• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
Mwanza Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Mwanza

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia ya Mkoa
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti Mkoa
    • Seksheni
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Serikali za Mitaa
      • Afya
      • Elimu
      • Maji
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa Ndani
      • ununuzi na Ugavi
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Kitengo cha Sheria
  • Wilaya
    • Ilemela
    • Nyamagana
    • Magu
    • Misungwi
    • Kwimba
    • Sengerema
    • Ukerewe
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Jiji la Mwanza
    • Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
    • Hamashauri ya Wilaya ya Magu
    • Hamashauri ya Wilaya ya Sengerema
    • Hamashauri ya Wilaya ya Misungwi
    • Hamashauri ya Wilaya ya Kwimba
    • Hamashauri ya Wilaya ya Ukerewe
    • Hamashauri ya Wilaya ya Buchosa
  • Fursa za uwekezaji
    • Miundombinu ya Umwagiliaji na kilimo cha mkataba
    • Kilimo
    • Madini
    • Sekta ya Huduma
  • Huduma zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Watumishi
  • Machapisho
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa Kwa vyombo vya habari
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya video

Katibu Mkuu SADC aipongeza Mwanza kwa maendeleo

Posted on: August 23rd, 2019


Katibu  Mkuu wa Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC) Mhe.Dkt. Stergomena Tax amewasili jijini Mwanza  kwa ziara ya siku mbili huku akishangazwa na  namna mkoa huo ulivyobadilika  kwa shughuli za maendeleo  kitendo kinachoashiria  kukua kwa uchumi wa nchi na mwananchi mmoja mmoja.

Dkt. Tax amewasili Mwanza  akitokea jijini Dar es Salaam na kupokelewa na viongozi wa ofisi ya Mkuu wa Mkoa huo na kufanya kikao kifupi kabla ya kuendelea na ziara Wilaya ya Magu ambapo alisema ameshangazwa na namna mkoa  huo ulivyobadilika kwa muda mfupi.

Alisema alipowasili katika Uwanja wa Ndege wa Mwanza, ameshuhudia maboresho makubwa yakiwamo upanuzi wa barabara ya kurukia ndege, jengo la mzigo na mnara wa kuongozea ndege na majengo mengine makubwa mitaani jambo ambalo linadhihirisha    wazi Serikali imekusudia kuimarisha uchumi wa nchi na wananchi wake.


Dkt. Tax ambaye ni mzaliwa wa Mkoa wa Mwanza, alisema kila anapobahatika kufika Mwanza anashuhudia mabadiliko makubwa ambapo aliwataka viongozi waliopewa dhamana  kuendelea na kaai hiyohiyo  ili  makusudio ya Rais Mhe. Dkt. John Magufuli yaweze kutimia  ndani ya miaka atakayotawala.

“Mwanza ni jiji kubwa na hivyo linastahili kuwa mwenyeji wa mikutano mikubwa kama SADC, binafsi nimefarijika kuona mabadiliko yanayoonekana kwa macho kuanzia uwanja wa ndege hadi huku mitaani, majengo ya kisasa ambayo awali tulikuwa tunayaona   kwingineko lakini leo tunayaona hapa,"alisema Dkt.Tax.

“Naomba viongozi  muendelee kwa kasi hiyo hiyo ya kusimamia shughuli za maendeleo ili wananchi waweze kufaidi utumishi wenu chini ya  utawala wa  Rais Dkt. Magufuli,  taifa limepata kiongozi ambaye ana uchungu na watu wake na rasilimali za nchi hivyo kila mmoja anapaswa  kuwajibika kwa nafasi yake,”alisema.

Awali, Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Mwanza, Emil Kasagara alimshukuru Dk. Tax kutembelea Mwanza  huku akimpongeza namna anavyoiwakilisha Tanzania  na kuongoza vizuri mkutano wa SADC uliofanyika hivi karibuni jijini Dar es Salaam.

“Tunashukuru kwa ujio wako mkoani kwetu na tunasema karibu sana, tunafarijika kwa nafasi yako ndani ya SADC na jinsi unavyoiwakilisha nchi katika mikutano mbalimbali, hivyo ni fahari kwetu kuona Tanzania tukipokea kijiti cha uenyekiti, bila shaka  tutafika salama ndani ya mwaka mmoja na kutimiza maazimio mliofikia,”alisema.



Matangazo

  • Tangazo la kukutana na Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Mwanza kwa shida mbalimbali. January 08, 2025
  • TANGAZO LA NANENANE TAREHE 8.8.2025 January 08, 2025
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • UZALISHAJI ZAO LA PAMBA WAONGEZEKA- MSIGWA

    May 03, 2025
  • DARAJA LA KIGONGO-BUSISI KUANZA KUTUMIKA MUDA WOWOTE KUANZIA SASA.

    May 02, 2025
  • SERIKALI YAANIKA TAKWIMU ZA MAENDELEO YA UTUMISHI YALIYOPATIKANA MWANZA

    May 01, 2025
  • MAKUNDI MAWILI YA MWISHO YALIYOFANYA ZIARA HIFADHI NA JNHPP YAWASILISHA NENO LA SHUKRANI KWA RAS BALANDYA

    April 29, 2025
  • Angalia zote

Video zinazotembea

Siku 365 za Mhe.Rais Samia Suluhu Hassan Mwanza
video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Fomu ya Ugonjwa
  • FFARS User Guidelines
  • Miongozo ya mfumo wa bajeti na Mipango
  • Makusanyo ya Ndani ya Halmashauri za Mkoa wa Mwanza
  • PReM
  • Maswali Yaulizwayo Mara kwa Mara
  • Opras fomu
  • OFISI MTANDAO

Viunganishi Linganishi

  • Tovuti ya Ikulu
  • Utumishi
  • Tamisemi
  • Ofisi ya Taifa ya Takwimu Tanzania
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Kuu ya Serikali

Watembeleaji

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive

    S.L.P: 119, Mwanza.

    Simu: 028-2501037

    Simu ya Mkononi: 028-2501037

    Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.