• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
Mwanza Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Mwanza

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia ya Mkoa
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti Mkoa
    • Seksheni
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Serikali za Mitaa
      • Afya
      • Elimu
      • Maji
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa Ndani
      • ununuzi na Ugavi
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Kitengo cha Sheria
  • Wilaya
    • Ilemela
    • Nyamagana
    • Magu
    • Misungwi
    • Kwimba
    • Sengerema
    • Ukerewe
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Jiji la Mwanza
    • Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
    • Hamashauri ya Wilaya ya Magu
    • Hamashauri ya Wilaya ya Sengerema
    • Hamashauri ya Wilaya ya Misungwi
    • Hamashauri ya Wilaya ya Kwimba
    • Hamashauri ya Wilaya ya Ukerewe
    • Hamashauri ya Wilaya ya Buchosa
  • Fursa za uwekezaji
    • Miundombinu ya Umwagiliaji na kilimo cha mkataba
    • Kilimo
    • Madini
    • Sekta ya Huduma
  • Huduma zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Watumishi
  • Machapisho
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa Kwa vyombo vya habari
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya video

Halmashauri ya Magu yapongezwa kwa ukusanyaji Mapato

Posted on: June 25th, 2022


Mhandisi Robert Gabriel, Mkuu wa Mkoa wa Mwanza ameipongeza Halmashauri ya Wilaya ya Magu kwa ufanisi kwenye kutekeleza maagizo mbalimbali ya viongozi na mwenendo mzuri wa Ukusanyaji wa mapato na matumizi ya fedha yanayozingatia sheria.

Mhe Mkuu wa Mkoa ametoa pongezi hizo leo jumamosi juni 25, 2022 wilayani Magu wakati wa Baraza la  Hoja za Mdhibiti na Mkaguzi wa Hesabu za Serikali kwa ripoti ya Mwaka 2020/21 ambayo imewapatia Halmshauri hiyo Hati Inayoridhisha.

"Nawapongeza kwa kuwa wasikivu na kutopuuza maagizo ya viongozi, mmeyatendea haki maelekezo na vilevile umakini wenu kwenye kujibu hoja wakati wa ukaguzi na haya ndio matunda leo tumekutana muda mfupi kupeana maelekezo ya kurekebisha dosari kidogo zilizojitojeza." RC Gabriel.

Vilevile, ametoa wito kwa watumishi waliolipwa fedha kinyume cha taratibu kurejesha fedha hizo chini ya usimamizi wa Ofisi ya Katibu Tawala Mkoa na Halmashauri kuhakikisha wanakamilisha Miradi mbalimbali iliyoanzishwa yenye thamani ya zaidi ya Tshs Bilioni 5.

Mkuu wa Wilaya ya Magu Mhe Salim Kalli ameupongeza uongozi wa Halmashauri kwa ufanisi kwenye ukusanyaji mapato na matumizi ya fedha na amewashukuru viongozi wa Halamshauri hiyo kwa ushirikiano na kamati ya Usalama na amewaahidi kuendeleza ushirikiano ili kuwaletea maendeleo wananchi.

"Baada ya baraza hili halmashauri lazima muwe na mpango kazi mzuri wa kufuatilia maagizo yote yaliyotolewa na wakuu wa idara hakikisheni mnashiriki kwa kina kwenye kujibu hoja zote." Mkaguzi wa ndani kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa kwa niaba ya Katibu Tawala Mkoa.

Mwenyekiti wa Halmshauri ya Wilaya ya Magu, Mhe Simon Pandalume amekiri kuwepo kwa changamoto ya upungufu wa madawati kwenye baadhi ya shule kwenye Halmashauri hiyo na ameahidi kuwa kupitia fedha za mapato ya ndani wanakwenda kulitatua tatizo hilo kwa kushirikisha na wananchi na wadau.  

"Mhe Mkuu wa Mkoa, tumeshavuka malengo ya makusanyo kwa 130% ya makusanyo na tumeshapeleka Tshs Bilioni 1 kwenye miradi ya Maendeleo wakati tulikasimia Tshs Milioni 800 na Milioni 260 tumevikopesha vikundi ikiwa tulikasimia kupeleka milioni 200 tu, haya ni matunda ya maelekezo yako na tunakushukuru sana."amebainisha Mwenyekiti.

Awali, Kaimu Mdhibiti na Mkaguzi wa Hesabu za Serikali Mkoa wa Mwanza, Waziri Shabani alisema Mwaka 2020/21 Halmashauri ya Wilaya ya Magu ilifanyiwa Ukaguzi na kupata Hati Inayoridhisha na kwamba kuanzia 2013/14 hadi 2021 Halmashauri hiyo imekua na jumla ya hoja 32  ambazo hazijatekelezwa kikamilifu na hazijafungwa.


Matangazo

  • Tangazo la kukutana na Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Mwanza kwa shida mbalimbali. January 08, 2025
  • TANGAZO LA NANENANE TAREHE 8.8.2025 January 08, 2025
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • UZALISHAJI ZAO LA PAMBA WAONGEZEKA- MSIGWA

    May 03, 2025
  • DARAJA LA KIGONGO-BUSISI KUANZA KUTUMIKA MUDA WOWOTE KUANZIA SASA.

    May 02, 2025
  • SERIKALI YAANIKA TAKWIMU ZA MAENDELEO YA UTUMISHI YALIYOPATIKANA MWANZA

    May 01, 2025
  • MAKUNDI MAWILI YA MWISHO YALIYOFANYA ZIARA HIFADHI NA JNHPP YAWASILISHA NENO LA SHUKRANI KWA RAS BALANDYA

    April 29, 2025
  • Angalia zote

Video zinazotembea

Siku 365 za Mhe.Rais Samia Suluhu Hassan Mwanza
video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Fomu ya Ugonjwa
  • FFARS User Guidelines
  • Miongozo ya mfumo wa bajeti na Mipango
  • Makusanyo ya Ndani ya Halmashauri za Mkoa wa Mwanza
  • PReM
  • Maswali Yaulizwayo Mara kwa Mara
  • Opras fomu
  • OFISI MTANDAO

Viunganishi Linganishi

  • Tovuti ya Ikulu
  • Utumishi
  • Tamisemi
  • Ofisi ya Taifa ya Takwimu Tanzania
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Kuu ya Serikali

Watembeleaji

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive

    S.L.P: 119, Mwanza.

    Simu: 028-2501037

    Simu ya Mkononi: 028-2501037

    Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.