• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
Mwanza Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Mwanza

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia ya Mkoa
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti Mkoa
    • Seksheni
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Serikali za Mitaa
      • Afya
      • Elimu
      • Maji
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa Ndani
      • ununuzi na Ugavi
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Kitengo cha Sheria
  • Wilaya
    • Ilemela
    • Nyamagana
    • Magu
    • Misungwi
    • Kwimba
    • Sengerema
    • Ukerewe
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Jiji la Mwanza
    • Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
    • Hamashauri ya Wilaya ya Magu
    • Hamashauri ya Wilaya ya Sengerema
    • Hamashauri ya Wilaya ya Misungwi
    • Hamashauri ya Wilaya ya Kwimba
    • Hamashauri ya Wilaya ya Ukerewe
    • Hamashauri ya Wilaya ya Buchosa
  • Fursa za uwekezaji
    • Miundombinu ya Umwagiliaji na kilimo cha mkataba
    • Kilimo
    • Madini
    • Sekta ya Huduma
  • Huduma zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Watumishi
  • Machapisho
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa Kwa vyombo vya habari
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya video

Kujifunza kwa waliofanikiwa kutasaidia kuongeza Ufaulu

Posted on: October 22nd, 2019

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. John Mongella amewataka Wakuu wa Wilaya na viongozi wengine wakiwemo wakuu wa shule za misingi za Serikali Mkoani hapa kujifunza kutoka kwa shule zilizofanikiwa.

Hayo ameyasema  alipotembelea Shule ya Msingi Mugini iliyopo Wilayani Magu ambayo imeshika nafasi ya tisa kitaifa kwa matokeo ya darasa la saba.

Amesema kuwa kuna wakati Shule za Serikali zinaendelea kufanya vibaya kutokana na na baadhi ya watendaji wa Wilaya kutokuwa na utayari wa kujifunza kutoka kwa shule zinazofanya vizuri.

"Binafsi nimefurahishwa sana na matokeo ya mtihani wa darsa la saba mwaka huu kwani kwenye kumi bora kitaifa mkoa wa Mwanza umeingiza shule nne Mugini ikiwa mojawapo," alisema Mongella.

"Nimeamua kuwatembelea hapa ili kujua nini siri ya mafanikio kwa sababu mimi nipo tayari kujifunza kutoka kwanu, kwa hiyo niwaombe na viongozi wenzangu ikiwemo wewe Mkuu wa Wilaya ya Magu, ongea nao ili hiyo siri ya mafanikio uipeleke kwenye shule zetu za Serikali.

"Tusione aibu kuwafuata wakatuambia wamefanikiwaje kwa sababu unakuta eti kuna wakurugenzi na wadau wengine wa elimu wanaenda hadi Rwanda kutafuta mbinu ya kuongeza ufaulu wakati watu wa mfano tunao hapa hapa, hebu tuwatumie hawa hawa naamini tutafikia malengo," alisema Mongella.

Awali akisoma risala ya shule hiyo kwa niaba ya Mkurugenzi wa Shule mmoja wa walimu wa Shule hiyo  ameeleza kuwa mafanikio ya shule hiyo kitaifa yametokana na juhudi za kila mfanyakazi kutimiza majukumu yake  pamoja na huduma bora zinazotolewa shuleni hapo.

"Shule yetu ambayo hadi sasa ina jumla ya wanafunzi 262, kati yao wavulana ni 124 na wasicahana 138, kwa mwaka huu wamehitimu waanafunzi 48 imefanikiwa kushika nafasi ya kwanza kiwilaya, nafasi ya nne kimkoa na nafasi ya 9 kitaifa.

"Ndugu mgeni rasmi mafanikio haya yametokana na juhudi za kila mtumishi kutimiza majukumu yake pamoja na huduma bora zinazotolewa shuleni  kutosheleza mahitaji ya wanafunzi kwa kuwatengenezea mazingira rafiki ya kujifunzia.

"Ingawa tumefanikiwa kuingia kumi bora kitaifa lakini bado kiu yetu kubwa ni kuona kuwa tunaendelea kufanya vizuri zaidi ya hapa na tunaingia nafasi tano za juu na baadaye kuongoza kitaifa ili kuujengea mkoa wetu heshima kubwa.

Hivyo tuuombe uongozi wa wilaya, mkoa hadi ngazi ya taifa kuendelea kushirikiana na shule binafsi ili kuziongezea morali ya kufanya vizuri zaidi na kuzalisha vijana walio na ufaulu bora kabisa,"alisema Mwalimu.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Magu  Dkt.Philemoni Sengati  alisema kuwa wilaya yake inajivunia uwepo wa shule kama hizo zinazoitambulisha kitaifa hivyo ataendelea kuungana na wadau wote wa elimu wilayani humo ili kuleta mafanikio yenye tija zaidi.




Matangazo

  • Tangazo la kukutana na Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Mwanza kwa shida mbalimbali. January 08, 2025
  • TANGAZO LA NANENANE TAREHE 8.8.2025 January 08, 2025
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • UZALISHAJI ZAO LA PAMBA WAONGEZEKA- MSIGWA

    May 03, 2025
  • DARAJA LA KIGONGO-BUSISI KUANZA KUTUMIKA MUDA WOWOTE KUANZIA SASA.

    May 02, 2025
  • SERIKALI YAANIKA TAKWIMU ZA MAENDELEO YA UTUMISHI YALIYOPATIKANA MWANZA

    May 01, 2025
  • MAKUNDI MAWILI YA MWISHO YALIYOFANYA ZIARA HIFADHI NA JNHPP YAWASILISHA NENO LA SHUKRANI KWA RAS BALANDYA

    April 29, 2025
  • Angalia zote

Video zinazotembea

Siku 365 za Mhe.Rais Samia Suluhu Hassan Mwanza
video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Fomu ya Ugonjwa
  • FFARS User Guidelines
  • Miongozo ya mfumo wa bajeti na Mipango
  • Makusanyo ya Ndani ya Halmashauri za Mkoa wa Mwanza
  • PReM
  • Maswali Yaulizwayo Mara kwa Mara
  • Opras fomu
  • OFISI MTANDAO

Viunganishi Linganishi

  • Tovuti ya Ikulu
  • Utumishi
  • Tamisemi
  • Ofisi ya Taifa ya Takwimu Tanzania
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Kuu ya Serikali

Watembeleaji

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive

    S.L.P: 119, Mwanza.

    Simu: 028-2501037

    Simu ya Mkononi: 028-2501037

    Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.