• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
Mwanza Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Mwanza

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia ya Mkoa
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti Mkoa
    • Seksheni
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Serikali za Mitaa
      • Afya
      • Elimu
      • Maji
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa Ndani
      • ununuzi na Ugavi
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Kitengo cha Sheria
  • Wilaya
    • Ilemela
    • Nyamagana
    • Magu
    • Misungwi
    • Kwimba
    • Sengerema
    • Ukerewe
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Jiji la Mwanza
    • Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
    • Hamashauri ya Wilaya ya Magu
    • Hamashauri ya Wilaya ya Sengerema
    • Hamashauri ya Wilaya ya Misungwi
    • Hamashauri ya Wilaya ya Kwimba
    • Hamashauri ya Wilaya ya Ukerewe
    • Hamashauri ya Wilaya ya Buchosa
  • Fursa za uwekezaji
    • Miundombinu ya Umwagiliaji na kilimo cha mkataba
    • Kilimo
    • Madini
    • Sekta ya Huduma
  • Huduma zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Watumishi
  • Machapisho
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa Kwa vyombo vya habari
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya video

MAAFISA TARAFA NA WATENDAJI,TUMIENI MAFUNZO HAYA MKATOE HUDUMA BORA KWA WANANCHI:RAS BALANDYA

Posted on: April 28th, 2024

MAAFISA TARAFA NA WATENDAJI,TUMIENI MAFUNZO HAYA MKATOE HUDUMA BORA KWA WANANCHI:RAS BALANDYA


Katibu Tawala wa Mkoa wa Mwanza Balandya Elikana leo Aprili 28, 2024 amefungua kikao kazi kwa Maafisa Tarafa na Watendaji Kata kutoka wilaya zote za mkoa huo na kuwataka kuyazingatia mafunzo hayo ili wakatoe huduma bora kwa wananchi.

Akizungumza na washiriki hao kwenye ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Balandya amebainisha bado baadhi ya maafisa hao hawatekelezi ipasavyo majukumu yao na kusababisha mlolongo wa kero za wananchi kutotatuliwa.

"Nikushukuru Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Tawala za Mikoa -TAMISEMI kwa kutuletea mafunzo haya, Serikali inatambua umuhimu wa watumishi hawa  miradi mingi imeanzia maeneo yao,"amesisitiza Mtendaji huyo wa Mkoa.

Amesema matarajio ya Serikali baada ya kutoa mafunzo hayo yanayotolewa nchi nzima ni kuona shughuli zote za  Serikali ikiwemo miradi na huduma kwa wananchi zinatolewa kwa kiwango bora na kwa wakati na pia usimamizi na ufuatiliaji ukifanyika kwa umakini.

"Maafisa Tarafa nyie ni wasaidizi wa Wakuu wa Wilaya,hakikisheni mnatimiza vizuri majukumu yenu kwa kuwahamasisha wananchi kushiriki shughuli za maendeleo kwenye Tarafa,"Katibu Tawala Mkoa.

Pia amewakumbusha Watendaji kata kuwa wabunifu na kuweka mpango kazi wa Maendeleo ya kata na kuwasilisha kwa Mkurugenzi wa Halmashauri kupitia kwa Maafisa Tarafa.

"Ndugu Katibu Tawala wa Mkoa hadi sasa jumla ya Mkoa 16 imepata mafunzo haya tunayotoa kwa awamu,hii ni awamu ya tatu ikihusisha Mikoa ya Mwanza,Simiyu,Geita na Kagera na tunatarajia kukamilisha yote kabla ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa utakaofanyika baadaye mwaka huu",Ibrahimu Minja,Mkurugenzi Msaidizi,Idara ya Tawala za Mikoa,Tamisemi.

Mafunzo hayo ya siku mbili yanatolewa na Wakufunzi kutoka Chuo cha Utumishi wa Umma na Chuo cha Mamlaka ya Serikali za Mitaa.

Matangazo

  • Tangazo la kukutana na Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Mwanza kwa shida mbalimbali. January 08, 2025
  • TANGAZO LA NANENANE TAREHE 8.8.2025 January 08, 2025
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • UZALISHAJI ZAO LA PAMBA WAONGEZEKA- MSIGWA

    May 03, 2025
  • DARAJA LA KIGONGO-BUSISI KUANZA KUTUMIKA MUDA WOWOTE KUANZIA SASA.

    May 02, 2025
  • SERIKALI YAANIKA TAKWIMU ZA MAENDELEO YA UTUMISHI YALIYOPATIKANA MWANZA

    May 01, 2025
  • MAKUNDI MAWILI YA MWISHO YALIYOFANYA ZIARA HIFADHI NA JNHPP YAWASILISHA NENO LA SHUKRANI KWA RAS BALANDYA

    April 29, 2025
  • Angalia zote

Video zinazotembea

Siku 365 za Mhe.Rais Samia Suluhu Hassan Mwanza
video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Fomu ya Ugonjwa
  • FFARS User Guidelines
  • Miongozo ya mfumo wa bajeti na Mipango
  • Makusanyo ya Ndani ya Halmashauri za Mkoa wa Mwanza
  • PReM
  • Maswali Yaulizwayo Mara kwa Mara
  • Opras fomu
  • OFISI MTANDAO

Viunganishi Linganishi

  • Tovuti ya Ikulu
  • Utumishi
  • Tamisemi
  • Ofisi ya Taifa ya Takwimu Tanzania
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Kuu ya Serikali

Watembeleaji

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive

    S.L.P: 119, Mwanza.

    Simu: 028-2501037

    Simu ya Mkononi: 028-2501037

    Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.