• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
Mwanza Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Mwanza

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia ya Mkoa
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti Mkoa
    • Seksheni
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Serikali za Mitaa
      • Afya
      • Elimu
      • Maji
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa Ndani
      • ununuzi na Ugavi
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Kitengo cha Sheria
  • Wilaya
    • Ilemela
    • Nyamagana
    • Magu
    • Misungwi
    • Kwimba
    • Sengerema
    • Ukerewe
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Jiji la Mwanza
    • Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
    • Hamashauri ya Wilaya ya Magu
    • Hamashauri ya Wilaya ya Sengerema
    • Hamashauri ya Wilaya ya Misungwi
    • Hamashauri ya Wilaya ya Kwimba
    • Hamashauri ya Wilaya ya Ukerewe
    • Hamashauri ya Wilaya ya Buchosa
  • Fursa za uwekezaji
    • Miundombinu ya Umwagiliaji na kilimo cha mkataba
    • Kilimo
    • Madini
    • Sekta ya Huduma
  • Huduma zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Watumishi
  • Machapisho
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa Kwa vyombo vya habari
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya video

Mwanza Yatekeleza agizo la Rais kwa vitendo

Posted on: October 11th, 2019

Mwanza Yatekeleza agizo la Rais Mhe.Dkt.John Pombe Magufuli kwa Vitendo


Serikali Mkoani Mwanza imeanza kutekeleza agizo la Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt.John Pombe Joseph Magufuli la kujenga jengo la abiria katika uwanja wa ndege Mkoani humo litakaloghalimu zaidi ya shilingi bilioni nne na lenye uwezo wa kuchukua abiria mia sita kwa wakati mmoja wanaoshuka kwenye ndege au wanaosubiri kusafiri.

Akikagua ujenzi wa jengo hilo katika uwanja wa ndege  Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe.John Mongella amesema ujenzi wa jengo hilo la kisasa lenye uwezo wa kuchukua abiria 600 unatarajiwa kukamilika ndani ya miezi 6.

"Kama mtakumbuka Mhe.Rais alipokuwa Mwanza kwa Ziara alielekeza tujenge jengo la abiria na sisi mara moja tukaanza utekelezaji wa jengo hilo kwa kuanza kazi ya kupata mchoro na sasa hivi ujenzi umeanza tupo kwenye msingi na jengo ni la kisasa na nila kudumu na kazi inaendelea vizuri,"alisema Mongella.

Kwa upande wake mbunifu majengo  kutoka Ofisi Ya Katibu Tawala Mkoa Wa Mwanza Chagu Mghoma amesema Ujenzi wa Jengo hilo unaendelea vizuri huku wakiwa na  wafanyakazi  wa kutosha na  vifaa vya kutosha Ili Kuhakikisha ujenzi huo unakamilika  ndani ya muda uliopangwa.

" Kazi inaendelea kama mliivyoona kila siku lazima tujiwekee malengo na lazima tuyatekeleze tuliagigwa tutekeleze kwa wakati nasi tunafuata maagizo na kazi inaendelea,"alisema Mghoma.

Naye Mtunza stoo Kopro Stephania  Nasibu  ameongeza kuwa wapo vizuri kuhakikisha kuwa kila kitu kinachongia na kutoka kipo katika usalama wa hali ya juu,ulinzi umeimalishwa vya kutosha.

Kwa upande wake Katibu Tawala Wa Mkoa huo Christopher Kadio amesema kukamilika kwa Jengo hilo la abiria kutasaidia kukabiliana na changamoto kubwa ya ongezeko la abiria wanaotumia usafiri wa ndege Mkoani humo.

"Ni matarajio yetu kwamba uwanja huu utakapokamilika utapunguza adha ya abiria wanayoipata pindi wanaposafiri kwani tuna taarifa kuwa uwanja huu unapokea ndege 5 zinazoenda mataifa mbalimbali kwa siku hili ni ongezeko kubwa sana," alisema Kadio.














Matangazo

  • Tangazo la kukutana na Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Mwanza kwa shida mbalimbali. January 08, 2025
  • TANGAZO LA NANENANE TAREHE 8.8.2025 January 08, 2025
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • UZALISHAJI ZAO LA PAMBA WAONGEZEKA- MSIGWA

    May 03, 2025
  • DARAJA LA KIGONGO-BUSISI KUANZA KUTUMIKA MUDA WOWOTE KUANZIA SASA.

    May 02, 2025
  • SERIKALI YAANIKA TAKWIMU ZA MAENDELEO YA UTUMISHI YALIYOPATIKANA MWANZA

    May 01, 2025
  • MAKUNDI MAWILI YA MWISHO YALIYOFANYA ZIARA HIFADHI NA JNHPP YAWASILISHA NENO LA SHUKRANI KWA RAS BALANDYA

    April 29, 2025
  • Angalia zote

Video zinazotembea

Siku 365 za Mhe.Rais Samia Suluhu Hassan Mwanza
video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Fomu ya Ugonjwa
  • FFARS User Guidelines
  • Miongozo ya mfumo wa bajeti na Mipango
  • Makusanyo ya Ndani ya Halmashauri za Mkoa wa Mwanza
  • PReM
  • Maswali Yaulizwayo Mara kwa Mara
  • Opras fomu
  • OFISI MTANDAO

Viunganishi Linganishi

  • Tovuti ya Ikulu
  • Utumishi
  • Tamisemi
  • Ofisi ya Taifa ya Takwimu Tanzania
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Kuu ya Serikali

Watembeleaji

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive

    S.L.P: 119, Mwanza.

    Simu: 028-2501037

    Simu ya Mkononi: 028-2501037

    Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.