• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
Mwanza Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Mwanza

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia ya Mkoa
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti Mkoa
    • Seksheni
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Serikali za Mitaa
      • Afya
      • Elimu
      • Maji
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa Ndani
      • ununuzi na Ugavi
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Kitengo cha Sheria
  • Wilaya
    • Ilemela
    • Nyamagana
    • Magu
    • Misungwi
    • Kwimba
    • Sengerema
    • Ukerewe
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Jiji la Mwanza
    • Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
    • Hamashauri ya Wilaya ya Magu
    • Hamashauri ya Wilaya ya Sengerema
    • Hamashauri ya Wilaya ya Misungwi
    • Hamashauri ya Wilaya ya Kwimba
    • Hamashauri ya Wilaya ya Ukerewe
    • Hamashauri ya Wilaya ya Buchosa
  • Fursa za uwekezaji
    • Miundombinu ya Umwagiliaji na kilimo cha mkataba
    • Kilimo
    • Madini
    • Sekta ya Huduma
  • Huduma zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Watumishi
  • Machapisho
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa Kwa vyombo vya habari
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya video

Changamoto ya msongamano wa wanafunzi yatatuliwa Shule ya Iseni

Posted on: March 10th, 2020

Vyumba vitano vya madarasa vyajengwa ili kutatua changamoto ya msongamano wa wanafunzi darasani  hali hiyo itakayoboresha mazingira ya kujifunza na walimu kufundisha vyema ili kupandisha ufaulu wa wanafunzi na kuhamasisha mahudhurio darasani.

Akisoma taarifa fupi ya mradi huo Mkuu wa shule ya msingi Iseni “B” Donald Jovine alisema shule hiyo ina wanafunzi 1390 ambapo awali ilikuwa ikikabiliwa na changamotoya madarasa hivyo mradi huo umegharimu Million 79.16 kutoka katika vyanzo mbalimbali ambapo Mhe.Rais  alichangia million tano, mbunge wa jimbo hilo million mbili ,Naibu Waziri wa maji million moja na halimashauri hiyo ikitoa millon 71.16.

“Awali tulikabiliwa na upungufu wa vyumba vya madarasa na matundu ya vyoo tunaishukuru Serikali kwa sababu watoto wetu hawataweza kubanana tena  kama ilivyokuwa awali “.alisema Jovine.

Akizungumza wakati wa ziara yake ya siku mbili ya ukaguzi wa miradi mbalimbali inayotekeleza katika wilaya ya Nyamagana Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. John Mongella aliwataka walimu kuongeza jitihada katika ufundishaji ili kuleta matokeo yaliyo bora na yenye tija ,huku akiwataka wanafunzi hao kuwa wasikivu kwa walimu na wazazi wao , kuwa na hekima na kuepukana na watu wenye nia ya kuwapotosha na kuwapotezea dira ya kufikia malengo yao .

“Ukiona mtu akakuamba mambo ya hovyo kamwambie mwalimu au mzazi kuna majitu mtaani yana akili mbovumbovu yanataka kuwaharibu akili za watoto usikubali, akija mkaka au mdada anakuambia maneno au mambo ya hovyo kataa kimbia alafu nenda kamwambie mkubwa aliyeko karibu yako na sisi mkitoa taarifa, hayo majitu tutayakamata na kuyashugulikia”alisema Mhe.Mongella.

 Ester Joel ni mmoja wa wanafunzi wa shule hiyo alisema wanamshukuru Mungu kwa zawadi ya mema yote yanayotokea shuleni hapo pamoja na Serikali kwa kuona changamoto yao hivyo wanaahidi kujituma katika masomo  na kuyatunza vyema majengo hayo kwa faida yao na kizazi kijacho.

Mradi huo waujenzi wa vyumba vya madarasa uliasisiwa na Mhe. Rais Dkt.John Magufuli Desemba 7 mwaka jana ambapo utekelezaji wake ulianza Desemba 8 mwaka jana huku  ukitarajiwa kukamilika February 18 mwaka 2020 ambapo kwa sasa mradi huo upo katika hatua yaukamilishaji.

Matangazo

  • Tangazo la kukutana na Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Mwanza kwa shida mbalimbali. January 08, 2025
  • TANGAZO LA NANENANE TAREHE 8.8.2025 January 08, 2025
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • UZALISHAJI ZAO LA PAMBA WAONGEZEKA- MSIGWA

    May 03, 2025
  • DARAJA LA KIGONGO-BUSISI KUANZA KUTUMIKA MUDA WOWOTE KUANZIA SASA.

    May 02, 2025
  • SERIKALI YAANIKA TAKWIMU ZA MAENDELEO YA UTUMISHI YALIYOPATIKANA MWANZA

    May 01, 2025
  • MAKUNDI MAWILI YA MWISHO YALIYOFANYA ZIARA HIFADHI NA JNHPP YAWASILISHA NENO LA SHUKRANI KWA RAS BALANDYA

    April 29, 2025
  • Angalia zote

Video zinazotembea

Siku 365 za Mhe.Rais Samia Suluhu Hassan Mwanza
video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Fomu ya Ugonjwa
  • FFARS User Guidelines
  • Miongozo ya mfumo wa bajeti na Mipango
  • Makusanyo ya Ndani ya Halmashauri za Mkoa wa Mwanza
  • PReM
  • Maswali Yaulizwayo Mara kwa Mara
  • Opras fomu
  • OFISI MTANDAO

Viunganishi Linganishi

  • Tovuti ya Ikulu
  • Utumishi
  • Tamisemi
  • Ofisi ya Taifa ya Takwimu Tanzania
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Kuu ya Serikali

Watembeleaji

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive

    S.L.P: 119, Mwanza.

    Simu: 028-2501037

    Simu ya Mkononi: 028-2501037

    Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.