• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
Mwanza Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Mwanza

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia ya Mkoa
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti Mkoa
    • Seksheni
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Serikali za Mitaa
      • Afya
      • Elimu
      • Maji
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa Ndani
      • ununuzi na Ugavi
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Kitengo cha Sheria
  • Wilaya
    • Ilemela
    • Nyamagana
    • Magu
    • Misungwi
    • Kwimba
    • Sengerema
    • Ukerewe
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Jiji la Mwanza
    • Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
    • Hamashauri ya Wilaya ya Magu
    • Hamashauri ya Wilaya ya Sengerema
    • Hamashauri ya Wilaya ya Misungwi
    • Hamashauri ya Wilaya ya Kwimba
    • Hamashauri ya Wilaya ya Ukerewe
    • Hamashauri ya Wilaya ya Buchosa
  • Fursa za uwekezaji
    • Miundombinu ya Umwagiliaji na kilimo cha mkataba
    • Kilimo
    • Madini
    • Sekta ya Huduma
  • Huduma zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Watumishi
  • Machapisho
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa Kwa vyombo vya habari
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya video

Kampeni ya Polio Kufanyika Mwanza Aprili 28 hadi Mei 1

Posted on: April 14th, 2022

Jumla ya watoto 846,733 waliochini ya miaka 5 mkoani Mwanza wanatarajia kupata chanjo ya matone (POLIO) ili kuwajengea kinga na kuzuia kuenea kwa virusi hivyo .

Hayo yamebainishwa na Mratibu wa chanjo Mkoa wa Mwanza Amos Kiteleja katika mkutano wa baraza la biashara  Kati ya Sekta ya Umma na  Binafsi uliofanyika leo Jijini Mwanza.

Ameeleza kuwa kampeni hiyo inachangiwa na nchi kuwa katika hatari ya ugonjwa huo kuingia mara baada ya February 17 mwaka huu nchi ya Malawi kutoa tamko la kuwepo kwa mlipuko wa ugonjwa huo nchini humo baada ya mtoto mmoja kutoka Mji Mkuu wa Lilongwe kudhibitika kuwa na ugonjwa huo.

" Nchi ya Malawi na Tanzania kuna mwingiliano mkubwa wa kibiashara na huduma nyingine za kijamii hivyo hatari ipo na chanjo ni muhimu itasaidia kuzuia ugonjwa huo usienee kwani kwa mara ya mwisho Tanzania ilipata mgonjwa wa Polio Julai 1996  hivyo kampeni hii inatarajiwa kufanyika katika nchi zinazopakana na Malawi ikiwemo Zambia,Msumbuji, Zimbabwe na Malawi yenyewe" anaeleza Kiteleja.

Anaeleza kuwa kampeni hiyo itaanza April 28 hadi Mei 1 mwaka huu watoto  wote wenye umri chini ya miaka mitano watachanja bila kujali chanjo alizopata siku za nyuma ambapo Halmashauri ya Ukerewe watafikiwa  watoto 108,937, Magu 93,721, Nyamagana 92,698, Kwimba 134,636, Sengerema 108,597, Ilemela 85,834, Misugwi 116,167 na Buchosa 106,143   .

" Jamii itambue kuwa mtoto ata kama alichanjwa jana lakini zoezi likianza atachanjwa tena chanjo hizi ni salama na katika zoezi ili kadi za watoto hazitatumika lakini kila baada ya mtoto kuchanjwa atawekewa alama maalum kwenye kidole kidogo cha mkono " anaeleza na kuongeza kuwa

"Kampeni hii ya siku nne itakuwa ni nyumba kwa nyumba na vituo  vya muda vitatumika katika maeneo mbalimbali ikiwemo masoko, shule,misikiti,makanisa,mashambani,vituo vya mabasi ,makambi ya wavuvi pia vituo vya kudumu timu za uchanjaji zitakuwa kwenye vituo vya kutoa huduma za afya kwa siku hizo." anaeleza Kiteleja.

Aidha ameeleza kuwa ugonjwa huo hauna tiba ila hukingwa na chanjo ya Polio ambayo ipo katika mfumo wa matone na sindano pia unapompata mtu hushambulia mishipa ya fahamu,kupooza na hatimaye kifo na unaweza kumpata mtu yeyote katika umri wowote ila mtoto huathirika zaidi .

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Robert Gabriel aliitaka jamii kuipokea na kutokuwa na hofu bali itambue chanjo ni ileile inayotumika miaka yote lengo ni kuongeza kinga , kuzuia mlipuko  na kuwa Taifa lenye afya njema na kuwa na uchumi imara.


Matangazo

  • Tangazo la kukutana na Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Mwanza kwa shida mbalimbali. January 08, 2025
  • TANGAZO LA NANENANE TAREHE 8.8.2025 January 08, 2025
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • UZALISHAJI ZAO LA PAMBA WAONGEZEKA- MSIGWA

    May 03, 2025
  • DARAJA LA KIGONGO-BUSISI KUANZA KUTUMIKA MUDA WOWOTE KUANZIA SASA.

    May 02, 2025
  • SERIKALI YAANIKA TAKWIMU ZA MAENDELEO YA UTUMISHI YALIYOPATIKANA MWANZA

    May 01, 2025
  • MAKUNDI MAWILI YA MWISHO YALIYOFANYA ZIARA HIFADHI NA JNHPP YAWASILISHA NENO LA SHUKRANI KWA RAS BALANDYA

    April 29, 2025
  • Angalia zote

Video zinazotembea

Siku 365 za Mhe.Rais Samia Suluhu Hassan Mwanza
video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Fomu ya Ugonjwa
  • FFARS User Guidelines
  • Miongozo ya mfumo wa bajeti na Mipango
  • Makusanyo ya Ndani ya Halmashauri za Mkoa wa Mwanza
  • PReM
  • Maswali Yaulizwayo Mara kwa Mara
  • Opras fomu
  • OFISI MTANDAO

Viunganishi Linganishi

  • Tovuti ya Ikulu
  • Utumishi
  • Tamisemi
  • Ofisi ya Taifa ya Takwimu Tanzania
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Kuu ya Serikali

Watembeleaji

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive

    S.L.P: 119, Mwanza.

    Simu: 028-2501037

    Simu ya Mkononi: 028-2501037

    Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.