Katibu Tawala Mkoa wa Mwanza Ndugu Balandya Elikana leo tarehe 16 Februari, 2026 amefungua Mafunzo kwa timu ya kukabiliana na dharula Mkoani humo ambapo ameishukuru Ofisi ya Waziri Mkuu kwa kushirikiana na Shirika la UNDP kwa kuichagua Mwanza kuwa mkoa wa kwanza kupewa mafunzo.

Aidha, amewataka wajumbe wa timu ya maafa ya Mkoa kuhakikisha wanapokea maelekezo vizuri ili kupata uelewa wa kutosha na wakasaidie kupunguza majanga ya Asili na yanayosababishwa na binadamu kutokana na uwezo wanaojengewa.

Bi. Winifrida Ngowi kutoka Idara ya Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu amesema ofisi ya Waziri Mkuu inaendelea kuratibu masuala ya maafa nchini na kwa sasa wapo Mwanza kwa ajili ya kuanzisha kituo cha Operesheni na Mawasiliano ya Dharula ngazi za Mikoa.

Pamoja na lengo hilo pia Ofisi ya Waziri Mkuu imejipanga kuhakikisha inaendelea kujenga jamii stahimilivu dhidi ya majanga na kuhakikisha vituo hivyo vinakuwa na wataalamu pamoja na vifaa vya dharula na kuwapatia mafunzo watenda kazi.

Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.