• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
Mwanza Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Mwanza

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia ya Mkoa
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti Mkoa
    • Seksheni
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Serikali za Mitaa
      • Afya
      • Elimu
      • Maji
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa Ndani
      • ununuzi na Ugavi
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Kitengo cha Sheria
  • Wilaya
    • Ilemela
    • Nyamagana
    • Magu
    • Misungwi
    • Kwimba
    • Sengerema
    • Ukerewe
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Jiji la Mwanza
    • Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
    • Hamashauri ya Wilaya ya Magu
    • Hamashauri ya Wilaya ya Sengerema
    • Hamashauri ya Wilaya ya Misungwi
    • Hamashauri ya Wilaya ya Kwimba
    • Hamashauri ya Wilaya ya Ukerewe
    • Hamashauri ya Wilaya ya Buchosa
  • Fursa za uwekezaji
    • Miundombinu ya Umwagiliaji na kilimo cha mkataba
    • Kilimo
    • Madini
    • Sekta ya Huduma
  • Huduma zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Watumishi
  • Machapisho
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa Kwa vyombo vya habari
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya video

ATCL yashauriwa kwenda na wakati ili wasafirishaji mizigo nje ya nchi wamudu soko la ushindani

Posted on: April 1st, 2023

**ATCL yashauriwa kwenda na wakati ili wasafirishaji wa mizigo nje ya nchi wamudu soko la ushindani.*


Wasafirishaji wa bidhaa za Tanzania nje ya nchi wameomba waendeshaji wa ndege ijayo ya mizigo kuzingatia muda wa kutoka nchini, ili waweze kumudu ushindani katika masoko ya dunia.


Wametoa wito huo leo Jijini Mwanza wakati  wa mkutano wa kukusanya maoni ya wadau uliondaliwa na shirika la ndege nchini (ATCL) ulioangazia juu ya nini kifanyike ili ndege hiyo ilete tija kwao na kwa nchi.

Ndege ya Shirika la ATCL aina ya B767-300F inatarajia kuwasili nchini wiki ijayo na ina uwezo wa kubeba tani 54.

Mhakiki Ubora Kampuni ya Victoria Perch inayosindika minofu ya samaki, Edwin Okong’o amesema inapotokea ndege ikachelewa hata kwa saa moja tu, tayari mteja wake huko nchi za Ulaya anapata hasara.

“Lakini hata sisi tunapoteza nafasi ya kushindana kibiashara. mara zote mteja wetu anaendana na ratiba ya mnada wa siku husika huko kwao, hivyo anapaswa kupokea mzigo kwa wakati ili auze ukiwa na ubora wa asili (fresh). Amesisitiza Okongo

Ameongeza kuwa usafirishaji wa mizigo unahitaji umakini na nidhamu ya hali ya juu ya kuzingatia muda tofauti na hapo wasafirishaji kutoka Tanzania wataonekana wababaishaji kwenye soko la Dunia.

Mkuu wa Mkoa  Mwanza Mhe.Adam Malima ameunga mkono hoja hiyo na wakati huohuo amewataka wafanyabiashara kuzingatia suala la ubora wa bidhaa zao  ili kumudu ushindani katika masoko ya kimataifa.

Ametolea mfano wa bidhaa za mifugo  hasa nyama  kwamba wazalishaji wanapaswa kuzingatia umri wa ng’ombe kuchinjwa, ambao si zaidi ya miaka miwili na nusu.

“Lakini pia muungane ninyi na wafanyabiashara wengine wa mikoa ya kanda ya ziwa, ili kuwe na mzigo wa uhakika kujaza ndege hiyo"RC Malima

Mtendaji Mkuu ATCL, Mhandisi Ladislaus Matindi, amebainisha  utakuwepo uhakika wa bidhaa za Tanzania kufika sokoni kwa wakati  kutokana na uwepo wa ndege ya serikali ya mizigo.

“Maana yake itakua ikiruka moja kwa moja kutoka nchini kwetu hadi mwisho wa safari ni tofauti na tulivyokua tukitegemea ndege za wenzetu nchi jirani".Amesema Mhanisi Matindi

Mbali na mazao ya uvuvi na mifugo, Matindi amesema ziko nchi nyingi zenye mahitaji ya mazao jamii ya kunde na maharage, lakini pia mbogamboga.

Matangazo

  • Tangazo la kukutana na Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Mwanza kwa shida mbalimbali. January 08, 2025
  • TANGAZO LA NANENANE TAREHE 8.8.2025 January 08, 2025
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • UZALISHAJI ZAO LA PAMBA WAONGEZEKA- MSIGWA

    May 03, 2025
  • DARAJA LA KIGONGO-BUSISI KUANZA KUTUMIKA MUDA WOWOTE KUANZIA SASA.

    May 02, 2025
  • SERIKALI YAANIKA TAKWIMU ZA MAENDELEO YA UTUMISHI YALIYOPATIKANA MWANZA

    May 01, 2025
  • MAKUNDI MAWILI YA MWISHO YALIYOFANYA ZIARA HIFADHI NA JNHPP YAWASILISHA NENO LA SHUKRANI KWA RAS BALANDYA

    April 29, 2025
  • Angalia zote

Video zinazotembea

Siku 365 za Mhe.Rais Samia Suluhu Hassan Mwanza
video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Fomu ya Ugonjwa
  • FFARS User Guidelines
  • Miongozo ya mfumo wa bajeti na Mipango
  • Makusanyo ya Ndani ya Halmashauri za Mkoa wa Mwanza
  • PReM
  • Maswali Yaulizwayo Mara kwa Mara
  • Opras fomu
  • OFISI MTANDAO

Viunganishi Linganishi

  • Tovuti ya Ikulu
  • Utumishi
  • Tamisemi
  • Ofisi ya Taifa ya Takwimu Tanzania
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Kuu ya Serikali

Watembeleaji

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive

    S.L.P: 119, Mwanza.

    Simu: 028-2501037

    Simu ya Mkononi: 028-2501037

    Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.