• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
Mwanza Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Mwanza

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia ya Mkoa
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti Mkoa
    • Seksheni
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Serikali za Mitaa
      • Afya
      • Elimu
      • Maji
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa Ndani
      • ununuzi na Ugavi
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Kitengo cha Sheria
  • Wilaya
    • Ilemela
    • Nyamagana
    • Magu
    • Misungwi
    • Kwimba
    • Sengerema
    • Ukerewe
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Jiji la Mwanza
    • Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
    • Hamashauri ya Wilaya ya Magu
    • Hamashauri ya Wilaya ya Sengerema
    • Hamashauri ya Wilaya ya Misungwi
    • Hamashauri ya Wilaya ya Kwimba
    • Hamashauri ya Wilaya ya Ukerewe
    • Hamashauri ya Wilaya ya Buchosa
  • Fursa za uwekezaji
    • Miundombinu ya Umwagiliaji na kilimo cha mkataba
    • Kilimo
    • Madini
    • Sekta ya Huduma
  • Huduma zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Watumishi
  • Machapisho
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa Kwa vyombo vya habari
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya video

MWANZA YAZINDUA UTOAJI ELIMU YA BIMA YA AFYA KWA WOTE

Posted on: December 17th, 2025

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mhe. Said Mtanda, leo Desemba 17, 2025 amezindua utoaji wa elimu ya Bima ya Afya kwa Wote mkoani Mwanza, akihimiza wananchi kushiriki ili kuhakikisha kila mmoja anakuwa na uhakika wa kupata huduma za matibabu.

Mhe. Mtanda amesema bima ya afya huwezesha wale wachache wanaougua kupata matibabu kwa urahisi, kwani si wote wanaochangia huugua kwa wakati mmoja.

Amewataka viongozi na wataalamu kuwa mabalozi wazuri wa kuhamasisha wananchi, akisisitiza kuwa bima ya afya ni jambo la msingi lenye faida kubwa kwa jamii.

Aidha, amewaelekeza Wakurugenzi wa Halmashauri za Mkoa huo kuhakikisha wataalamu wanapatiwa elimu na semina za kutosha ili kuongeza uelewa kuanzia ngazi ya juu hadi jamii.

Pia amewataka watoa huduma za afya kuboresha huduma kwa wateja ili wananchi waone fahari ya mfumo huo, akisisitiza uwajibikaji na uongozi bora katika utoaji wa huduma.

Katika hotuba yake, Mkuu wa Mkoa amebainisha mafanikio ya Serikali ya Awamu ya Sita katika sekta ya afya mkoani humo, akisisitiza kuwa maendeleo hayo hayatakuwa na maana iwapo wananchi hawatapata huduma, ndiyo maana matumizi ya bima ya afya yanahamasishwa.

Kwa upande wake, Dkt. Carolyne Damiani Mkurugenzi Msaidizi Uratibu Bima ya Afya kutoka wizara ya Afya ameeleza dhana ya bima ya afya ikijumuisha malipo kabla ya huduma, uchangiaji wa pamoja, kuchangiana kati ya wenye uwezo na wasio na uwezo, usawa katika mchango na huduma, upatikanaji wa huduma bora kwa wakati, pamoja na uwajibikaji wa pamoja kati ya Serikali, skimu za bima, vituo vya afya na wananchi.

Matangazo

  • Tangazo la kukutana na Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Mwanza kwa shida mbalimbali. January 08, 2025
  • TANGAZO LA NANENANE TAREHE 8.8.2025 January 08, 2025
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • RC MTANDA ATUMA SALAMU ZA KRISMASI NA MWAKA MPYA KWA WANA-MWANZA

    December 23, 2025
  • RC MTANDA AKUTANA NA NAIBU WAZIRI MAHUNDI

    December 23, 2025
  • RC MTANDA AZINDUA UGAWAJI BODABODA 100 KWA VIJANA WA ILEMELA

    December 22, 2025
  • WAHITIMU AFYA WAASWA KUTUMIA ELIMU KUCHOCHEA MABADILIKO YA JAMII

    December 21, 2025
  • Angalia zote

Video zinazotembea

Siku 365 za Mhe.Rais Samia Suluhu Hassan Mwanza
video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Fomu ya Ugonjwa
  • FFARS User Guidelines
  • Miongozo ya mfumo wa bajeti na Mipango
  • Makusanyo ya Ndani ya Halmashauri za Mkoa wa Mwanza
  • PReM
  • Maswali Yaulizwayo Mara kwa Mara
  • Opras fomu
  • OFISI MTANDAO

Viunganishi Linganishi

  • Tovuti ya Ikulu
  • Utumishi
  • Tamisemi
  • Ofisi ya Taifa ya Takwimu Tanzania
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Kuu ya Serikali

Watembeleaji

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive

    S.L.P: 119, Mwanza.

    Simu: 028-2501037

    Simu ya Mkononi: 028-2501037

    Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.