• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
Mwanza Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Prime Minister's Office Regional Administration and Local Government Mkoa wa Mwanza

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia ya Mkoa
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti Mkoa
    • Seksheni
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Serikali za Mitaa
      • Afya
      • Elimu
      • Maji
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa Ndani
      • ununuzi na Ugavi
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Kitengo cha Sheria
  • Wilaya
    • Ilemela
    • Nyamagana
    • Magu
    • Misungwi
    • Kwimba
    • Sengerema
    • Ukerewe
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Jiji la Mwanza
    • Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
    • Hamashauri ya Wilaya ya Magu
    • Hamashauri ya Wilaya ya Sengerema
    • Hamashauri ya Wilaya ya Misungwi
    • Hamashauri ya Wilaya ya Kwimba
    • Hamashauri ya Wilaya ya Ukerewe
    • Hamashauri ya Wilaya ya Buchosa
  • Fursa za uwekezaji
    • Miundombinu ya Umwagiliaji na kilimo cha mkataba
    • Kilimo
    • Madini
    • Sekta ya Huduma
  • Huduma zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Watumishi
  • Machapisho
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa Kwa vyombo vya habari
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya video

MWANZA YAIPONGEZA SERIKALI MABORESHO YA HUDUMA ZA SARATANI KWA WATOTO

Posted on: February 15th, 2026

Serikali ya Mkoa wa Mwanza imemshukuru Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa uwekezaji alioufanya katika sekta ya afya hususani kitengo cha saratani katika hospitali ya rufaa ya kanda Bugando.

Hayo yamebainishwa na Mkuu wa Wilaya ya Ilemela Mhe. Amir Mkalipa kwaniaba ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza katika maadhimisho ya siku ya saratani kwa watoto duniani ambayo iliambatana na mchezo wa kirafiki wa mpira wa miguu kati ya timu RC na timu RMO.

Mhe. Mkalipa amesema Mhe. Rais ameimarisha matibabu ya saratani kwa kununua mashine kubwa kwa ajili ya mionzi, kupeleka wataalamu kusomea ubingwa na ubingwa bobezi juu ya maswala ya saratani lakini pia amejenga wodi kwa wagonjwa wa saratani na ametenga fedha kwa ajili ya dawa na vifaa tiba kwa ujumla pamoja na kuajiri watumishi wapya katika sekta ya afya.

Aidha, amewashukuru wadau wote ambao amekua kipaumbele katika kutoa misaada katika matibabu ya watoto ikiwemo bima na vifaa mbali mbali huku akiiomba jamii iendelee kuchangia katika jitihada za serikali katika matibabu ya watu wenye saratani.

Naye Mganga Mkuu Mkoa wa Mwanza Dkt. Jesca Lebba amewasisitiza wananchi kuwa na tabia ya kuangalia afya za watoto kwakua saratani nyingi za watoto hazijulikani chanzo chake lakini inapogundulika mapema inatibika na gharama zake zinakua ni nafuu.

Ameongeza kwa kuwataka wananchi kubadili mfumo wa maisha na kujenga desturi ya kufanya mazoezi, kula mlo ulio kamili, kupata chanjo ambazo zitawasaidia katika kujikinga na ugonjwa wa saratani pamoja na kupunguza matumizi ya kemikali, mionzi na vitu vingine vyote kama pombe, sigara na tumbaku ambavyo vinaweza kupelekea mtu kupata saratani.

Sambamba na hayo, Dkt. Lebba amesisitiza juu ya umuhimu wa bima ya afya kwa wote kwakuwa inarahisisha matibabu na inamfanya mwananchi apate huduma kwa uharaka na gharama nafuu zaidi.

Hata hivyo mchezo huo wa kirafiki uliochezwa katika uwanja wa Nyamagana umetamatika kwa timu RC kuibuka na ushindi wa bao 2 kwa 1 dhidi ya timu RMO.Veternas wa mwanza wamechangia vitu mbalimbali kwa ajili ya watoto wenye saratani.

Matangazo

  • Tangazo la kukutana na Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Mwanza kwa shida mbalimbali. January 08, 2025
  • TANGAZO LA NANENANE TAREHE 8.8.2025 January 08, 2025
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • MKURUGENZI IDARA YA MAAFA OWM AFUNGA MAFUNZO YA KUKABILIANA NA DHARULA MWANZA

    February 20, 2026
  • KAYA 19,344 KUNUFAIKA NA BIMA YA AFYA KWA WOTE MWANZA AWAMU YA KWANZA

    February 20, 2026
  • RC MTANDA AMPOKEA WAZIRI DEUS SANGU MWANZA

    February 20, 2026
  • RC MTANDA AWATAKA WASIMBE NA WABANZA KUUNGANA KUKATA BIMA YA AFYA KWA WOTE

    February 20, 2026
  • Angalia zote

Video zinazotembea

Siku 365 za Mhe.Rais Samia Suluhu Hassan Mwanza
video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Fomu ya Ugonjwa
  • FFARS User Guidelines
  • Miongozo ya mfumo wa bajeti na Mipango
  • Makusanyo ya Ndani ya Halmashauri za Mkoa wa Mwanza
  • PReM
  • Maswali Yaulizwayo Mara kwa Mara
  • Opras fomu
  • OFISI MTANDAO

Viunganishi Linganishi

  • Tovuti ya Ikulu
  • Utumishi
  • Tamisemi
  • Ofisi ya Taifa ya Takwimu Tanzania
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Kuu ya Serikali

Watembeleaji

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive

    S.L.P: 119, Mwanza.

    Simu: 028-2501037

    Simu ya Mkononi: 028-2501037

    Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.