• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
Mwanza Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Mwanza

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia ya Mkoa
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti Mkoa
    • Seksheni
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Serikali za Mitaa
      • Afya
      • Elimu
      • Maji
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa Ndani
      • ununuzi na Ugavi
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Kitengo cha Sheria
  • Wilaya
    • Ilemela
    • Nyamagana
    • Magu
    • Misungwi
    • Kwimba
    • Sengerema
    • Ukerewe
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Jiji la Mwanza
    • Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
    • Hamashauri ya Wilaya ya Magu
    • Hamashauri ya Wilaya ya Sengerema
    • Hamashauri ya Wilaya ya Misungwi
    • Hamashauri ya Wilaya ya Kwimba
    • Hamashauri ya Wilaya ya Ukerewe
    • Hamashauri ya Wilaya ya Buchosa
  • Fursa za uwekezaji
    • Miundombinu ya Umwagiliaji na kilimo cha mkataba
    • Kilimo
    • Madini
    • Sekta ya Huduma
  • Huduma zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Watumishi
  • Machapisho
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa Kwa vyombo vya habari
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya video

"Pikipiki ya Afisa Tarafa ipo kijiweni inasanya ni marufuku"- Mongella

Posted on: April 6th, 2020


Rais  Dkt .John Magufuli ametimiza ahadi yake aliyoitoa mwezi juni mwaka jana ya kuwapa pikipiki maofisa tarafa nchini ambapo pikipiki 24 aina ya Sanlg zimekabidhiwa kwa maafisa tarafa wa Mkoa wa Mwanza kwa lengo la kurahisisha utendaji kazi kwa maafisa tarafa hao.

Akikabidhi pikipiki hizo kwa niaba ya Mhe. Rais Magufuli Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. John Mongella aliwataka maafisa tarafa hao kuzitumia pikipiki hizo kwa shughuli za Serikali  zilizokusudiwa na kuzingatia maadili ya kazi katika maeneo yao ili kuleta maendeleo kwa wananchi .

“ Rais amewaamini Maofisa Tarafa akaamua kuwapa nyenzo hizo ambazo ni mali ya Serikali kwa ajili ya kuondoa kilio cha usafiri,hivyo mzitunze kama mnavyotunza ofisi na nyaraka nyingine,sijawai kusikia sifa mbaya kwa Maofisa hawa wa Mkoa wangu,sitegemei baada ya kupatiwa chombo hiki cha usafiri ndiyo hadithi zianze nachotarajia pikipiki hizi zitumike kwa matumizi yaliyolengwa ya kusimamia ulinzi na usalama wa wananchi kwa kutunza watu na mali zao,kuhamasisha maendeleo na kusimamia maendeleo ndiyo kazi yenu kubwa.”alisema Mhe. Mongella.

Aidha Mhe. Mongella ameongeza kuwa usafiri huo utawafanya wafike kila eneo kwa urahisi zaidi na kuchochea kasi ya maendeleo.

"Nategemea  nikifika kwenye tarafa nikute amsha amsha ya maendeleo,kwa sababu mtakuwa hamjachoka mkitoka eneo moja kwenda vijiji vitatu vinne mnakagua kisha mnarudi baada ya hapo mnaenda tena vijiji vingine ambapo mnapaswa kuwa na mpangilio mzuri wa kazi,hivyo mwaka huu kuna kazi nyingi za maendeleo mhakikishe mnazifanya na uchaguzi mkuu unakuja mtimize wajibu wanu, alisisitiza."

 Hata hivyo pamoja na msisitizo mkubwa Mhe. Mongella  alioutoa,alifafanua  kuwa maofisa hao ni kiungo kikubwa katika maendeleo kwani wapo katika kazi zote(all functions) ambapo kwenye kazi za maendeleo na  ulinzi, usalama wa maendeleo pia,ukienda kwenye Wilaya mtu anayefanya kazi katika ofisi zote mbili za Mkurugenzi na Mkuu wa Wilaya ni Maafisa Tarafa vyo ni tegemeo kubwa katika Shughuli za kila siku.

"Rais ameisha toa pikipiki,tusimuangushe ametutendea jambo jema,kwahiyo mimi nawaachia nyiye nendeni mkafanye kazi kwa kushirikiana,msianze kufanyia ujasiriamali na hizi pikipiki lisije likatokea hilo tukio,kwamba sasa unakuta mwanadada,Afisa Tarafa hawezi kuendesha katafuta kijana, pikipiki ya Afisa Tarafa ipo kijiweni inasanya ni marufuku tafadhali sana zitumike kwa malengo yaliyo pangwa, nategemea kwa nyenzo hizi ufanisi utakuwa maradufu,"alisema Mongella.

Kwa upande wake Katibu Tawala wa Mkoa huo  Emmanuel Tutuba, akitoa mchanganuo wa namna pikipiki hizo zitakavyogawanywa kwa maafisa tarafa wa wilaya za mkoa huo alisema, Mkoa huo umepokea  jumla ya pikipiki 24 ambazo wamegawiwa Maofisa Tarafa wote ambapo Wilaya ya Kwimba tarafa 5, Sengerema 5,Magu 4,Misungwi 4, Nyamagana 1, Ilemela 1 na Ukerewe 4.

" Pikipiki hizi ni utekelezaji wa ahadi iliyotolewa na Rais Mhe.Dkt.John Magufuli katika kikao cha Juni 4,2019 kilichofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam baada ya Maafisa Tarafa  kuomba kupatiwa usafiri ili kuweza kutekeleza majukumu yao kwa wakati ambapo kila Afisa Tarafa amepewa pikipiki hii Kama chombo cha usafiri  kwa shughuli za Serikali katika eneo lake la kazi," alisema Tutuba.

Naye Afisa Tarafa Ukara Wilayani Ukerewe James Chuwa, alimshukuru Mhe. Rais kwa kuwapatia pikipiki hizo ambazo zitawasaidia katika usafiri na kudai kuwa awali wamepitia kipindi kigumu katika kuwafikia wananchi wa chini kabisa pamoja na kutatua matatizo yao ilikuwa lazima watumie fedha zao za mfukoni kwa ajili ya usafiri kwa ajili ya kutatua kero za wananchi.


"Ila sasa hivi  tunamuahidi   Mhe. Rais kwa vile ameishatupatia vyombo vya usafiri na tuna uhakika wa kufika field(eneo husika) ili kutatua kero za wananchi,sasa mabango hatoyaona tena,lakini jambo jingine la kumshukuru Mhe. Rais tunakwenda kufanya kazi kama ambavyo yeye alituahidi usafiri na sisi sasa tumeisha pokea na tunaenda kutenda kazi sawa sawa," alisema Chuwa.


Kwa upande wake Afisa Tarafa Mbarika Wilayani Misungwi Cresensia Mwalongo, alisema kupitia pikipiki hizo,zitawasaidia kwa kuwafikia wananchi na kutatua kero zao kwa  wakati,nyuma walikuwa wanaletewa kesi ila ukiangalia ni kwa namna gani ya kufika eneo la tukio ilikuwa inawapa wakati mgumu ambapo pia wanajifunza kuendesha vyombo hivyo vya usafiri ili waweze kuvitumia kama ilivyokusudiwa.

Matangazo

  • Tangazo la kukutana na Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Mwanza kwa shida mbalimbali. January 08, 2025
  • TANGAZO LA NANENANE TAREHE 8.8.2025 January 08, 2025
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • UZALISHAJI ZAO LA PAMBA WAONGEZEKA- MSIGWA

    May 03, 2025
  • DARAJA LA KIGONGO-BUSISI KUANZA KUTUMIKA MUDA WOWOTE KUANZIA SASA.

    May 02, 2025
  • SERIKALI YAANIKA TAKWIMU ZA MAENDELEO YA UTUMISHI YALIYOPATIKANA MWANZA

    May 01, 2025
  • MAKUNDI MAWILI YA MWISHO YALIYOFANYA ZIARA HIFADHI NA JNHPP YAWASILISHA NENO LA SHUKRANI KWA RAS BALANDYA

    April 29, 2025
  • Angalia zote

Video zinazotembea

Siku 365 za Mhe.Rais Samia Suluhu Hassan Mwanza
video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Fomu ya Ugonjwa
  • FFARS User Guidelines
  • Miongozo ya mfumo wa bajeti na Mipango
  • Makusanyo ya Ndani ya Halmashauri za Mkoa wa Mwanza
  • PReM
  • Maswali Yaulizwayo Mara kwa Mara
  • Opras fomu
  • OFISI MTANDAO

Viunganishi Linganishi

  • Tovuti ya Ikulu
  • Utumishi
  • Tamisemi
  • Ofisi ya Taifa ya Takwimu Tanzania
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Kuu ya Serikali

Watembeleaji

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive

    S.L.P: 119, Mwanza.

    Simu: 028-2501037

    Simu ya Mkononi: 028-2501037

    Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.