• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
Mwanza Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Mwanza

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia ya Mkoa
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti Mkoa
    • Seksheni
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Serikali za Mitaa
      • Afya
      • Elimu
      • Maji
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa Ndani
      • ununuzi na Ugavi
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Kitengo cha Sheria
  • Wilaya
    • Ilemela
    • Nyamagana
    • Magu
    • Misungwi
    • Kwimba
    • Sengerema
    • Ukerewe
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Jiji la Mwanza
    • Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
    • Hamashauri ya Wilaya ya Magu
    • Hamashauri ya Wilaya ya Sengerema
    • Hamashauri ya Wilaya ya Misungwi
    • Hamashauri ya Wilaya ya Kwimba
    • Hamashauri ya Wilaya ya Ukerewe
    • Hamashauri ya Wilaya ya Buchosa
  • Fursa za uwekezaji
    • Miundombinu ya Umwagiliaji na kilimo cha mkataba
    • Kilimo
    • Madini
    • Sekta ya Huduma
  • Huduma zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Watumishi
  • Machapisho
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa Kwa vyombo vya habari
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya video

Mafunzo ya Usimamizi wa Maafa Yafanyika mwanza

Posted on: April 17th, 2019


Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. John Mongella amebainisha kuwa takribani ajali za majini  zaidi ya mia tatu huripotiwa kuwa zimetokea mkoani humo. Ajali hizo ni zile ambazo huripotiwa rasmi  tu  katika mamlaka husika , aidha inasadikika zipo ajali nyingi ambazo hutokea lakini huwa haziripitiwi  kutokana na jiografia ya mkoa huo. Mkoa wa Mwanza una visiwa zaidi ya 162 ambapo kati ya Visiwa hivyo vipo ambavyo watu wanayo makazi ya kudumu na vingine watu huishi kwa muda mfupi.

Akiongea wakati  akifungua Mafunzo kwa Kamati  ya  Usimamizi wa maafa  ya mkoa huo,  yaliyoratibiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu, Idara ya Uratibu wa shughulii za maafa Leo, tarehe 17 Aprili, 2019, jiijini Mwanza, Mongella amefafanua kuwa ajali za vyombo vya usafiri hasa vya majini zinaweza kupunguzwa sana kama wamiliki na waendeshaji wa vyombo hivyo watazingatia sheria na Kanuni  zinazotawala uendeshaji wa vyombo hivyo.

“Suala muhimu la Kuzingatia ni kuhakikisha mamlaka zetu za serikali za mitaa zinaimarisha utawala bora unaotoa nafasi kwa  jamii kushiriki katika kuzuia na Kupunguza madhara ya majanga, kujiandaa, kukabili na kurejesha hali baada ya maafa kutokea ikiwa ni pamoja na kutoa elimu, taarifa za tahadhari ya awali kwa wakati muafaka na kuandaa rasilimali zinazohiotajika , Ni wajibu wetu kuhakikisha sheria zinasimamiwa kikamilifu ili kuepuka maafa“ alisisitiza Mongella.


Naye Mkurugenzi wa Uratibu wa Shughuli za Maafa, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kanali, Jimmy Matamwe, ameitaka Kamati ya Usimamizi wa Maafa ya mkoa huo  kuandaa Mkakati wa Kupunguza madhara  ya maafa pamoja na Mpango wa kujiandaa na kukabili maafa, Aidha, ameeleza kuwa  Ofisi ya waziri Mkuu imeendesha mafunzo hayo  ili kuijengea uwezo kamati hiyo ambayo ni chombo cha kisheria hapa nchini kwa ajili ya kutathimini na kutekeleza masuala ya kitaalam kuhusu usimamizi wa maafa, kuzuia na kupunguza madhara ya majanga ya aina zote katika mkoa.

“Upunguzaji wa madhara ya maafa ni suala mtambuka linalohusika katika shughuli za maendeleo ya kiuchumi na kijamii sekta zote. Suala la usimamizi wa maafa linahitaji utashi wa kisiasa na kuwajibika kitaalam, kisheria, uelewa wa umma, elimu ya kisayansi, mipango makini ya maendeleo, ufanisi wa utekelezaji wa sera, mifumo ya tahadhari inayojibu matakwa ya jamii” alisema  Kanali., Matamwe.

Mwaka jana, Mwezi Septemba, mkoa wa Mwanza ulipata maafa makubwa baada ya Kivuko cha MV. Nyerere kuzama na kupoteza maisha ya watu zaidi ya 200 na wengine 40 waliokolewa. Kufuatia maafa hayo Mkoa huo umeendelea na jitihada za kuzijengea uwezo kamati za Usimamizi wa Maafa za mkoa huo.

Mafunzo hayo yaliyoratibiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu, Idara ya Uratibu wa shughuli za maafa, yamehudhuriwa na wajumbe wote wa Kamati ya Usimamizi wa maafa kwa kuzingatia Kifungu cha 13 cha sheria ya Usimamizi wa Maafa Na. 7 ya mwaka 2015.


Matangazo

  • Tangazo la kukutana na Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Mwanza kwa shida mbalimbali. January 08, 2025
  • TANGAZO LA NANENANE TAREHE 8.8.2025 January 08, 2025
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • UZALISHAJI ZAO LA PAMBA WAONGEZEKA- MSIGWA

    May 03, 2025
  • DARAJA LA KIGONGO-BUSISI KUANZA KUTUMIKA MUDA WOWOTE KUANZIA SASA.

    May 02, 2025
  • SERIKALI YAANIKA TAKWIMU ZA MAENDELEO YA UTUMISHI YALIYOPATIKANA MWANZA

    May 01, 2025
  • MAKUNDI MAWILI YA MWISHO YALIYOFANYA ZIARA HIFADHI NA JNHPP YAWASILISHA NENO LA SHUKRANI KWA RAS BALANDYA

    April 29, 2025
  • Angalia zote

Video zinazotembea

Siku 365 za Mhe.Rais Samia Suluhu Hassan Mwanza
video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Fomu ya Ugonjwa
  • FFARS User Guidelines
  • Miongozo ya mfumo wa bajeti na Mipango
  • Makusanyo ya Ndani ya Halmashauri za Mkoa wa Mwanza
  • PReM
  • Maswali Yaulizwayo Mara kwa Mara
  • Opras fomu
  • OFISI MTANDAO

Viunganishi Linganishi

  • Tovuti ya Ikulu
  • Utumishi
  • Tamisemi
  • Ofisi ya Taifa ya Takwimu Tanzania
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Kuu ya Serikali

Watembeleaji

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive

    S.L.P: 119, Mwanza.

    Simu: 028-2501037

    Simu ya Mkononi: 028-2501037

    Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.