• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
Mwanza Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Mwanza

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia ya Mkoa
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti Mkoa
    • Seksheni
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Serikali za Mitaa
      • Afya
      • Elimu
      • Maji
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa Ndani
      • ununuzi na Ugavi
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Kitengo cha Sheria
  • Wilaya
    • Ilemela
    • Nyamagana
    • Magu
    • Misungwi
    • Kwimba
    • Sengerema
    • Ukerewe
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Jiji la Mwanza
    • Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
    • Hamashauri ya Wilaya ya Magu
    • Hamashauri ya Wilaya ya Sengerema
    • Hamashauri ya Wilaya ya Misungwi
    • Hamashauri ya Wilaya ya Kwimba
    • Hamashauri ya Wilaya ya Ukerewe
    • Hamashauri ya Wilaya ya Buchosa
  • Fursa za uwekezaji
    • Miundombinu ya Umwagiliaji na kilimo cha mkataba
    • Kilimo
    • Madini
    • Sekta ya Huduma
  • Huduma zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Watumishi
  • Machapisho
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa Kwa vyombo vya habari
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya video

Mwanza kutoa kinga – Tiba Ugonjwa wa Kichocho, Minyoo ya Tumbo

Posted on: July 31st, 2018

 

Mikoa ya Mwanza na Mara inaongoza kwa kuwa na maambukizi ya ugonjwa wa kichocho na minyoo ya tumbo nchini kwa kuwa na juu ya asilimia 30.

Akiongea kwenye uzinduzi wa kampeni ya ugawaji dawa za kukinga na kutibu magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele katika Mkoa wa Mwanza Oscar Kaitaba Afisa Mpango wa magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele Kutoka Wizara ya Afya alisema Mikoa hiyo inamaambukizi makubwa kwa sababu wadudu wanaoeneza ugonjwa wanazaliana kwa wingi.

“Wananchi wa kanda ya ziwa ikiwemo Mwanza na Mara wanatabia ya kujisaidia pembezoni mwa ziwa, wanachota maji ya kutumia ziwani na sio tu kwa ajili ya wadudu kuzaliana sana lakini pia na zao la mpunga linachangia kuwepo kwa maambukizi ya magonjwa haya”alisema Kaitaba.

Naye Mratibu wa magojwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele Mkoa wa Mwanza, Mabai Thobias alisema, walengwa ni  watoto wenye umri wa kuanzia miaka mitano hadi kumi na nne ambao wapo mashuleni ambapo kwa mkoa wa mwanza ni zaidi ya watoto 878,624 kwenye shule 663  za mkoa wa huo.

“Walengwa wetu ni watu  627,917 katika kata 41 za Halmashauri za Ukelewe, magu, Ilemela, Buchosa na Mwanza mjini ambao tutawatembelea kaya moja baada ya nyingine ili kukamilisha ugawaji dawa baada ya kugawa kwa wanafunzi mashuleni”alisema Thobias

Akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. John Mongella, Mkuu wa Wilaya ya Sengerema Mhe. Emmanuel Kipole alisema, kwa mujibu ya tathimini ya awali kupitia Taasisi ya Utafiti wa magonjwa ya binadamu, NIMR kituo cha Mwanza, kwa kushirikiana na Mradi wa udhibiti endelevu wa kudhibiti kichocho katika jiji la Mwanza wa mwaka 2018 katika Halmashauri za Ilemela na Nyamagana, kati ya watu 2,148 wenye umri wa miaka 15 na Zaidi waliofanyiwa uchunguzi 1,748 sawa na 81,4% walikutwa na maambukizi ya kichocho.

“Kutokana na kiwango hicho cha maambukizi na kwamujibu wa tafiti na maelekezo ya kitaalamu ya Shirika la Afya Duniani (WHO) jamii inapaswa ipewe dawa ya kukinga na kutibu hivyo, Mkoa unawajulisha wananchi na wakazi wote kuwa tarehe 6 agosti mwaka huu tutaendesha kampeni za ugawaji dawa wa kukinga na kutibu magonjwa ya minyoo ya tumbo na kichocho  kwa umri wa kwenda shule, waliopo na wasiokuwepo shuleni,” alisema Kipole.


Mhe Kipole aliongeza kuwa, dawa hizo zinatakiwa mtoto awe amekula chakula ndani ya masaa yasiyozidi mawili na baada ya kula ndo apatiwe dawa hizo na kuwa chakula kiandaliwe shuleni siku hiyo ya kumeza dawa.

Matangazo

  • Tangazo la kukutana na Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Mwanza kwa shida mbalimbali. January 08, 2025
  • TANGAZO LA NANENANE TAREHE 8.8.2025 January 08, 2025
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • MWANZA, SIMIYU ZANG'ARA UTAMILIFU DARASA LA SABA KANDA YA ZIWA

    May 30, 2025
  • RAS MWANZA AZINDUA RASMI MRADI WA KUPAMBANA NA UGONJWA WA SELI MUNDU

    May 30, 2025
  • WAANDISHI WA HABARI MWANZA WAPIGWA MSASA MIKAKATI YA KUTOKOMEZA WATOTO WA MITAANI

    May 29, 2025
  • RAS MWANZA AWATAKA VIONGOZI WA UMMA KUDUMISHA NIDHAMU NA UFANISI KAZINI

    May 26, 2025
  • Angalia zote

Video zinazotembea

Siku 365 za Mhe.Rais Samia Suluhu Hassan Mwanza
video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Fomu ya Ugonjwa
  • FFARS User Guidelines
  • Miongozo ya mfumo wa bajeti na Mipango
  • Makusanyo ya Ndani ya Halmashauri za Mkoa wa Mwanza
  • PReM
  • Maswali Yaulizwayo Mara kwa Mara
  • Opras fomu
  • OFISI MTANDAO

Viunganishi Linganishi

  • Tovuti ya Ikulu
  • Utumishi
  • Tamisemi
  • Ofisi ya Taifa ya Takwimu Tanzania
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Kuu ya Serikali

Watembeleaji

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive

    S.L.P: 119, Mwanza.

    Simu: 028-2501037

    Simu ya Mkononi: 028-2501037

    Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.