• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
Mwanza Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Mwanza

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia ya Mkoa
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti Mkoa
    • Seksheni
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Serikali za Mitaa
      • Afya
      • Elimu
      • Maji
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa Ndani
      • ununuzi na Ugavi
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Kitengo cha Sheria
  • Wilaya
    • Ilemela
    • Nyamagana
    • Magu
    • Misungwi
    • Kwimba
    • Sengerema
    • Ukerewe
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Jiji la Mwanza
    • Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
    • Hamashauri ya Wilaya ya Magu
    • Hamashauri ya Wilaya ya Sengerema
    • Hamashauri ya Wilaya ya Misungwi
    • Hamashauri ya Wilaya ya Kwimba
    • Hamashauri ya Wilaya ya Ukerewe
    • Hamashauri ya Wilaya ya Buchosa
  • Fursa za uwekezaji
    • Miundombinu ya Umwagiliaji na kilimo cha mkataba
    • Kilimo
    • Madini
    • Sekta ya Huduma
  • Huduma zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Watumishi
  • Machapisho
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa Kwa vyombo vya habari
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya video

Mwanza Yaanzisha safari ya vyakula kwenda Ulaya

Posted on: May 12th, 2020

Usafirishaji wa mizigo kwenda ulaya wazinduliwa kwa tani 8 za minofu ya samaki kusafirishwa kwenda Brusels nchini Ubelgiji kwa kutumia ndege ya Rwada  A330-300 yenye usajiri 9xR-WP.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa ndenge hiyo Waziri wa Ujenzi ,Uchukuzi na Mawasiliano ,Eng Isack Kamwelwe amesema kuna umuhimu wa kuwa na ndege ya ubebaji mzigo kutoka Mwanza kwenda Ulaya kwa kuwa Mwanza wanauwezo wa kuzalisha tani 200 za samaki kwa siku hivyo zoezi hilo limeanza rasmi leo na wiki ijayo ndege itarejea nchini.

" Miaka miwili iliyopita Rais wa Tanzania na Rwanda walikutana na kuzungumzia miradi mbalimbali na wakaona kuna umuhimu wa kuwa na ndege ya ubebaji mzigo kutoka uwanja huu kwenda Ulaya,juhudi za kutafuta ndege za mizigo ili kutimiza maagizo ya Rais wetu yametimia "anasema Kamwelwe

Ameongeza kuwa unapozalisha na kuuza nje, soko linapanuka na uchumi wa nchi kukuwa hivyo wameanza na vyakula baadaye matunda .


Naye Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Abdallah Ulega amesema kitendo cha kusafirisha minofu ya samaki na nyama kwenda masoko ya nje kupitia kiwanja cha Mwanza zitapunguza gharama za usafirishaji ,chakula kuwa fresh usafirishaji unapokuwa wa moja kwa moja ubora wa chakula unakuwa mkubwa tofauti na kusafirisha na kutatisha safari hadi siku nyingine kama ilivyokuwa awali hayo ni mambo muhimu ya  kujivunia.

Aidha Mkuu wa mkoa wa Mwanza John Mongella amesema kiuchumi Mwanza ndio eneo la kati na kuwa chachu ya  kukuza uchumi hivyo wananchi wawajibike na kufanya kazi na kuongeza nguvu katika uzalishaji, kuchangamkia fursa iliyojitokeza kwa kuwa mzunguko wa fedha utakuwa mkubwa sambamba na upatikanaji wa ajila utaongezeka.


"Mara ya mwisho ndege kubeba samaki ni 2008 leo tena tumeamka ni mapinduzi makubwa yameletwa na serikali ya awamu hii hivyo wawekezaji wachangamkie Mwanza ni mahali salama pakuwekeza biashara zao "anasema Mongella.


Kwa upande wake Meja Gen Charles Karamba Balozi wa Rwanda anasema leo ni siku muhimu baada ya kuyatekeleza maagizo ya Marais wawili hivyo wajibu wao ni kufanya kazi ili kuimarisha mawasiliano baina ya Tanzania na Rwanda .


"Ndio tumeanza kazi bado..lazima tufanye kazi kwa pamoja bidhaa iliyopo Tanzinia ni nyingi kutoka kwa wavuvi na wafugaji wajibu wetu ni kuifurahia hii kazi na kutaifanya ili kuleta tija na kukuza uchumi"anasema Karamba.

Katibu Mkuu Uchukuzi Dr.Leonard Chamuriho anasema wafanyabiashara watafute masoko ya nje kwa sababu vikwazo vyote vya kiufundi,mahitaji ya kukidhi viwango vya uhifadhi wa chakula na viwango vya usalama vyote vimekamilika  hivyo wachangamkie fursa hiyo muhimu.

Aidha Meneja Rasilimali watu kutoka Tanzania Fish Processors Ltd Godfrey Samwel anasema mzigo pamoja na usafirishaji gharama zake ni USD 32000, mwanzo walikuwa wanasafirisha mzigo kupitia nchi jirani ya Kenya na walikuwa wakitumia gharama kubwa na muda mrefu hivyo kuwepo kwa usafiri huo kutawasaidia kwenda na wakati sambamba na kupunguza gharama.

"Tunaiomba serikali ijaribu kutafuta mashirika mengine ili tuweze kusafirisha nchi mbalimbali " anasema

Pascal Kalumbeta ni meneja wa uwanja wa ndege Mwanza anasema serikali imefanya uwekezaji mkubwa pamoja na kujenga jengo la mzigo la kisasa ambapo Mwanza kuna mazao ya samaki mengi hivyo ni wakati wa kuvutia wawekezaji na kutengeneza soko la kimataifa .

Matangazo

  • Tangazo la kukutana na Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Mwanza kwa shida mbalimbali. January 08, 2025
  • TANGAZO LA NANENANE TAREHE 8.8.2025 January 08, 2025
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • UZALISHAJI ZAO LA PAMBA WAONGEZEKA- MSIGWA

    May 03, 2025
  • DARAJA LA KIGONGO-BUSISI KUANZA KUTUMIKA MUDA WOWOTE KUANZIA SASA.

    May 02, 2025
  • SERIKALI YAANIKA TAKWIMU ZA MAENDELEO YA UTUMISHI YALIYOPATIKANA MWANZA

    May 01, 2025
  • MAKUNDI MAWILI YA MWISHO YALIYOFANYA ZIARA HIFADHI NA JNHPP YAWASILISHA NENO LA SHUKRANI KWA RAS BALANDYA

    April 29, 2025
  • Angalia zote

Video zinazotembea

Siku 365 za Mhe.Rais Samia Suluhu Hassan Mwanza
video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Fomu ya Ugonjwa
  • FFARS User Guidelines
  • Miongozo ya mfumo wa bajeti na Mipango
  • Makusanyo ya Ndani ya Halmashauri za Mkoa wa Mwanza
  • PReM
  • Maswali Yaulizwayo Mara kwa Mara
  • Opras fomu
  • OFISI MTANDAO

Viunganishi Linganishi

  • Tovuti ya Ikulu
  • Utumishi
  • Tamisemi
  • Ofisi ya Taifa ya Takwimu Tanzania
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Kuu ya Serikali

Watembeleaji

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive

    S.L.P: 119, Mwanza.

    Simu: 028-2501037

    Simu ya Mkononi: 028-2501037

    Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.