• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
Mwanza Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Mwanza

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia ya Mkoa
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti Mkoa
    • Seksheni
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Serikali za Mitaa
      • Afya
      • Elimu
      • Maji
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa Ndani
      • ununuzi na Ugavi
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Kitengo cha Sheria
  • Wilaya
    • Ilemela
    • Nyamagana
    • Magu
    • Misungwi
    • Kwimba
    • Sengerema
    • Ukerewe
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Jiji la Mwanza
    • Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
    • Hamashauri ya Wilaya ya Magu
    • Hamashauri ya Wilaya ya Sengerema
    • Hamashauri ya Wilaya ya Misungwi
    • Hamashauri ya Wilaya ya Kwimba
    • Hamashauri ya Wilaya ya Ukerewe
    • Hamashauri ya Wilaya ya Buchosa
  • Fursa za uwekezaji
    • Miundombinu ya Umwagiliaji na kilimo cha mkataba
    • Kilimo
    • Madini
    • Sekta ya Huduma
  • Huduma zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Watumishi
  • Machapisho
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa Kwa vyombo vya habari
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya video

Mkoa wa Mwanza wachukua hatua kukabiliana na ugonjwa wa Marburg

Posted on: March 24th, 2023


Mkoa wa Mwanza umeishachukua hatua mbalimbali ili kukabiliana na homa inayosababishwa na Virus vya Marburg ikiwemo kuwapa watumishi wa afya  mafunzo mahususi   ya kuhudumia wagonjwa, kutenga maeneo maalum  ya kuwahudumia wagonjwa wa ugonjwa huo na kuwaelimisha wananchi kuhusu ugonjwa wa Marburg na jinsi ya kujikinga.

Ikumbukwe kwamba Machi 21, 2023 Waziri wa Afya Ummy Mwalimu alitoa taarifa kwa Umma kwamba uchunguzi wa kimaabara uliofanyika katika Maabara ya Taifa ya Jamii umethibitisha uwepo wa ugonjwa wa homa inayosababishwa na Virus vya Marburg mkoani Kagera ambapo kulikuwa na  juma ya wagonjwa  nane kati yao watano walifariki na watatu wanaendeleana matibabu katika vituo vya kutolea huduma za afya vilivyoandaliwa Mkoani humo.

Akizungumza leo Machi2 4,2023  kwenye kikao kilichokutanisha  wadau mbalimbali wakiwemo viongozi wa dini, wavuvi, na machinga kilicholenga kuwaelimisha kuhusu ugonjwa huo, dalli, jinsi ya kujikinga, unavyoambukizwa na  athari zake, Mratibu wa Elimu ya Afya kwa Umma Mkoa wa Mwanza, Renard Mlyakado amesema hadi sasa jumla ya watumishi 94 kutoka Wilaya nne kati ya  saba zilizopo mkoani humo wamekwishapata mafunzo jinsi ya kuhudumia wagonjwa wa ugonjwa huo na mafunzo yanaendelea katika halmashauri zote na mahala pa kazi.

"Pia halmashauri zote zilizopo mkoani humu zimekwishatenga maeneo maalum ya kuhudumia wagonjwa wa ugonjwa wa Virus vya Marburg ambapo Nyamagana ni Hospitali ya Wilaya na SRRH,Ilemela ni Hospitali ya Wilaya Kabusungu, Kwimba zahanati ya Mwamajila, Misungwi Zahanati ya Igokello, Buchosa ni Hospitali ya Wilaya, Ukerewe ni hospitali ya Nansio na Bwisya, Sengerema  ni zahanati ya Mwabaluhi na Magi ni zahanati ya John Mongela," ameeleza  Mlyakado.

Akieleza namna  ugonjwa huo unavyoambukiza  Mlyakado amesema unaambulizwa kwa haraka kutoka mtu mmoja aliye na Virus vya Ugonjwa huo  hadi mwingine kwa kugusa majimaji ya mwili mfano damu, matapishi, mkojo, jasho, machozi na kamasi,kugusa au kuosha maiti ya mtu aliyefariki kwa ugonjwa huo, kugusa godoro,shuka, blankenti au nguo zilizotumiwa na mgonjwa wa  Ugonjwa wa Virus vya Marburg.

"Ugonjwa huu pia unaambukizwa kwa kuchomwa sindano au vifaa visivyosafi na salama  vilivyotumiwa na ugonjwa wa  Virus vya Marburg, kugusa mizoga au kula wanyama pori kama vile nyani,polo na sokwe na kula matunda yaliyoliwa nusu na wanyama" ameeleza na kutaja dalili za ugonjwa huo.

"Dalili huanza kujitokza kati ya Siku mbili hadi 21 baada ya mtu kupata maambukizi  ikiwemo homa Kali ya ghafla, maumivu ya kichwa, mwili, misuli  na viungo vya mwili, kuharisha  na kutapika kunakoweza kuambatana na damu, vipele mwilini, kuvia damu chini ya ngozi au kutokwa na damu puani, mdomoni,machoni na masikioni," amebainisha Mlyakado.

Mlyakado amesema ugonjwa huo hauna tiba maalum wala chanjo bali ugonjwa hupatiwa tiba saizi kulingana na dalili alizonazo ambapo alisisitiza kwamba  ili kukabiliana na mlipuko wa Ugonjwa wa  Virus vya Marburg kila mtu na sekta ashiriki na atimize wajibu wake kwa kushirikiana na wataalamu wa afya katika kutoa elimu kwa Umma juu ya ugonjwa huo.

Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Mwanza, Mbunifu wa Majengo Chagu Ng'homa ameitaka jamii kutokuwa na hofu kwa kuwa Mkoa huo umejipanga kukabiliana na kuingia kwa ugonjwa huo ikiwa ni pamoja na kutoka elimu kwa wananchi jinsi ya kujikinga ili wasipate maambukizi.

"Tunatakiwa tupambane na hili janga bila kuleta taharuki kwa jamii natambua kwamba Ugonjwa wa Virus vya Marburg  husababisha unyanyapaa  na athari za kisaikolojia kwa waathirika na familia zao na pia ni gharama kubwa kuhudumia wagonjwa wa ugonjwa huo lakini ni lazima tushirikiane tusiwe na hofu Serikali inaendelea kuchukua hatua mbalimbali  hasa kule Mkoani Kagera ulikoanzia hii inatupa matumaini  na hatujatangaziwa ongezeko la wagonjwa," alisema Ng'homa.

Mganga Mkuu wa Mkoa wa Mwana Dkt.Thomas Rutachunzibwa alisema endapo MTU atakuwa na dalili moja wapo kati ya zilizotajwa au akiona MTU kwenye dalili hizo asimnyanyapae  bali waende  au wawashauri kwenda haraka kwenye vituo vya kutolea huduma za afya, watoe taarifa mapema kwenye vituo cha huduma za afya, oisi ya Serikali ya Mtaa au Kijiji.

Matangazo

  • Tangazo la kukutana na Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Mwanza kwa shida mbalimbali. January 08, 2025
  • TANGAZO LA NANENANE TAREHE 8.8.2025 January 08, 2025
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • UZALISHAJI ZAO LA PAMBA WAONGEZEKA- MSIGWA

    May 03, 2025
  • DARAJA LA KIGONGO-BUSISI KUANZA KUTUMIKA MUDA WOWOTE KUANZIA SASA.

    May 02, 2025
  • SERIKALI YAANIKA TAKWIMU ZA MAENDELEO YA UTUMISHI YALIYOPATIKANA MWANZA

    May 01, 2025
  • MAKUNDI MAWILI YA MWISHO YALIYOFANYA ZIARA HIFADHI NA JNHPP YAWASILISHA NENO LA SHUKRANI KWA RAS BALANDYA

    April 29, 2025
  • Angalia zote

Video zinazotembea

Siku 365 za Mhe.Rais Samia Suluhu Hassan Mwanza
video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Fomu ya Ugonjwa
  • FFARS User Guidelines
  • Miongozo ya mfumo wa bajeti na Mipango
  • Makusanyo ya Ndani ya Halmashauri za Mkoa wa Mwanza
  • PReM
  • Maswali Yaulizwayo Mara kwa Mara
  • Opras fomu
  • OFISI MTANDAO

Viunganishi Linganishi

  • Tovuti ya Ikulu
  • Utumishi
  • Tamisemi
  • Ofisi ya Taifa ya Takwimu Tanzania
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Kuu ya Serikali

Watembeleaji

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive

    S.L.P: 119, Mwanza.

    Simu: 028-2501037

    Simu ya Mkononi: 028-2501037

    Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.