• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
Mwanza Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Mwanza

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia ya Mkoa
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti Mkoa
    • Seksheni
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Serikali za Mitaa
      • Afya
      • Elimu
      • Maji
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa Ndani
      • ununuzi na Ugavi
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Kitengo cha Sheria
  • Wilaya
    • Ilemela
    • Nyamagana
    • Magu
    • Misungwi
    • Kwimba
    • Sengerema
    • Ukerewe
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Jiji la Mwanza
    • Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
    • Hamashauri ya Wilaya ya Magu
    • Hamashauri ya Wilaya ya Sengerema
    • Hamashauri ya Wilaya ya Misungwi
    • Hamashauri ya Wilaya ya Kwimba
    • Hamashauri ya Wilaya ya Ukerewe
    • Hamashauri ya Wilaya ya Buchosa
  • Fursa za uwekezaji
    • Miundombinu ya Umwagiliaji na kilimo cha mkataba
    • Kilimo
    • Madini
    • Sekta ya Huduma
  • Huduma zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Watumishi
  • Machapisho
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa Kwa vyombo vya habari
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya video

Mikakati ya kufanikisha nanenane Yasisitizwa Mwanza

Posted on: July 26th, 2019

Kikao cha Maandalizi ya Maonesho ya Kilimo (Nane Nane) Kanda ya Ziwa Magharibi kimefanyika katika Ukumbi wa ofisi ya mkuu wa mkoa wa Mwanza.

Akifungua kikao hicho kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa,Katibu Tawala wa mkoa wa Mwanza Christopher Kadio amesisitiza Halmashauri zote za kanda ya ziwa magharibi kushiriki kikamilifu katika Maonyesho ya mwaka huu na kuwataka washiriki wa kikao kutoa mawazo ya kuboresha maonyesho ya mwaka huu.

Aidha amezitaka Halmashauri zinazodaiwa michango ya maandalizi ya shughuli za nanenane kumalizia michango hiyo kwa wakati.

Awali akiwasilisha mada ya mapato na matumizi ya maadhimisho ya nane nane  Katibu Tawala Msaidizi Uchumi na Uzalishaji  Emil Kasagala amesema kiasi cha Shilingi 120,939,400 zimekisiwa kutumika kufanikisha maadhimisho ya mwaka huu kwa kanda ya Ziwa Magharibi.

Akichangia kikao hicho Mkuu wa Wilaya ya Geita Mhe. Josephat Maganga aliyemwakilisha Mkuu wa Mkoa Geita  amesisitiza mshikamano na ushirikiano miongoni mwa Halmashauri na Mikoa shiriki kama nguzo muhimu ya mafanikio ya maadhimisho haya ya Nane nane 2019.

Akihitimisha kikao hicho Katibu Tawala Mkoa wa Mwanza Christopher Kadio amewashukuru wajumbe wote waliohudhuria na kusema  kuwa mambo mazuri hufanywa na watu wachache ila yakifanikiwa wanakuwa wengi zaidi hana wasiwasi na uchache wa wajumbe na kuonyesha imani kubwa ya mafanikio.

Naye Mwakilishi wa Mkuu wa Mkoa wa Geita ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Geita ameahirisha kikao kwa kuwashukuru washiriki wote kwa usikivu,utulivu na hasa kwa mawazo ya michango na kusema kuwa anaamini mawazo yote yatarejea katika Halmashauri zote na kufanyiwa kazi kama maekezo yalivyotolewa.

Matangazo

  • Tangazo la kukutana na Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Mwanza kwa shida mbalimbali. January 08, 2025
  • TANGAZO LA NANENANE TAREHE 8.8.2025 January 08, 2025
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • UZALISHAJI ZAO LA PAMBA WAONGEZEKA- MSIGWA

    May 03, 2025
  • DARAJA LA KIGONGO-BUSISI KUANZA KUTUMIKA MUDA WOWOTE KUANZIA SASA.

    May 02, 2025
  • SERIKALI YAANIKA TAKWIMU ZA MAENDELEO YA UTUMISHI YALIYOPATIKANA MWANZA

    May 01, 2025
  • MAKUNDI MAWILI YA MWISHO YALIYOFANYA ZIARA HIFADHI NA JNHPP YAWASILISHA NENO LA SHUKRANI KWA RAS BALANDYA

    April 29, 2025
  • Angalia zote

Video zinazotembea

Siku 365 za Mhe.Rais Samia Suluhu Hassan Mwanza
video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Fomu ya Ugonjwa
  • FFARS User Guidelines
  • Miongozo ya mfumo wa bajeti na Mipango
  • Makusanyo ya Ndani ya Halmashauri za Mkoa wa Mwanza
  • PReM
  • Maswali Yaulizwayo Mara kwa Mara
  • Opras fomu
  • OFISI MTANDAO

Viunganishi Linganishi

  • Tovuti ya Ikulu
  • Utumishi
  • Tamisemi
  • Ofisi ya Taifa ya Takwimu Tanzania
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Kuu ya Serikali

Watembeleaji

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive

    S.L.P: 119, Mwanza.

    Simu: 028-2501037

    Simu ya Mkononi: 028-2501037

    Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.