• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
Mwanza Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Mwanza

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia ya Mkoa
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti Mkoa
    • Seksheni
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Serikali za Mitaa
      • Afya
      • Elimu
      • Maji
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa Ndani
      • ununuzi na Ugavi
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Kitengo cha Sheria
  • Wilaya
    • Ilemela
    • Nyamagana
    • Magu
    • Misungwi
    • Kwimba
    • Sengerema
    • Ukerewe
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Jiji la Mwanza
    • Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
    • Hamashauri ya Wilaya ya Magu
    • Hamashauri ya Wilaya ya Sengerema
    • Hamashauri ya Wilaya ya Misungwi
    • Hamashauri ya Wilaya ya Kwimba
    • Hamashauri ya Wilaya ya Ukerewe
    • Hamashauri ya Wilaya ya Buchosa
  • Fursa za uwekezaji
    • Miundombinu ya Umwagiliaji na kilimo cha mkataba
    • Kilimo
    • Madini
    • Sekta ya Huduma
  • Huduma zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Watumishi
  • Machapisho
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa Kwa vyombo vya habari
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya video

Mwanafunzi aliyetekwa Mwanza akutwa Lamadi amejiteka

Posted on: April 30th, 2019


Taharuki  iliyokuwa imetanda Jiji la Mwanza juu ya mwanafunzi  wa kidato cha pili  Shule  ya  Mtakatifu Mary’s  Apostos, Yela Cosmas (17)  kutekwa na watu wasiojulika huku  wakiwataka wazazi wake kutuma fedha  haraka vinginevyo wangempeleka  nchini  Zambia amekamatwa na Jeshi la Polisi akiwa amejiteka.

Ujumbe wa kutekwa kwa mwanafunzi huyo ulianza kusambaa juzi kwenye mitandao ya kijamii  kupitia namba mpya ya simu  0689447247 ikiwa ni masaa machache baada ya wazazi wake kumsindikiza  na kumpandisha  basi la Sheraton kwenda shuleni.

Akizungumza na waandishi wa habari, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Jumanne Murilo alisema tukio hilo lilitokea juzi na  baada ya taarifa  hiyo kuwafikia  walianza kazi ya kufuatilia kwa   kutumia kikosi maalumu walifanikiwa kumpata  mwanafunzi huyo  Lamadi  mkoani Simiyu akiwa amejiteka lengo ni kupata fedha kutoka kwa wazazi wake.

“Mwanafunzi huyu  alisindikizwa na wazazi wake hadi kituo cha Buruzuga na kupandishwa basi la Sheraton linalofanya safari zake kati ya Mwanza-Geita lakini baadaye alishuka na kusajili namba mpya  ya simu  0689447247 ambayo wazazi wake hawaijui, ujumbe ule uliwataka wazazi  fedha bila kutaja kiasi ili mtoto aachiwe kwani ametekwa vinginevyo angepelekwa nchini Zambia.

“Jeshi la polisi lilifuatilia  tukio hilo kwa ukaribu kwa kutumia kikosi maalum na kumtia nguvuni mwanafunzi huyo  Lamadi mkoani Simiyu akiwa salama na tunamshikilia ili kufanya mahojiano na baadaye tutamfikisha mahakamani kwani kitendo alichokifanya ni kinyume na sheria za nchi, tunaomba wanafunzi wenye nia kama hiyo waache haraka sana,”alisema Murilo.

Wakati huo huo polisi inamshikilia  Lazaro Isaack (32) Mkazi wa Machinjioni mkoani Mwanza kwa kosa la  kughushi nyaraka mbalimbali za Serikali, wizi kwa njia ya mtandao, kutapeli watu kwa kisingizio cha kutopata ajira, kujifanya mtumishi wa Serikali.

Kamanda  Murilo alisema  mtuhumiwa huyo alikamatwa juzi akiwa na kitambulisho cha kazi kutoka Vodacom Cap View  Ltd  na baada ya kufanya upekuzi katika makazi yake alikutwa na nakala 34 za TIN  kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) za mikoa ya Mwanza, Pwani, Dar es Salaam, Dodoma, Geita, Kagera, Mtwara na Shinyanga.

Murilo alisema mtuhumiwa huyo alikutwa na vifaa vingi  zikiwamo fomu za Serikali ambazo ziliwafanya watu  wengi kuamini ni mtumishi wa Serikali na kuwatepeli kirahisi kwa kumpatia pesa ambapo polisi inaendelea kuchunguiza mtandao huo ili kuwabaini wanaoshirikiana katika mtandao huo.

Matangazo

  • Tangazo la kukutana na Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Mwanza kwa shida mbalimbali. January 08, 2025
  • TANGAZO LA NANENANE TAREHE 8.8.2025 January 08, 2025
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • UZALISHAJI ZAO LA PAMBA WAONGEZEKA- MSIGWA

    May 03, 2025
  • DARAJA LA KIGONGO-BUSISI KUANZA KUTUMIKA MUDA WOWOTE KUANZIA SASA.

    May 02, 2025
  • SERIKALI YAANIKA TAKWIMU ZA MAENDELEO YA UTUMISHI YALIYOPATIKANA MWANZA

    May 01, 2025
  • MAKUNDI MAWILI YA MWISHO YALIYOFANYA ZIARA HIFADHI NA JNHPP YAWASILISHA NENO LA SHUKRANI KWA RAS BALANDYA

    April 29, 2025
  • Angalia zote

Video zinazotembea

Siku 365 za Mhe.Rais Samia Suluhu Hassan Mwanza
video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Fomu ya Ugonjwa
  • FFARS User Guidelines
  • Miongozo ya mfumo wa bajeti na Mipango
  • Makusanyo ya Ndani ya Halmashauri za Mkoa wa Mwanza
  • PReM
  • Maswali Yaulizwayo Mara kwa Mara
  • Opras fomu
  • OFISI MTANDAO

Viunganishi Linganishi

  • Tovuti ya Ikulu
  • Utumishi
  • Tamisemi
  • Ofisi ya Taifa ya Takwimu Tanzania
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Kuu ya Serikali

Watembeleaji

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive

    S.L.P: 119, Mwanza.

    Simu: 028-2501037

    Simu ya Mkononi: 028-2501037

    Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.