• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
Mwanza Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Mwanza

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia ya Mkoa
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti Mkoa
    • Seksheni
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Serikali za Mitaa
      • Afya
      • Elimu
      • Maji
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa Ndani
      • ununuzi na Ugavi
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Kitengo cha Sheria
  • Wilaya
    • Ilemela
    • Nyamagana
    • Magu
    • Misungwi
    • Kwimba
    • Sengerema
    • Ukerewe
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Jiji la Mwanza
    • Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
    • Hamashauri ya Wilaya ya Magu
    • Hamashauri ya Wilaya ya Sengerema
    • Hamashauri ya Wilaya ya Misungwi
    • Hamashauri ya Wilaya ya Kwimba
    • Hamashauri ya Wilaya ya Ukerewe
    • Hamashauri ya Wilaya ya Buchosa
  • Fursa za uwekezaji
    • Miundombinu ya Umwagiliaji na kilimo cha mkataba
    • Kilimo
    • Madini
    • Sekta ya Huduma
  • Huduma zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Watumishi
  • Machapisho
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa Kwa vyombo vya habari
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya video

KAMBI YA MAGONJWA YA MASIKIO, PUA NA KOO YAZINDULIWA RASMI SEKOU TOURE

Posted on: November 15th, 2024

KAMBI YA MAGONJWA YA MASIKIO, PUA NA KOO YAZINDULIWA RASMI SEKOU TOURE


Katibu Tawala Msaidizi Utawala na Rasilimali watu Bw. Daniel Machunda amezindua utoaji wa huduma ya masikio, pua na koo, inayofanyika katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mwanza Sekou Toure ikishirikiana na jumuiya ya wataalamu wa Magonjwa hayo Tanzania.

Akizindua huduma hizo Novemba 15, 2024 Bw. Machunda amesema kutokana na shida kubwa kwenye jamii wameandaa utoaji wa huduma za Kibingwa na Kibingwa Bobezi za masikio, pua na koo zinazotolewa kuanzia Novemba15 -16  2024.

Ameongeza kuwa huduma hii itakuwa suluhisho kwa wagonjwa wenye changamoto ya masikio, pua na koo na kuwasihi wananchi wajitokeze kwa wingi ili kupata huduma bora na staha kwa ajili ya ustawi mzuri wa wananchi.

Sambamba na hilo Mganga Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Dkt. Jesca Lebba amesema magonjwa hayo  yameendelea kuwasumbua wananchi wengi hivyo amewahimiza wananchi wenye changamoto hiyo kufika katika Hospitali ya Sekou Toure na kupata matibabu.

"Niwaombe wagonjwa wenye changamoto za masikio, pua na koo wafike na wapate matibabu kutoka Kwa Madaktari Bingwa na Bingwa Bobezi wa masikio, pua na koo." Dkt Jesca Lebba

Kwa upande wake Kaimu Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Sekoutoure Dkt. Englebert Rauya amemshukuru uongozi wa jumuiya ya wataalamu wa magonjwa ya masikio, pua na koo Tanzania waliofika katika Hospitali ya Sekoutoure kwa kutaka huduma ya matibabu kwa wagonjwa waliojitokeza na kuwahakikishia huduma nzuri na za haraka.

Matangazo

  • Tangazo la kukutana na Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Mwanza kwa shida mbalimbali. January 08, 2025
  • TANGAZO LA NANENANE TAREHE 8.8.2025 January 08, 2025
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • UZALISHAJI ZAO LA PAMBA WAONGEZEKA- MSIGWA

    May 03, 2025
  • DARAJA LA KIGONGO-BUSISI KUANZA KUTUMIKA MUDA WOWOTE KUANZIA SASA.

    May 02, 2025
  • SERIKALI YAANIKA TAKWIMU ZA MAENDELEO YA UTUMISHI YALIYOPATIKANA MWANZA

    May 01, 2025
  • MAKUNDI MAWILI YA MWISHO YALIYOFANYA ZIARA HIFADHI NA JNHPP YAWASILISHA NENO LA SHUKRANI KWA RAS BALANDYA

    April 29, 2025
  • Angalia zote

Video zinazotembea

Siku 365 za Mhe.Rais Samia Suluhu Hassan Mwanza
video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Fomu ya Ugonjwa
  • FFARS User Guidelines
  • Miongozo ya mfumo wa bajeti na Mipango
  • Makusanyo ya Ndani ya Halmashauri za Mkoa wa Mwanza
  • PReM
  • Maswali Yaulizwayo Mara kwa Mara
  • Opras fomu
  • OFISI MTANDAO

Viunganishi Linganishi

  • Tovuti ya Ikulu
  • Utumishi
  • Tamisemi
  • Ofisi ya Taifa ya Takwimu Tanzania
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Kuu ya Serikali

Watembeleaji

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive

    S.L.P: 119, Mwanza.

    Simu: 028-2501037

    Simu ya Mkononi: 028-2501037

    Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.