Swahili
  • English
  • Swahili
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
Mwanza Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Mwanza

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia ya Mkoa
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti Mkoa
    • Seksheni
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Serikali za Mitaa
      • Afya
      • Elimu
      • Maji
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa Ndani
      • ununuzi na Ugavi
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Kitengo cha Sheria
  • Wilaya
    • Ilemela
    • Nyamagana
    • Magu
    • Misungwi
    • Kwimba
    • Sengerema
    • Ukerewe
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Jiji la Mwanza
    • Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
    • Hamashauri ya Wilaya ya Magu
    • Hamashauri ya Wilaya ya Sengerema
    • Hamashauri ya Wilaya ya Misungwi
    • Hamashauri ya Wilaya ya Kwimba
    • Hamashauri ya Wilaya ya Ukerewe
    • Hamashauri ya Wilaya ya Buchosa
  • Fursa za uwekezaji
    • Miundombinu ya Umwagiliaji na kilimo cha mkataba
    • Kilimo
    • Madini
    • Sekta ya Huduma
  • Huduma zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Watumishi
  • Machapisho
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa Kwa vyombo vya habari
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya video

LENGO LILILOKUSUDIWA NANE NANE KANDA YA ZIWA MAGHARIBI LIMEFANIKIWA:RC MTANDA

Posted on: August 8th, 2024

LENGO LILILOKUSUDIWA NANE NANE KANDA YA ZIWA MAGHARIBI  LIMEFANIKIWA:RC MTANDA


Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. Said Mtanda ameipongeza kamati ya maandalizi ya maonesho ya kilimo na sherehe za wakulima (Nane nane) 2024 kwa maandalizi ambayo yamefanyika katika viwanja vya Nyamhongolo wilayani Ilemela.

Mhe. Mtanda ametoa pongezi hizo leo Agosti 08, 2024 wakati alipokuwa akihutubia wananchi waliojitokeza katika kilele cha sherehe za Nane nane Kanda ya Ziwa Magharibi (Mwanza, Geita na Kagera), Mhe. Mtanda amesema amefanikiwa kupita katika mabanda mbalimbali ya waoneshaji ameona na kujifunza teknolojia mbalimbali hakika lengo lililokusudiwa limefanikiwa.

"Nimefurahi kuona baadhi ya bidhaa na huduma zinazopatikana katika maonesho haya, nimetembelea makampuni, Taasisi, huduma za kifedha za mikopo ya kilimo, Taaisisi za elimu na zile za utafiti mkusanyo wa wadau wote hawa umechangia hamasa kubwa kwa wananchi wetu wa kanda ya ziwa nawapongeza na kuwahukuru sana". Mhe. Mtanda.

Aidha, Mkuu huyo wa Mkoa amesena katika maonesho hayo Wakulima na wananchi kwa ujumla pia wamepata nafasi ya kuona, kujifunza na kubadilishana uzoefu, teknolojia juu ya bidhaa na huduma  mbalimbali na hivyo kupanua wigo wa uelewa kuhusu uzalishaji, uongezaji thamani wa mazao pamoja na mtandao wa masoko ya bidhaa zinazozalishwa.

"Maonesho haya pia yametumika kuonesha mafanikio yaliyofikiwa pamoja na changamoto zinazoikabili sekta ya kilimo, mifugo na uvuvi ndivyo ambavyo watu wengi wetu tunatarajia kuona mabadiliko makubwa yanayotokea kwenye sekta hizi za kiuchimi". RC Mtanda.

Sambamba na hayo Mkuu wa Mkoa pia ametumia wasaa huo kuwakumbusha na kuwaomba wananchi kushiriki zoezi muhimu kwa Taifa la uchaguzi wa Serikali za Mitaa kwa amani, nidhamu na utulivu ili tuilinde amani ya nchi.

Akuzungumza kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhe. Martine Shigella ameipongeza pia kamati ya maandalizi ya sherehe hiyo huku akisema amekuwa akihudhuria maonesho hayo kwa kipindi cha miaka miwili lakini sherehe za mwaka huu zimefana sana.

Maonesho na sherehe za Wakulima kwa mwaka 2024 yamefanyika kwa kauli mbiu isemayo "Chagua Viongozi Bora wa Serikali za Mitaa kwa Maendeleo Endelevu ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi".

Matangazo

  • Tangazo la kukutana na Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Mwanza kwa shida mbalimbali. January 08, 2025
  • TANGAZO LA NANENANE TAREHE 8.8.2025 January 08, 2025
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • UKAMILIFU WA HOTELI YA NSSSF MWANZA NI FURSA YA KUKUZA UCHUMI - RC MTANDA

    June 11, 2025
  • RC MTANDA ASHIRIKI MAZISHI YA MZEE SILVIN MONGELLA

    June 07, 2025
  • BARAZA LA RAIS LA USHAURI WA KILIMO NA CHAKULA LAKUTANA NA WADAU WA KILIMO KANDA YA ZIWA

    June 04, 2025
  • MWANZA, SIMIYU ZANG'ARA UTAMILIFU DARASA LA SABA KANDA YA ZIWA

    May 30, 2025
  • Angalia zote

Video zinazotembea

Siku 365 za Mhe.Rais Samia Suluhu Hassan Mwanza
video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Fomu ya Ugonjwa
  • FFARS User Guidelines
  • Miongozo ya mfumo wa bajeti na Mipango
  • Makusanyo ya Ndani ya Halmashauri za Mkoa wa Mwanza
  • PReM
  • Maswali Yaulizwayo Mara kwa Mara
  • Opras fomu
  • OFISI MTANDAO

Viunganishi Linganishi

  • Tovuti ya Ikulu
  • Utumishi
  • Tamisemi
  • Ofisi ya Taifa ya Takwimu Tanzania
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Kuu ya Serikali

Watembeleaji

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive

    S.L.P: 119, Mwanza.

    Simu: 028-2501037

    Simu ya Mkononi: 028-2501037

    Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.