa na majimbo ya uchaguzi yafuatayo:

Buchosa : mbunge ni Dk. Charles Tizeba (CCM)
Ilemela : mbunge ni Angelina Mabula (CCM)
Kwimba : mbunge ni Mansoor Hirani (CCM)
Magu : mbunge ni Kiswaga Boniventura (CCM)
Misungwi : mbunge ni Charles Kitwanga (CCM)
Nyamagana : mbunge ni Stanslaus Mabula (CCM)
Sengerema : mbunge ni William Ngeleja (CCM)
Sumve : mbunge ni Richard Mganga Ndassa (CCM)
Ukerewe : mbunge ni Joseph Mkundi (Chadema)


Makao makuu ya mkoa yapo Mwanza mjini.

Makabila ya Mkoa wa Mwanza
Makabila makubwa katika Mwanza ni Wasukuma kwa wilya za Sengerema, Magu, Kwimba, Misungwi na Ilemela ili hali Wilaya ya Nyamagana wanaishi makabila tofauti tofauti na wilya ya Ukerewe hupatikana Wakerewe na na Wakara.


Historia ya Wakuu wa Mikoa na Makatibu Tawala walio wahi kuongoza Mkoa wa Mwanza

Wakuu wa Mikoa walioongoza Mkoa wa Mwanza toka 1961 hadi sasa.

NA
Jina Kamili
Mwaka alionza
Mwaka alioondoka
1.
Mhe. Richard Wambura
1961
1963
2.
Mhe. J Samwel Malecela
1963
1965
3.
Mhe.Joseph Nyerere
1965
1967
4.
Mhe.Joseph Namata
1967
1969
5.
Mhe.Omary Muhaji
1969
1972
6.
Mhe.Lawi Sijona
1972
1975
7.
Mhe.Peter Kisumo
1975
1977
8.
Mhe.Muhidin Kimario
1977
1979
9.
Mhe.Abdulnuru Suleiman
1979
1981
10.
Mhe.Daniel Machemba
1981
1987
11.
Mhe.Timoth Shindika
1987
1992
12.
Mhe.Philip Mangula
1992
1993
13.
Mhe.Ernest Nyanda
1993
1994
14.
Mhe.Dkt.William Shija
1994
1995
15.
Mhe.Mj. Gen.James Luhanga
1996
1999
16.
Mhe.Stephen Mashishanga
1999
2003
17.
Mhe.Daniel Ole Njolai
2003
2006
18.
Mhe.Dkt Eng.James Allex Msekela
2006
2009
19.
Mhe. Abbas H. Kandoro
2009
2011
20.
Mhe.Eng.Evarist W. Ndikilo 
2011
2014
21.
Mhe.Magessa S. Mulongo
2014
2016
22.
Mhe.John V.K Mongella
2016
2021
23.
Mhe. Albert Chalamila
2021
2021
24.
Mhe. Eng. Robert Gabriel
2021
Mpaka Sasa



Makatibu Tawala Walioongoza Mkoa wa Mwanza toka 1972 hadi sasa

NA.
Jina Kamili
Mwaka alioanza
Mwaka alioondoka
1.
C. Y.  Mpuya
1972
1975
2.
R. Ringo
1975
1977
3.
W. K. Kasera
1977
1981
4.
W. H. Shelukindo
1981
1983
5.
J. R. Kyambwa
1983
1984
6.
E. O. Oluoch
1984
1987
7.
M. D. Mapunda
1987
1990
8.
J. K. Kyambwa
1990
1995
9.
R. R. Kiravu
1995
1997
10.
C. M. Rutaihwa
1997
2006
11.
Alh. Y. Mbila
2006
2009
12.
Doroth S. Mwanyika
2009
2013
13.
D. Faisal H. H.  Issa
2014
2016
14.
C.P.Clodwig M. Mtweve
2016
2018
15. Christopher Derek Kadio 
2018 2020
16.
Emmanuel M. Tutuba
2020
2021
17.
Ngusa D. Samike
2021
Mpaka Sasa



Matangazo

  • Tangazo la kukutana na Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Mwanza kwa shida mbalimbali. July 29, 2022
  • TANGAZO LA NANENANE TAREHE 8.8.2022 July 03, 2022
  • TANGAZO LA KUITWA KAZINI ICAP October 21, 2022
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • Kamati ya Uwekezaji Yashauri Madini yote Yasafishwe Nchini kabla ya kusafirishwa nje

    March 26, 2023
  • Kamati ya Uwekezaji Yaridhishwa utekelezaji mradi wa Daraja la JPM*

    March 25, 2023
  • Mkoa wa Mwanza wachukua hatua kukabiliana na ugonjwa wa Marburg

    March 24, 2023
  • TAMISEMI ilivyotumia Wiki ya Kitaifa ya Usalama Barabarani Mkoani Mwanza kwa kutoa huduma mbalimbali kwa jamii

    March 22, 2023
  • Angalia zote

Video zinazotembea

Siku 365 za Mhe.Rais Samia Suluhu Hassan Mwanza
video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Fomu ya Ugonjwa
  • FFARS User Guidelines
  • Miongozo ya mfumo wa bajeti na Mipango
  • Makusanyo ya Ndani ya Halmashauri za Mkoa wa Mwanza
  • PReM
  • Maswali Yaulizwayo Mara kwa Mara
  • Opras fomu
  • OFISI MTANDAO

Viunganishi Linganishi

  • Tovuti ya Ikulu
  • Utumishi
  • Tamisemi
  • Ofisi ya Taifa ya Takwimu Tanzania
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Kuu ya Serikali

Watembeleaji

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive

    S.L.P: 33180, Mwanza.

    Simu: 028-2501037

    Simu ya Mkononi: 028-2501037

    Barua Pepe: ras.mwanza@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.