• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
Mwanza Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Mwanza

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia ya Mkoa
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti Mkoa
    • Seksheni
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Serikali za Mitaa
      • Afya
      • Elimu
      • Maji
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa Ndani
      • ununuzi na Ugavi
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Kitengo cha Sheria
  • Wilaya
    • Ilemela
    • Nyamagana
    • Magu
    • Misungwi
    • Kwimba
    • Sengerema
    • Ukerewe
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Jiji la Mwanza
    • Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
    • Hamashauri ya Wilaya ya Magu
    • Hamashauri ya Wilaya ya Sengerema
    • Hamashauri ya Wilaya ya Misungwi
    • Hamashauri ya Wilaya ya Kwimba
    • Hamashauri ya Wilaya ya Ukerewe
    • Hamashauri ya Wilaya ya Buchosa
  • Fursa za uwekezaji
    • Miundombinu ya Umwagiliaji na kilimo cha mkataba
    • Kilimo
    • Madini
    • Sekta ya Huduma
  • Huduma zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Watumishi
  • Machapisho
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa Kwa vyombo vya habari
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya video

Miradi Mikubwa ya maji kuwanufaisha wananchi Magu

Posted on: January 28th, 2020

Zaidi ya wananchi laki moja wilayani Magu Mkoani Mwanza wanatarajia kunufaika  na mradi mkubwa wa maji kutoka ziwa Victoria uliojengwa na Serikali kwa gharama ya Sh.bilioni 16, ukitarajiwa kuzifikia baadhi ya wilaya za Mkoa huo  ikiwemo wilaya ya Misungwi.

Akizungumza wakati akiwasilisha taarifa ya kituo cha usambazaji maji kilichopo kitongoji cha Busulwa wilayani Magu kwa Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Mkoa wa Mwanza, Mkuu wa Wilaya hiyo Dkt. Philemon Sengati alisema changamoto kubwa iliyokuwa ikiwakabili wananchi wa Magu ni ukosefu wa maji safi na salama ya uhakika japo kuwa wapo mita chache kutoka ziwa Victoria.

Alisema  kukamilika kwa mradi huo mwezi Septemba mwaka jana  umekuwa mkombozi kwa wananchi ambapo hali ya upatikanaji wa maji kwa wilaya hiyo ni zaidi ya asilimia 80 ,huku upatikanaji wa maji kwa eneo lengwa ambalo ni Magu mjini likiwa ni zaidi ya asilimia 100 ambapo uzalishaji huo unauwezo wa kuzalisha maji lita za ujazo million 7 zenye uwezo wa kukudhi mahitaji ya watu zaidi ya laki moja.


“Pia tunayo miradi mingine katika maeneo mbalimbali ya pembezoni ambayo inaendelea huku mingine ikiwa imekamilika mfano kata ya Lugeye, Nsolwa bubinza na Kitongosima ambayo yote imefadhiliwa na serikali yenye lengo la kuwaondolea wananchi changamoto zilizokuwa zikiwakabili”alisema Sengati.

Kwa upande wake Katibu wa CCM mkoa wa Mwanza Salum Kalli amewataka watendaji wa serikali wawe waaminifu na watekeleze miradi ya serikali kwa viwango vilivyo bora na kwa wakati ili kuhakikisha wananchi wanapata huduma pasipo kuhujumu miundombinu mbalimbali inayotekelezwa.


Naye Mwakilishi wa Mkuu wa mkoa wa Mwanza ambaye ni Mkuu wa wilaya ya Ilemela Mhe.Dkt. Severine Lalika alisema Mradi huo wa maji ukitumika vizuri kwa wakazi wa Magu pato lake litakuza uchumi wa wilaya hiyo na taifa kwa ujumla.


Paulo Shabani na Samson Gibui Wakazi wa kijiji cha Busulwa waliipongeza serikali kuwajenge mradi huo ambao umeweza kuwaepusha na magonjwa ya mlipuko yaliyokuwa yakiwatesa kipindi cha nyuma kutokana na  kutokutumia maji yasiyokuwa safi na salama .


“ Tulikuwa tukitumia maji ya ziwani tena bila kuchemshwa hivyo tulipata magonjwa ya mlipuko kama magonjwa ya tumbo (Typhoid), lakini kwa sasa tunapata maji yaliyo safi na salama tena yenye dawa” alisema Gibui.


Wajumbe wa Halmashauri kuu ya CCM mkoa wa Mwanza walifanya ziara ya ukaguzi wa miradi ya maendeleo ambapo wameweza kukagua miradi mbalimbali inayotekelezwa na serikali ikiwemo ujenzi wa  jengo la kuhifadhi mizigo, jengo la abiria, mnara wa kuongozea ndege, urefushaji wa barababara ya kuruka na kutua ndege kwa mita 500,  kukagua maendeleo ya ujenzi wa vivuko vipya vitakavyokuwa vinafanya kazi katika maeneo ya Kayenze, Bezi ,Chato,Nkome ,Bugorola na Ukara.


Pia waliendelea na ukaguzi wa miradi ya ujenzi wa chelezo, ujenzi wa meli mpya ndani ya ziwa Victoria ,ukarabati wa meli za Mv.Viktoria na Mv.Butiama , ukaguzi wa maendeleo  ya ujenzi wa daraja lenye urefu wa kilometa 3.2 linalojengwa busisi na kigongo pamoja na kukagua maendeleo ya ujenzi wa mradi wa maji wilayani Magu unaosimamiwa na MWAUWASA.









Matangazo

  • Tangazo la kukutana na Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Mwanza kwa shida mbalimbali. January 08, 2025
  • TANGAZO LA NANENANE TAREHE 8.8.2025 January 08, 2025
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • UZALISHAJI ZAO LA PAMBA WAONGEZEKA- MSIGWA

    May 03, 2025
  • DARAJA LA KIGONGO-BUSISI KUANZA KUTUMIKA MUDA WOWOTE KUANZIA SASA.

    May 02, 2025
  • SERIKALI YAANIKA TAKWIMU ZA MAENDELEO YA UTUMISHI YALIYOPATIKANA MWANZA

    May 01, 2025
  • MAKUNDI MAWILI YA MWISHO YALIYOFANYA ZIARA HIFADHI NA JNHPP YAWASILISHA NENO LA SHUKRANI KWA RAS BALANDYA

    April 29, 2025
  • Angalia zote

Video zinazotembea

Siku 365 za Mhe.Rais Samia Suluhu Hassan Mwanza
video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Fomu ya Ugonjwa
  • FFARS User Guidelines
  • Miongozo ya mfumo wa bajeti na Mipango
  • Makusanyo ya Ndani ya Halmashauri za Mkoa wa Mwanza
  • PReM
  • Maswali Yaulizwayo Mara kwa Mara
  • Opras fomu
  • OFISI MTANDAO

Viunganishi Linganishi

  • Tovuti ya Ikulu
  • Utumishi
  • Tamisemi
  • Ofisi ya Taifa ya Takwimu Tanzania
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Kuu ya Serikali

Watembeleaji

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive

    S.L.P: 119, Mwanza.

    Simu: 028-2501037

    Simu ya Mkononi: 028-2501037

    Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.