• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
Mwanza Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Mwanza

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia ya Mkoa
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti Mkoa
    • Seksheni
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Serikali za Mitaa
      • Afya
      • Elimu
      • Maji
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa Ndani
      • ununuzi na Ugavi
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Kitengo cha Sheria
  • Wilaya
    • Ilemela
    • Nyamagana
    • Magu
    • Misungwi
    • Kwimba
    • Sengerema
    • Ukerewe
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Jiji la Mwanza
    • Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
    • Hamashauri ya Wilaya ya Magu
    • Hamashauri ya Wilaya ya Sengerema
    • Hamashauri ya Wilaya ya Misungwi
    • Hamashauri ya Wilaya ya Kwimba
    • Hamashauri ya Wilaya ya Ukerewe
    • Hamashauri ya Wilaya ya Buchosa
  • Fursa za uwekezaji
    • Miundombinu ya Umwagiliaji na kilimo cha mkataba
    • Kilimo
    • Madini
    • Sekta ya Huduma
  • Huduma zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Watumishi
  • Machapisho
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa Kwa vyombo vya habari
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya video

Mafundi ujenzi vyumba vya Madarasa Ilemela waonesha uzalendo kufanikisha lengo la Mkoa

Posted on: July 27th, 2022


Shule ya Msingi Kahama wilayani Ilemela imepokea kijiti cha kampeni ya Mkoa ya Ujenzi wa vyumba vya madarasa ikiwa ni siku ya tatu tangu ilipoanza ambapo wananchi wamechimba Msingi wa vyumba vya Madarasa 9 katika kukabiliana na msongamano kwenye shule hiyo unaosababishwa na upungufu wa vyumba 38.

Akiongoza kampeni hiyo, Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. Mhandisi Robert Gabriel amesema changamoto yoyote kwenye jamii inatatuliwa kwa urahisi zaidi endapo watashirikiana wananchi wenyewe kuitatua, na ndio maana Mkoa umeona umalize tatizo la msongamano wa vyumba vya Madarasa kwa kuchangia nguvu wenyewe kwanza na madarasa hayo yakifika hatua fulani basi Serikali itaongezea nguvu.

"Upungufu wa Madarasa 38 kwenye shule moja inatafsiri kuwa watoto wetu hawana pa kusomea ndio maana tumekuja hapa chini ya kampeni ya Mkoa ya kuanzisha ujenzi wa Madarasa na kukomesha kabisa tatizo hili sugu na Mbunge wetu Mahiri wa Jimbo hili ametupa baraka zote kwani anawapenda sana."

"Tumeanza  kampeni ya zaidi ya Bilioni 200 tukiwa hatuna hata shilingi moja na tutafanikiwa maana hakuna jambo jema linakwama kwa Mwenyezi Mungu, nawashukuru sana mafundi wangu kwa kuamua kujenga madarasa haya kwa nusu bei." Mkuu wa Mkoa.

Pamoja na kutoa Mchango wa Matofali 500 kwenye Ujenzi huo, Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Mwanza Mhe. Kabula Shitobelo amempongeza Mkuu wa Mkoa kwa kujitoa sio tu kwa kuanzisha kampeni hiyo bali kuitendea haki kwa vitendo kwani amekua akishirikiana na wananchi kuchimba msingi wa Madarasa kwenye kila wilaya kazi inayofanywa kuanzia saa 11 alfajiri.

Mhe Hassan Masala, Mkuu wa Wilaya ya Ilemela amebainisha kuwa kwa kushirikiana na Idara ya Elimu zipo taarifa za upungufu wa vyumba vya madarasa 1000 na msongamano upo zaidi kwenye Kata kumi zikiongozwa na Kahama na Buswelu na kwamba wataanzia kwenye maeneo hayo kujenga madarasa.

Meya wa Manispaa ya Ilemela, Mhe. Renatus Mulunga amesema Kata ya Kahama ni hodari wa maendeleo ndani ya kata 19 zilizo kwenye Halmashauri hiyo na kutokana na suala hilo Halmashauri yake itachangia zaidi ya Milioni 2 zilizobakia kukamilisha suala la Kiwanja cha ujenzi wa shule mpya kabla ya kuleta nguvu kubwa kwenye Ujenzi wa madarasa yenyewe.

"Tuna upungufu wa vyumba vya Madarasa 38 kwenye shule ya msingi Kahama na idadi hiyo imetufanya tutafute eneo la kujenga shule ingine na ndipo viongozi na wananchi wa Mtaa huu waliamua kununua eneo hili na tutajenga madarasa 15 hapa na kwenye Mtaa wa Isela tutajenga 15 na pale kwenye shule mama tutajenga vyumba 8" Amesema Masala.

"Suala la ujifunzaji linakua changamoto kutokana na msongamano wa wanafunzi hali ambayo kwenye madarasa mengine wanafunzi wanakaa hadi mlangoni hivyo Ujenzi wa vyumba vipya utasaidia sana na tunakushukuru serikali ya Rais Mama Samia na viongozi wote kwa kuamua kutupunguzia adha hiyo." Mwalimu Johari Maluba kutoka Shule Msingi Kahama.

Bi. Tedi Shibola amesema kwa kipindi kirefu wananchi wa Mtaa wa Kahama wamekua wakitafakari ni wapi watapata eneo la Kujenga shule ingine maana kumekua na msongamano mkubwa wa wanafunzi kwenye shule ya Msingi Kahama hivyo sasa wanaishukuru serikali kwa kusikia kilio chao na kuja kuanzisha shule mpya ndani ya kata hiyo.

Matangazo

  • Tangazo la kukutana na Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Mwanza kwa shida mbalimbali. January 08, 2025
  • TANGAZO LA NANENANE TAREHE 8.8.2025 January 08, 2025
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • LENGO LA HOSPITALI ZA WILAYA NI KILA MWANANCHI APATE HUDUMA MAHALI ALIPO - WAZIRI MKUU

    May 19, 2025
  • MITAMBO YA KUOPOA MAGUGUMAJI KUWASILI MWISHONI MWA MWEZI JULAI.

    May 19, 2025
  • WAZIRI MKUU AWATAKA WANAMALYA KUCHANGAMKIA FURSA YA CHUO CHA MICHEZO

    May 18, 2025
  • NIA YA SERIKALI KILA MWANANCHI AUNGANISHIWE MAJI NYUMBANI KWAKE - WAZIRI MKUU

    May 18, 2025
  • Angalia zote

Video zinazotembea

Siku 365 za Mhe.Rais Samia Suluhu Hassan Mwanza
video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Fomu ya Ugonjwa
  • FFARS User Guidelines
  • Miongozo ya mfumo wa bajeti na Mipango
  • Makusanyo ya Ndani ya Halmashauri za Mkoa wa Mwanza
  • PReM
  • Maswali Yaulizwayo Mara kwa Mara
  • Opras fomu
  • OFISI MTANDAO

Viunganishi Linganishi

  • Tovuti ya Ikulu
  • Utumishi
  • Tamisemi
  • Ofisi ya Taifa ya Takwimu Tanzania
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Kuu ya Serikali

Watembeleaji

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive

    S.L.P: 119, Mwanza.

    Simu: 028-2501037

    Simu ya Mkononi: 028-2501037

    Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.