• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
Mwanza Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Mwanza

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia ya Mkoa
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti Mkoa
    • Seksheni
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Serikali za Mitaa
      • Afya
      • Elimu
      • Maji
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa Ndani
      • ununuzi na Ugavi
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Kitengo cha Sheria
  • Wilaya
    • Ilemela
    • Nyamagana
    • Magu
    • Misungwi
    • Kwimba
    • Sengerema
    • Ukerewe
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Jiji la Mwanza
    • Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
    • Hamashauri ya Wilaya ya Magu
    • Hamashauri ya Wilaya ya Sengerema
    • Hamashauri ya Wilaya ya Misungwi
    • Hamashauri ya Wilaya ya Kwimba
    • Hamashauri ya Wilaya ya Ukerewe
    • Hamashauri ya Wilaya ya Buchosa
  • Fursa za uwekezaji
    • Miundombinu ya Umwagiliaji na kilimo cha mkataba
    • Kilimo
    • Madini
    • Sekta ya Huduma
  • Huduma zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Watumishi
  • Machapisho
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa Kwa vyombo vya habari
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya video

"Hakikisheni wananchi wanahamasishwa kushiriki uchaguzi Selikali za mitaa" - Mongella

Posted on: October 7th, 2019


Watendaji na viongozi wa ngazi zote Mkoani Mwanza wametakiwa kuwajibika vilivyo ili kuongeza hamasa kwa wananchi kushiriki uchaguzi wa serikali za mitaa unaotarajiwa kufanyika nchini novemba 24 mwaka huu.

Agizo hilo limetolewa na Mkuu wa Mkoa wa mwanza  Mhe.John Mongella  wakati akizungumuza  na wakuu wa wilaya nawatendaji wa halmashauri zote za Mkoa wa Mwanza pamoja na kamati za ulinzi na usalama ya mkoa na wilaya  ili kujadili mikakati mbalimbali itakayofanikisha uchaguzi huo bila dosari.

“Sasa tupo tunaelekea kwenye uchaguzi wa serikali za mtaa ambao utatupatia viongozi  wa wananchi ngazi za vijiji, vitongoji na mitaa, lakini kumekuwa na tatizo la ushiriki duni kwa wananchi wetu labda kutokana na uelewa hafifu juu ya umuhimu wa chaguzi hizi.

“Sasa ninawaagiza watendaji wote mkawajibike kuhakikisha mnaongeza hamasa kwa wananchi wetu ili wajitokeze kwa wingi kushiriki uchaguzi huu hasa kwa kuanza na kujiandikisha kwenye daftari la wakazi na wananchi ili wapate sifa ya msingi kabisa cha kushiriki uchaguzi huu ili kuimarisha demokrasia.

“Kwani kwa mfumo wa nchi yetu demokrasia inaambatana kabisa na mchakato wa maendeleo na mfumo wa ulinzi na usalama, ndiyo maana katika ngazi husika viongozi hawa watakaochaguliwa ndiyo wanatambulika kama viongozi wa kamati ya ulinzi na usalama kwenye maeneo yao.

“kwa hiyo nitumie fursa hii kuwaelekeza viongozi wote kwenye mkoa, wilaya hadi ngazi ya vitongoji kukahakikisha tunatengeneza hamasa ya kutosha ili wananchi wetu wajiandikishe, pia tunajenga hamasa kwa viongozi wa kijamii na wao wasiwe nyuma katika hili.

“Lakini pia pamoja na hayo wote tunaohusika na kamati ya ulinzi na usalama tuhakikishe zoezi hili linafanyika kwa amani kwenye maeneo yote kuanzia zoezi la uandikishaji hadi kupiga kura, na yeyote atakayeonekana kuvuruga mchakato huu achukuliwe hatua mara moja kwani huu ni kama mwanzo wa kuelekea uchaguzi mkuu mwaka kesho,”alisema Mongella.

Akizungumza kwa niaba ya Wakuu wa wilaya wengine, Mkuu wa wilaya ya  Sengerema,  Mhe.Emmanuel Kipole amesema kuwa maagizo ya Mkuu wa Mkoa ni ya msingi na yanatekelezeka hasa ukizingatiwa kuwa yanalenga kuleta tija na kufanikisha adhima ya kupata viongozi bora bila kupoteza amani ya Mkoa na Taifa kwa ujumla.

“Maagizo haya ni muhimu kwani uchaguzi tunaouendea wavitongoji na vijiji ndiyo chimbuko la serikali za mitaa na ndio msingi wa maendeleo kwa maeneo hayo kwani ina machango mkubwa katika kushirikiana na serikali kuu ili kufanikisha utekelezaji wa sera mbalimbali.

“Hivyo sisi kama wakuu wa wilaya ikiwemo mimi ni lazima tuwahamasishe wananchi kushiriki uchaguzi huu kwa maana serikali ya mtaa ndio serikali iliyo karibu zaidi na wao na inayoweza kujionea kwa macho matatizo wanayokutana nayo na pengine kuyatatuia kabla ya serikali kuu.

“Lakini pia nitumie nafasi hii kuwasihi wananchi wa wilaya yangu na mkoa wa mwanza kwa ujumla kuacha kufanya uchaguzi huu kwa mazoea kwani kuna maeneo unakuta viongozi ndiyo walewale ambao kwa muda mrefu wameshindwa kupeleka mbele sera na dhamira ya maendeleo, sasa kila mmoja ashiriki kikamilifu ili kwa tupeleke maendeleo mbele,"alisema Kipole.

  





Matangazo

  • Tangazo la kukutana na Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Mwanza kwa shida mbalimbali. January 08, 2025
  • TANGAZO LA NANENANE TAREHE 8.8.2025 January 08, 2025
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • UZALISHAJI ZAO LA PAMBA WAONGEZEKA- MSIGWA

    May 03, 2025
  • DARAJA LA KIGONGO-BUSISI KUANZA KUTUMIKA MUDA WOWOTE KUANZIA SASA.

    May 02, 2025
  • SERIKALI YAANIKA TAKWIMU ZA MAENDELEO YA UTUMISHI YALIYOPATIKANA MWANZA

    May 01, 2025
  • MAKUNDI MAWILI YA MWISHO YALIYOFANYA ZIARA HIFADHI NA JNHPP YAWASILISHA NENO LA SHUKRANI KWA RAS BALANDYA

    April 29, 2025
  • Angalia zote

Video zinazotembea

Siku 365 za Mhe.Rais Samia Suluhu Hassan Mwanza
video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Fomu ya Ugonjwa
  • FFARS User Guidelines
  • Miongozo ya mfumo wa bajeti na Mipango
  • Makusanyo ya Ndani ya Halmashauri za Mkoa wa Mwanza
  • PReM
  • Maswali Yaulizwayo Mara kwa Mara
  • Opras fomu
  • OFISI MTANDAO

Viunganishi Linganishi

  • Tovuti ya Ikulu
  • Utumishi
  • Tamisemi
  • Ofisi ya Taifa ya Takwimu Tanzania
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Kuu ya Serikali

Watembeleaji

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive

    S.L.P: 119, Mwanza.

    Simu: 028-2501037

    Simu ya Mkononi: 028-2501037

    Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.