• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
Mwanza Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Mwanza

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia ya Mkoa
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti Mkoa
    • Seksheni
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Serikali za Mitaa
      • Afya
      • Elimu
      • Maji
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa Ndani
      • ununuzi na Ugavi
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Kitengo cha Sheria
  • Wilaya
    • Ilemela
    • Nyamagana
    • Magu
    • Misungwi
    • Kwimba
    • Sengerema
    • Ukerewe
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Jiji la Mwanza
    • Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
    • Hamashauri ya Wilaya ya Magu
    • Hamashauri ya Wilaya ya Sengerema
    • Hamashauri ya Wilaya ya Misungwi
    • Hamashauri ya Wilaya ya Kwimba
    • Hamashauri ya Wilaya ya Ukerewe
    • Hamashauri ya Wilaya ya Buchosa
  • Fursa za uwekezaji
    • Miundombinu ya Umwagiliaji na kilimo cha mkataba
    • Kilimo
    • Madini
    • Sekta ya Huduma
  • Huduma zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Watumishi
  • Machapisho
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa Kwa vyombo vya habari
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya video

Kikao cha bodi ya Barbara chapanga mikakati ya mafanikio Mwanza

Posted on: December 21st, 2020

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe.John Mongella amefungua kikao kikao kazi cha kwanza cha bodi ya Barbara ya Mkoa wa Mwanza cha mwaka wa fedha  2020/2021 na kusema kuwa kwa kipindi cha miaka mitano ijayo Mwanza itakuwa na sura mpya tofauti kutokana na viongozi waliopo kwa sasa hivyo mshikamano unahitajika ili  kuimarisha miundombinu ya mkoa kwani serikali imetoa fedha nyingi za kutekeleza miradi mbalimbali.

Amesema kwa miaka mitano  iliyopita wamefanikiwa katika sekta ya elimu siri ya mafanikio hayo ni uchapakazi ,umoja na utendaji kazi wenye tija ambao ulichangia watoto wote waliochaguliwa walifanikiwa kujiunga na shule hivyo hata kwa walichaguliwa kwa mwaka huu lazima wote wataingia madarasani, viongozi wote wafanye Kazi ili kuijenga nchi.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Magu Mhe.Salum Kalli na Mbunge wa Jimbo la Magu Mhe.Boniventura Kiswaga, walisema barabara ya Mahaha- Bariadi inaunganisha Mkoa wa Mwanza na Simiyu hivyo waliomba kujengwa kwa daraja ili kuweza kuunganisha mikoa hiyo na wananchi waweze kufanya shughuli zao za kimaendeleo .

Naye Mbunge wa Sumve Kasalali Mageni alisema kuna madaraja matatu ambayo  mvua ikinyesha  maji yanapita  juu yake hivyo kufanya wananchi kupita kwa kudra za Mungu na ameiomba TARURA  kuyapa kipaumbele madaraja hayo.

Akizungumzia  utekelezaji wa Kazi na matengenezo ya barabara wakala wa TARURA Mkoa wa Mwanza Mhandisi Gaston Paschal  amesema wanashughulikia matengenezo ya barabara za Mjini na vijijini katika Halmashauri Magu, Misungwi, Ukerewe,Buchosa, Sengerema, Kwimba, Ilemela na jiji la Mwanza hivyo kwa mwaka wa fedha 2020 hadi 2021 kwa Mkoa wa Mwanza wamepangiwa bilioni 11.2.

Ameongeza kuwa halmashauri zote zina mtandao wa barabara jumla ya 8628.039Km hadi Disemba 2020 kulingana na uthibitisho wa mtandao wa Wizara ya ujenzi uchukuzi na mawasiliano, nje ya mtandao huo barabara za lami ni 72.89 km, barabara za changarawe ni 1286.16km, barabara za udongo 7253.156 km,zege zikiwa 4.795km na za mawe zikiwa ni 11.03km.

Aidha, ameeleza matatizo yanayowasibu ni pamoja na wananchi kufanya shughuli za kibinadamu ,kilimo katika maeneo ya hifadhi pamoja na kiwango kidogo cha fedha za matengenezo ukilinganisha na Hali halisi ya mahitaji ya matengenezo ya barabara.

" Wizi na hujuma za alama za barabarani,makalavati,vyuma vya madaraja ,taa za barabarani,betri ,waya za umeme ,uchimbaji wa wananchi kupitisha mifugo barabarani, magari mazito kutumia barabara za viwango vidogo hayo yote ni matatizo" amesema Mhandisi Paschal.

Matangazo

  • Tangazo la kukutana na Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Mwanza kwa shida mbalimbali. January 08, 2025
  • TANGAZO LA NANENANE TAREHE 8.8.2025 January 08, 2025
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • UZALISHAJI ZAO LA PAMBA WAONGEZEKA- MSIGWA

    May 03, 2025
  • DARAJA LA KIGONGO-BUSISI KUANZA KUTUMIKA MUDA WOWOTE KUANZIA SASA.

    May 02, 2025
  • SERIKALI YAANIKA TAKWIMU ZA MAENDELEO YA UTUMISHI YALIYOPATIKANA MWANZA

    May 01, 2025
  • MAKUNDI MAWILI YA MWISHO YALIYOFANYA ZIARA HIFADHI NA JNHPP YAWASILISHA NENO LA SHUKRANI KWA RAS BALANDYA

    April 29, 2025
  • Angalia zote

Video zinazotembea

Siku 365 za Mhe.Rais Samia Suluhu Hassan Mwanza
video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Fomu ya Ugonjwa
  • FFARS User Guidelines
  • Miongozo ya mfumo wa bajeti na Mipango
  • Makusanyo ya Ndani ya Halmashauri za Mkoa wa Mwanza
  • PReM
  • Maswali Yaulizwayo Mara kwa Mara
  • Opras fomu
  • OFISI MTANDAO

Viunganishi Linganishi

  • Tovuti ya Ikulu
  • Utumishi
  • Tamisemi
  • Ofisi ya Taifa ya Takwimu Tanzania
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Kuu ya Serikali

Watembeleaji

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive

    S.L.P: 119, Mwanza.

    Simu: 028-2501037

    Simu ya Mkononi: 028-2501037

    Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.