• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
Mwanza Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Mwanza

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia ya Mkoa
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti Mkoa
    • Seksheni
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Serikali za Mitaa
      • Afya
      • Elimu
      • Maji
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa Ndani
      • ununuzi na Ugavi
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Kitengo cha Sheria
  • Wilaya
    • Ilemela
    • Nyamagana
    • Magu
    • Misungwi
    • Kwimba
    • Sengerema
    • Ukerewe
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Jiji la Mwanza
    • Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
    • Hamashauri ya Wilaya ya Magu
    • Hamashauri ya Wilaya ya Sengerema
    • Hamashauri ya Wilaya ya Misungwi
    • Hamashauri ya Wilaya ya Kwimba
    • Hamashauri ya Wilaya ya Ukerewe
    • Hamashauri ya Wilaya ya Buchosa
  • Fursa za uwekezaji
    • Miundombinu ya Umwagiliaji na kilimo cha mkataba
    • Kilimo
    • Madini
    • Sekta ya Huduma
  • Huduma zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Watumishi
  • Machapisho
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa Kwa vyombo vya habari
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya video

Makinda awataka wasomi na wananchi kuyatumia matokeo ya Sensa ya Watu na Makazi kujiinua kiuchumi

Posted on: March 29th, 2023


Kamisaa wa Sensa ya Watu na Makazi mwaka 2022, Mheshimiwa Anne Makinda amewashauri wasomi na Wananchi Nchini kutumia takwimu za sensa ya watu na Makazi katika kubuni biashara ili waweze kujikwamua kiuchumi.

Mheshimiwa Makinda ametoa ushauri huo leo Machi 29, 2023 wakati akizungumza na   wananchi pamoja na viongozi kutoka makundi mbalimbali Wilaya ya Ilemela Mkoani Mwanza kuhusu matumizi ya Matokeo ya  Sensa ya watu na Makazi  2022 katika kupanga  na kutekeleza Mipango ya Maendeleo.

 Amesema  Serikali haikufanya sensa ili takwimu  hizo zikae kwenye shelfu zake bali ziwasaidie watanzania kuona fursa ili wazitumie kujikwamua kiuchumi wao na taifa kwa ujumla.

Amesema kwa mujibu wa sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2022  zaidi ya nusu yao  ni kundi lenye uwezo wa kufanya kazi hivyo wote wakishiriki kikamilifu katika shughuli za kiuchumi watajikwamua wao, familia zao na taifa kwa ujumla.

 "Tuanze kufikiri kitakwimu badala ya kufanya kazi kama watu tuliofungwa kitambaa usoni, sensa iwafungue wasomi na vijana kuona fursa, fanyeni biashara na dunia nzima  kimtandao.

"Fursa zinakwenda na wakati hazirudi mara mbili ukichelewa zitakuacha  wasomi acheni kuchagua kazi  kikubwa ninachoweza kuwashauri  kuweni waaminifu   tatizo letu asilimia kubwa si waaminifu kama tukiendelea kufanya kazi kwa udanganyifu kama ambavyo wengi wetu walivyozoea itakula kwetu," amesema Mheshimiwa Makinda na kuongeza.

"Ukichagua kazi hautapata kazi mpaka utastaafu(utazeeka) kabla ya kuajiriwa,"amesema.


Akizungumzia kuhusu takwimu za Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2022, Mheshimiwa Makonda amewashukuru watanzania kwa kujitokeza kwa wingi kuhesabiwa hali iliyosaidia zoezi hilo kufanikiwa kwa kiwango kikubwa.

Mkuu wa Wilaya ya Ilemela Mkoani Mwanza Hassan Masala amesema Wilaya hiyo ilitekeleza zoezi la sensa kwa heshima na umakini mkubwa ndiyo maana wamepata fursa ya kuwa miongoni mwa maeneo ya mfano ambayo Kamisaa Makinda amewapendekeza kuyafikia.

"Wilaya ya Ilemela tulitekeleza zoezi la sensa ya watu na Makazi iliyofanyika mwaka jana kwa weledi mkubwa na tuko tayari kuyafanyia kazi maelekezo yote utakayotoa leo,"amesema Mheshimiwa Masala

Naye Meneja Takwimu wa Mkoa wa Mwanza, Goodluck Lyimo amesema  asilimia kubwa  ya wakazi wa mkoa huo walijitokeza kuhesabiwa  hali iliyosaidia kufanikisha zoezi hilo kwa kiwango kikubwa.

Matangazo

  • Tangazo la kukutana na Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Mwanza kwa shida mbalimbali. January 08, 2025
  • TANGAZO LA NANENANE TAREHE 8.8.2025 January 08, 2025
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • UZALISHAJI ZAO LA PAMBA WAONGEZEKA- MSIGWA

    May 03, 2025
  • DARAJA LA KIGONGO-BUSISI KUANZA KUTUMIKA MUDA WOWOTE KUANZIA SASA.

    May 02, 2025
  • SERIKALI YAANIKA TAKWIMU ZA MAENDELEO YA UTUMISHI YALIYOPATIKANA MWANZA

    May 01, 2025
  • MAKUNDI MAWILI YA MWISHO YALIYOFANYA ZIARA HIFADHI NA JNHPP YAWASILISHA NENO LA SHUKRANI KWA RAS BALANDYA

    April 29, 2025
  • Angalia zote

Video zinazotembea

Siku 365 za Mhe.Rais Samia Suluhu Hassan Mwanza
video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Fomu ya Ugonjwa
  • FFARS User Guidelines
  • Miongozo ya mfumo wa bajeti na Mipango
  • Makusanyo ya Ndani ya Halmashauri za Mkoa wa Mwanza
  • PReM
  • Maswali Yaulizwayo Mara kwa Mara
  • Opras fomu
  • OFISI MTANDAO

Viunganishi Linganishi

  • Tovuti ya Ikulu
  • Utumishi
  • Tamisemi
  • Ofisi ya Taifa ya Takwimu Tanzania
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Kuu ya Serikali

Watembeleaji

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive

    S.L.P: 119, Mwanza.

    Simu: 028-2501037

    Simu ya Mkononi: 028-2501037

    Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.