• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
Mwanza Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Mwanza

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia ya Mkoa
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti Mkoa
    • Seksheni
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Serikali za Mitaa
      • Afya
      • Elimu
      • Maji
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa Ndani
      • ununuzi na Ugavi
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Kitengo cha Sheria
  • Wilaya
    • Ilemela
    • Nyamagana
    • Magu
    • Misungwi
    • Kwimba
    • Sengerema
    • Ukerewe
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Jiji la Mwanza
    • Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
    • Hamashauri ya Wilaya ya Magu
    • Hamashauri ya Wilaya ya Sengerema
    • Hamashauri ya Wilaya ya Misungwi
    • Hamashauri ya Wilaya ya Kwimba
    • Hamashauri ya Wilaya ya Ukerewe
    • Hamashauri ya Wilaya ya Buchosa
  • Fursa za uwekezaji
    • Miundombinu ya Umwagiliaji na kilimo cha mkataba
    • Kilimo
    • Madini
    • Sekta ya Huduma
  • Huduma zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Watumishi
  • Machapisho
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa Kwa vyombo vya habari
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya video

Mwanza Yawatunuku wachangiaji damu

Posted on: September 4th, 2019

Wadau na Wataalamu wa afya wametakiwa kuweka mkakati wa kuelimisha na kuhamasisha jamii kuchangia damu ili kusaidia kuokoa maisha ya watu.

Rai hiyo ilitolewa  na Katibu Tawala wa Mkoa wa Mwanza, Christopher Kadio, wakati akiwakabidhi vyeti wadau waliofanikisha uchangiaji damu kwenye maadhimisho ya siku ya damu yaliyofanyika mkoani Mwanza kitaifa , Juni mwaka huu.

Alisema ili kuokoa maisha ya wananchi wenye uhitaji wa damu wadau na wataalamu wa afya waweke mkakati endelevu wa kutoa elimu kwa jamii na kuhamasisha uchangiaji damu.

“Wataalamu wa afya mnatakiwa kulifanya zoezi la uchangiaji damu kuwa endelevu na hivyo mtafute jukwaa la kuelimisha jamii ili tufike mahali ijenge utamaduni wa kuchangia damu kwa hiari na kuweza kutatua changamoto hiyo,”alisema Kadio.

Pia alishauri kutokana na hospitali nyingi kumilikiwa na taasisi za dini ni vyema viongozi wa madhehebu ya dini wakawahamasisha waumini wao kuona umuhimu wa kutoa damu kwa maslahi ya jamii.

Awali Mkuu wa Huduma Maabara Mkoa wa Mwanza, Julius Shigela alisema wadau hao wametunukiwa vyeti hivyo ili kutambua na kuthamini mchango wao kutokana na mafanikio ya ukusanyaji na uchangaji damu.

Alisema Mkoa wa Mwanza katika maadhimisho ya damu duniani yaliyofanyika jijini humu Juni mwaka huu, ulifanikiwa kukusanya unit (chupa) 10,669 na kuvuka lengo la wizara kwa asilimia 203, kwa mkoa wakivuka kwa asilimia 101 la kukusanya chupa 4000.

Miongoni mwa wadau waliotunukiwa vyeti kwa niaba ya wengine  zaidi ya 30 ni pamoja na The Desk & Chair Foundation,halmashauri za Jiji la Mwanza na Manispaa ya Ilemela, Isamilo Lodge,Aga Khan Foundation, hospitali za Pasiansi SDA,Hindu na CF.

Matangazo

  • Tangazo la kukutana na Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Mwanza kwa shida mbalimbali. January 08, 2025
  • TANGAZO LA NANENANE TAREHE 8.8.2025 January 08, 2025
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • UZALISHAJI ZAO LA PAMBA WAONGEZEKA- MSIGWA

    May 03, 2025
  • DARAJA LA KIGONGO-BUSISI KUANZA KUTUMIKA MUDA WOWOTE KUANZIA SASA.

    May 02, 2025
  • SERIKALI YAANIKA TAKWIMU ZA MAENDELEO YA UTUMISHI YALIYOPATIKANA MWANZA

    May 01, 2025
  • MAKUNDI MAWILI YA MWISHO YALIYOFANYA ZIARA HIFADHI NA JNHPP YAWASILISHA NENO LA SHUKRANI KWA RAS BALANDYA

    April 29, 2025
  • Angalia zote

Video zinazotembea

Siku 365 za Mhe.Rais Samia Suluhu Hassan Mwanza
video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Fomu ya Ugonjwa
  • FFARS User Guidelines
  • Miongozo ya mfumo wa bajeti na Mipango
  • Makusanyo ya Ndani ya Halmashauri za Mkoa wa Mwanza
  • PReM
  • Maswali Yaulizwayo Mara kwa Mara
  • Opras fomu
  • OFISI MTANDAO

Viunganishi Linganishi

  • Tovuti ya Ikulu
  • Utumishi
  • Tamisemi
  • Ofisi ya Taifa ya Takwimu Tanzania
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Kuu ya Serikali

Watembeleaji

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive

    S.L.P: 119, Mwanza.

    Simu: 028-2501037

    Simu ya Mkononi: 028-2501037

    Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.