• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
Mwanza Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Mwanza

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia ya Mkoa
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti Mkoa
    • Seksheni
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Serikali za Mitaa
      • Afya
      • Elimu
      • Maji
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa Ndani
      • ununuzi na Ugavi
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Kitengo cha Sheria
  • Wilaya
    • Ilemela
    • Nyamagana
    • Magu
    • Misungwi
    • Kwimba
    • Sengerema
    • Ukerewe
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Jiji la Mwanza
    • Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
    • Hamashauri ya Wilaya ya Magu
    • Hamashauri ya Wilaya ya Sengerema
    • Hamashauri ya Wilaya ya Misungwi
    • Hamashauri ya Wilaya ya Kwimba
    • Hamashauri ya Wilaya ya Ukerewe
    • Hamashauri ya Wilaya ya Buchosa
  • Fursa za uwekezaji
    • Miundombinu ya Umwagiliaji na kilimo cha mkataba
    • Kilimo
    • Madini
    • Sekta ya Huduma
  • Huduma zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Watumishi
  • Machapisho
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa Kwa vyombo vya habari
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya video

Jafo ”Nimekoshwa na Kasi Yenu"

Posted on: August 7th, 2017

Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Selemani Jafo (Mb), ameonesha kukoshwa na kazi za maendeleo zinazofanywa katika halmashauri ya Ukerewe Mkoani Mwanza, huku akiwataka kuongeza kasi hiyo ili kuendana na dhamira njema ya Serikali ya awamu ya tano chini ya Rais John Pombe Magufuli katika kuwahudumia wananchi.

Jafo alikuwa ziarani Wilayani Ukerewe kwa dhumuni la kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo ambapo ametembelea Hospitali ya Wilaya, vituo viwili vya afya ambavyo ni Nakatunguru na Muriti sambamba na mradi wa maji Lutare Chabilungo na miradi ya P4R ya mabweni, shighuli zingine alizo kagua ni madarasa na vyoo katika shule za sekondari za Pius Msekwa na Bukongo na kisha kuzungumza na watumishi wa halmashauri katika ukumbi mkubwa mikutano.

“Naomba niishukuru sana Miradi mingi sana imefanywa vizuri hongereni kwa kazi nzuri, nimetembelea mradi wa maji vijijini Lutare Chabilungo kazi imeenda vizuri na ninaamini tukisimamia mradi ule ipasavyo katika sehemu iliyobakia wilaya itakua na uwezo wa kupata maji vijijini kwa wastani wa 77% kutoka 55%  ya sasa, hivyo usimamiwe vizuri mpaka mwisho. Alisema Jafo. Na kuongeza “Miradi unatekelezwa kwa bajeti ya Bilioni 7 ambapo mpaka sasa serikali imeshalipa Bilioni 5, haya ni mafanikio makubwa.

Akiwa katika ukaguzi wa mradi huo Naibu Waziri jafo ameagiza kufanywa marekebisho mapema na kama kuna mabomba yaliyo chini ya kiwango yasitumike ilikuiepushia Halmashauri gharama za kununua mabomba pindi mradi utakapo anza kazi huku akimuagiza mhandisi wa maji wilayani humo William Kahurananga kuhakikisha vijiji 13 vilivyo kwenye mradi vinapata maji.

Akizungumzia suala la Sekta ya afya amesema sekta hiyo imekua na changamoto ya upungufu wa dawa hivyo amemwagiza Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo,  kuhakikisha wananunua dawa kwa ajili ya kuwahudumia wananchi.

“Pesa zote za kununua dawa zitumike kununua dawa na sio vinginevyo” alisema Jafo, huku akisifu matumizi ya mfumo wa malipo hospitali ukiwa unafanya kazi katika hospitali ya wilaya.

Akizungumza na watumishi wa Halmashauri hiyo, katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri amewataka watumishi wabadilike katika utendaji wa kazi maana “a business as usual” imekufa na amesema pamejengeka tabia ya watumishi kufanya kazi pekee zenye maslahi.

Singependa kuona watumishi wanajikita katika shughuli zenye manufaa pekee na shghuli zingine vile vile hakikisheni zinafanyika kwa ufanisi alisistiza waziri Jafo.

Jafo, ameonya kuwa  OPRAS system imekua haifanyiki ipasavyo “katika maeneo mengi imekua ni ya (copy and paste) kama celebration form ya  harusi au zinafanyika pale wakaguzi au upandaji wa madaraja lakini katika sekta binafsi unafanya kazi na utendaji unapimwa hivyo”, alisema na kuongeza kwamba  “watumishi wa serikali wanapaswa kubadilika na kuanza kuweka mpango kazi wa nini anatarajia kutekeleza lengo moja baada ya lingine na mkuu wa idara afanye hivyo na ikifika mwaka mwingine wa fedha uhakiki ufanyike kubaini malengo mliokubaliana yamefanyiwa kazi au lasivyo wakuu wa idara wanaoshindwa kutimiza majukumu yao ipasavyo nafasi zao zijazwe na wengine kwani Halmashauri ina wataalamu wengi wazuri na wenye elimu kuanzia shahada ya kwanza (Degree) na shahada ya uzamili (masters degree). “Lazima tubadilike”alisema Jafo.

Aidha kuhusu miradi ya  elimu Jafo alipo tembelea shule mbili za sekondari za Pius Msekwa na Bukongo ambazo zililetewa fedha zaidi ya shilingi milioni 500 za  utekelezaji ujenzi wa mabweni ya kulala wanafunzi mawili kwa kila shule, madarasa mannne kila shule pamoja na matundu ya vyoo.

Serikali ya awamu ya tano, imejizatiti katika kuhakikisha wananchi wanapata huduma za msingi ikiwapo elimu, afya na uboreshwaji wa huduma za miundombinu ya huduma za jamii kama Maji na barabara.

Matangazo

  • Tangazo la kukutana na Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Mwanza kwa shida mbalimbali. January 08, 2025
  • TANGAZO LA NANENANE TAREHE 8.8.2025 January 08, 2025
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • UZALISHAJI ZAO LA PAMBA WAONGEZEKA- MSIGWA

    May 03, 2025
  • DARAJA LA KIGONGO-BUSISI KUANZA KUTUMIKA MUDA WOWOTE KUANZIA SASA.

    May 02, 2025
  • SERIKALI YAANIKA TAKWIMU ZA MAENDELEO YA UTUMISHI YALIYOPATIKANA MWANZA

    May 01, 2025
  • MAKUNDI MAWILI YA MWISHO YALIYOFANYA ZIARA HIFADHI NA JNHPP YAWASILISHA NENO LA SHUKRANI KWA RAS BALANDYA

    April 29, 2025
  • Angalia zote

Video zinazotembea

Siku 365 za Mhe.Rais Samia Suluhu Hassan Mwanza
video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Fomu ya Ugonjwa
  • FFARS User Guidelines
  • Miongozo ya mfumo wa bajeti na Mipango
  • Makusanyo ya Ndani ya Halmashauri za Mkoa wa Mwanza
  • PReM
  • Maswali Yaulizwayo Mara kwa Mara
  • Opras fomu
  • OFISI MTANDAO

Viunganishi Linganishi

  • Tovuti ya Ikulu
  • Utumishi
  • Tamisemi
  • Ofisi ya Taifa ya Takwimu Tanzania
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Kuu ya Serikali

Watembeleaji

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive

    S.L.P: 119, Mwanza.

    Simu: 028-2501037

    Simu ya Mkononi: 028-2501037

    Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.