• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
Mwanza Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Mwanza

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia ya Mkoa
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti Mkoa
    • Seksheni
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Serikali za Mitaa
      • Afya
      • Elimu
      • Maji
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa Ndani
      • ununuzi na Ugavi
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Kitengo cha Sheria
  • Wilaya
    • Ilemela
    • Nyamagana
    • Magu
    • Misungwi
    • Kwimba
    • Sengerema
    • Ukerewe
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Jiji la Mwanza
    • Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
    • Hamashauri ya Wilaya ya Magu
    • Hamashauri ya Wilaya ya Sengerema
    • Hamashauri ya Wilaya ya Misungwi
    • Hamashauri ya Wilaya ya Kwimba
    • Hamashauri ya Wilaya ya Ukerewe
    • Hamashauri ya Wilaya ya Buchosa
  • Fursa za uwekezaji
    • Miundombinu ya Umwagiliaji na kilimo cha mkataba
    • Kilimo
    • Madini
    • Sekta ya Huduma
  • Huduma zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Watumishi
  • Machapisho
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa Kwa vyombo vya habari
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya video

RC Malima alishauri Baraza la Taifa la Usalama Barabarani kutazama upya adhabu zake kwa wakiukwaji wa Sheria

Posted on: January 25th, 2023

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe.Adam Malima amelishauri Baraza la Taifa la Usalama Barabarani kuangalia upya adhabu zake kwa wanaokiua Sheria kutokana na zilizopo kuonesha kupitwa na wakati.

Akizungumza na ujumbe wa Baraza hilo ulioongozwa na  Kamanda wa kikosi cha Usalama Barabarani Kamishna Msaidizi mwandamizi wa Polisi Ramadhan Ng'anzi, Mhe. Malima amesema kumekuwa na hali ya kutozingatia sheria zilizopo kutokana na watumiaji kuona wepesi wa adhabu husika.

"Unakuta mtu anatumia kilevi huku gari lake limebeba abiria na inapotokea amesabanisha ajali na kuuwa watu anaishia kuonekana uraiani na kulipa adhabu ndogo, hii siyo sawa". Amesisitiza Mkuu huyo wa Mkoa.

Mhe.Malima amebainisha kuwa amepania kuuweka Mkoa wa Mwanza kama mfano wa kutokuwa na ajali kutokana na sheria zote za barabarani kuziwekea mkakati wa kuheshiwa na watumiaji wake.

"Tutaanza na kuweka ujumbe mahususi kwenye mabango yatayowekwa kwenye barabara kuu zote zinazoingia Mkoani Mwanza zinazowataka watumiaji kuzingatia sheria zote husika".Mhe Malima

Amesema,  amepoke kwa dhati  maamuzi ya kuufanya Mkoa wa Mwanza kuwa mwenyeji wa Sherehe za Kitaifa za Usalama Barabarani ambapo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Rais wa Zanzibar Mhe. Dkt Hussein Mwinyi.

Kwa upande wake Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani Kamishna Msaidizi mwandamizi Ramadhan Ng'anzi amesema mchakato wa marekebisho ya adhabu kwa wanaokwenda kinyume upo mbioni kufanyiwa kazi.

Sherehe za Kitaifa za Usalama Barabarani zitafanyika kuanzia tarehe 13 hadi 17 Machi mwaka huu Mkoani Mwanza zikitanguliwa na wiki ya Usalama Barabarani ambapo elimu mbalimbali zitatolewa kuhusiana vyombo vya moto vitumikavyo eneo hilo na haki ya mwenda kwa miguuu.

Matangazo

  • Tangazo la kukutana na Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Mwanza kwa shida mbalimbali. January 08, 2025
  • TANGAZO LA NANENANE TAREHE 8.8.2025 January 08, 2025
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • UZALISHAJI ZAO LA PAMBA WAONGEZEKA- MSIGWA

    May 03, 2025
  • DARAJA LA KIGONGO-BUSISI KUANZA KUTUMIKA MUDA WOWOTE KUANZIA SASA.

    May 02, 2025
  • SERIKALI YAANIKA TAKWIMU ZA MAENDELEO YA UTUMISHI YALIYOPATIKANA MWANZA

    May 01, 2025
  • MAKUNDI MAWILI YA MWISHO YALIYOFANYA ZIARA HIFADHI NA JNHPP YAWASILISHA NENO LA SHUKRANI KWA RAS BALANDYA

    April 29, 2025
  • Angalia zote

Video zinazotembea

Siku 365 za Mhe.Rais Samia Suluhu Hassan Mwanza
video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Fomu ya Ugonjwa
  • FFARS User Guidelines
  • Miongozo ya mfumo wa bajeti na Mipango
  • Makusanyo ya Ndani ya Halmashauri za Mkoa wa Mwanza
  • PReM
  • Maswali Yaulizwayo Mara kwa Mara
  • Opras fomu
  • OFISI MTANDAO

Viunganishi Linganishi

  • Tovuti ya Ikulu
  • Utumishi
  • Tamisemi
  • Ofisi ya Taifa ya Takwimu Tanzania
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Kuu ya Serikali

Watembeleaji

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive

    S.L.P: 119, Mwanza.

    Simu: 028-2501037

    Simu ya Mkononi: 028-2501037

    Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.