• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
Mwanza Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Mwanza

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia ya Mkoa
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti Mkoa
    • Seksheni
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Serikali za Mitaa
      • Afya
      • Elimu
      • Maji
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa Ndani
      • ununuzi na Ugavi
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Kitengo cha Sheria
  • Wilaya
    • Ilemela
    • Nyamagana
    • Magu
    • Misungwi
    • Kwimba
    • Sengerema
    • Ukerewe
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Jiji la Mwanza
    • Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
    • Hamashauri ya Wilaya ya Magu
    • Hamashauri ya Wilaya ya Sengerema
    • Hamashauri ya Wilaya ya Misungwi
    • Hamashauri ya Wilaya ya Kwimba
    • Hamashauri ya Wilaya ya Ukerewe
    • Hamashauri ya Wilaya ya Buchosa
  • Fursa za uwekezaji
    • Miundombinu ya Umwagiliaji na kilimo cha mkataba
    • Kilimo
    • Madini
    • Sekta ya Huduma
  • Huduma zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Watumishi
  • Machapisho
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa Kwa vyombo vya habari
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya video

Kamishna wa Maadili nchini ataka Siri za watoa taarifa zilindwe ili Wananchi kuwajengea imani

Posted on: June 17th, 2022

Kamishna wa  Maadili nchini Jaji wa Rufani Mhe. Sivangilwa Mwangesi, amewataka watumishi  wa Sekretarieti ya maadili ya viongozi wa umma kulinda siri za watoa taarifa kuhusu malalamiko ya ukiukwaji wa maadili ya viongozi wa umma ili  kujenga imani ya wananchi kwa serikali yao.

Aidha, Mhe.Jaji Mwangesi amewataka watumishi wa umma kutekeleza majukumu yao kwa uadilifu wakijiepusha na shughuli zinazosababisha mgongano wa maslahi wanapotekeleza majukumu yao kwani hiyo ndiyo changamoto kubwa inayowakabili.

Jaji Mwangesi,ametoa agizo hilo jijini hapa leo Juni 16, 2022  wakati akizungumza na viongozi wa Mkoa wa Mwanza ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya wiki ya utumishi wa umma ambayo huadhimishwa  Juni 16 hadi 23 kila mwaka.


“Msijinufaishe na taarifa mnazozipata kutokana na nafasi zenu  kwa kujinufaisha nyie wenyewe binafsi, ndugu, jamaa au  rafiki zenu  kwa kufanya hivyo mtakuwa mnakiuka sheria ya maadili ya viongozi wa umma namba 13 ya mwaka 1995 sura ya 398 ambayo inalenga kuenzi na kudumisha suala zima la utawala bora, kujenga na kudumisha amani na utulivu nchini.


 “Mgongano wa maslahi ndiyo changamoto kubwa inayotukumba watumishi wa umma  mfano Serikali  inaweza kuwa inataka kutoa ajira ambazo bado haijazitangaza lakini wewe mtumishi ukajua unaanza kuwaambia ndugu, jamaa au rafiki zako ili waanze kujiandaa  kwa kufanya hivyo unawaondolea wengine ambao hawajajua haki ya kushiriki kupata nafasi hiyo kikamilifu, au kutokana na  nafasi yako labda nafasi za ajira zimetoka unamshinikiza yule anayesimamia nafasi hizo kumpa kipaumbele mwanao, ndugu, au jamaa yako, ”alisema Jaji Mwangesi.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Mwanza,Mhe. Mhandisi Robert Gabriel, alisema ataendelea kutoa kipaumbele kushirikisha jamii nzima kupambana na vitendo vya ukiukwaji wa maadili, haki za binadamu, uwajibikaji, utawala bora na mapambano dhidi ya rushwa.

"Suala la kujenga, kukuza na kusimamia maadili ni jukumu la kila mmoja wetu hivyo nitoe  rai kwa jamii nzima tushirikiane sote kwa pamoja katika ngazi zote na hasa  sisi tulioshiriki kikao hiki  tuwe mabalozi wa kwanza kufikisha ujumbe vizuri kwa watumishi wenzetu ambao hawajapata  fursa ya kuhudhuria kikao hiki na kwa jamii nzima.

Kwa mujibu wa Mhe.Mhandisi Gabriel, lengo la kikao hicho ni kuendelea kutambua dhamira ya kuufanya utumishi wa umma kuwa wenye ufanisi ,kuheshimika, watumishi wa umma  kufuata sheria ya utumishi wa umma, kanuni pamoja na kuzingatia viwango vya juu vya maadili ili kukuza utu, uwazi, uadilifu, uwajibikaji na kuimarisha imani ya wananchi kuhusu utendaji kazi serikalini.

Matangazo

  • Tangazo la kukutana na Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Mwanza kwa shida mbalimbali. January 08, 2025
  • TANGAZO LA NANENANE TAREHE 8.8.2025 January 08, 2025
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • UZALISHAJI ZAO LA PAMBA WAONGEZEKA- MSIGWA

    May 03, 2025
  • DARAJA LA KIGONGO-BUSISI KUANZA KUTUMIKA MUDA WOWOTE KUANZIA SASA.

    May 02, 2025
  • SERIKALI YAANIKA TAKWIMU ZA MAENDELEO YA UTUMISHI YALIYOPATIKANA MWANZA

    May 01, 2025
  • MAKUNDI MAWILI YA MWISHO YALIYOFANYA ZIARA HIFADHI NA JNHPP YAWASILISHA NENO LA SHUKRANI KWA RAS BALANDYA

    April 29, 2025
  • Angalia zote

Video zinazotembea

Siku 365 za Mhe.Rais Samia Suluhu Hassan Mwanza
video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Fomu ya Ugonjwa
  • FFARS User Guidelines
  • Miongozo ya mfumo wa bajeti na Mipango
  • Makusanyo ya Ndani ya Halmashauri za Mkoa wa Mwanza
  • PReM
  • Maswali Yaulizwayo Mara kwa Mara
  • Opras fomu
  • OFISI MTANDAO

Viunganishi Linganishi

  • Tovuti ya Ikulu
  • Utumishi
  • Tamisemi
  • Ofisi ya Taifa ya Takwimu Tanzania
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Kuu ya Serikali

Watembeleaji

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive

    S.L.P: 119, Mwanza.

    Simu: 028-2501037

    Simu ya Mkononi: 028-2501037

    Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.