• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
Mwanza Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Mwanza

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia ya Mkoa
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti Mkoa
    • Seksheni
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Serikali za Mitaa
      • Afya
      • Elimu
      • Maji
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa Ndani
      • ununuzi na Ugavi
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Kitengo cha Sheria
  • Wilaya
    • Ilemela
    • Nyamagana
    • Magu
    • Misungwi
    • Kwimba
    • Sengerema
    • Ukerewe
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Jiji la Mwanza
    • Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
    • Hamashauri ya Wilaya ya Magu
    • Hamashauri ya Wilaya ya Sengerema
    • Hamashauri ya Wilaya ya Misungwi
    • Hamashauri ya Wilaya ya Kwimba
    • Hamashauri ya Wilaya ya Ukerewe
    • Hamashauri ya Wilaya ya Buchosa
  • Fursa za uwekezaji
    • Miundombinu ya Umwagiliaji na kilimo cha mkataba
    • Kilimo
    • Madini
    • Sekta ya Huduma
  • Huduma zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Watumishi
  • Machapisho
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa Kwa vyombo vya habari
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya video

RAS BALANDYA AZINDUA HUDUMA ZA KIBINGWA AWAMU YA PILI, AWATAKA WANANCHI KUCHANGAMKIA

Posted on: November 4th, 2024

RAS BALANDYA AZINDUA HUDUMA ZA KIBINGWA  AWAMU YA PILI, AWATAKA WANANCHI KUCHANGAMKIA


Katibu Tawala Mkoa wa Mwanza ndugu Balandya Elikana amemshukuru Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuwajali wananchi kwa kuboresha huduma za afya hadi kuwasogezea huduma bobezi katika vijiji ili wananchi wasipate adha ya kusafiri kwenda kwenye hospitali za rufaa.

Ametoa shukrani hizo leo Novemba 04, 2024 wakati akizindua huduma za kibingwa na bingwa bobezi awamu ya pili katika hospitali za halmashauri za mkoa huo zitakazofanywa na madaktari wa Dkt. Samia kwa juma moja.

Balandya ametumia wasaa huo kuwaalika wananchi kwenye hospitali zote za wilaya za mkoa huo kuanzia leo   Novemba 04, 2024 hadi Novemba 06, 2024 huku akisema kuwa wamesogezewa huduma hadi vijijini hivyo hakuna sababu yoyote ya kutofika kwenye hospitali kupata huduma za kibingwa.

Aidha, amebainisha kuwa wagonjwa zaidi ya milioni 2.6 wamefika kwenye vituo vya  kutolea huduma za afya na wengine walipewa rufaa kwenda kwenye hospitali kubwa kwa ajili ya kupata huduma bobezi hivyo ni fursa kwa wananchi kupata huduma hizo katika maeneo yao.

"Huduma za afya zinamgusa mwananchi moja kwa moja, Mwanza tunatambua umuhimu wenu na tunaahidi kuwapa ushirikiano mkunlbwa katika kipindi chote mtakachokuwepo hapa ili msikwame kwa lolote na ni matarajio yetu mtawarithisha wataalamu wetu utaalamu wenu." Balandya.

Mkurugenzi msaidizi huduma za afya za mtoto, mtoto mchanga na vijana kutoka Wizara ya Afya Dkt. Felix Bundala amesema uwepo wao kwenye huduma hizo tangu Septemba 9 mwaka huu wamehudumia wagonjwa elfu 60 katika mikoa 20 kabla ya wiki 2 zilizobaki kukamilisha mikoa yote 26.

"Pamoja na kuwapatia huduma wananchi, tunatambua faida wanayoipata familia wenye wagonjwa na kwa hakika familia zimefutwa machozi katika mazingira tofauti na tunamshukuru Mhe. Rais kwa kuona umuhimu wa kundi hili kurudia kutoa huduma kwa wananchi wa vijjijini." Dkt. Bundala.

"Mtapokua huko tuna upungufu mkubwa sana wa madaktari bingwa hivyo niwaombe sana mkajitoe hata usiku mtakapohitajika kwani tuna uhitaji mkubwa wa huduma za kibobezi mathalani Sengerema." Dkt. Jesca Lebba, Mganga Mkuu wa Mkoa wa Mwanza.

Matangazo

  • Tangazo la kukutana na Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Mwanza kwa shida mbalimbali. January 08, 2025
  • TANGAZO LA NANENANE TAREHE 8.8.2025 January 08, 2025
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • UZALISHAJI ZAO LA PAMBA WAONGEZEKA- MSIGWA

    May 03, 2025
  • DARAJA LA KIGONGO-BUSISI KUANZA KUTUMIKA MUDA WOWOTE KUANZIA SASA.

    May 02, 2025
  • SERIKALI YAANIKA TAKWIMU ZA MAENDELEO YA UTUMISHI YALIYOPATIKANA MWANZA

    May 01, 2025
  • MAKUNDI MAWILI YA MWISHO YALIYOFANYA ZIARA HIFADHI NA JNHPP YAWASILISHA NENO LA SHUKRANI KWA RAS BALANDYA

    April 29, 2025
  • Angalia zote

Video zinazotembea

Siku 365 za Mhe.Rais Samia Suluhu Hassan Mwanza
video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Fomu ya Ugonjwa
  • FFARS User Guidelines
  • Miongozo ya mfumo wa bajeti na Mipango
  • Makusanyo ya Ndani ya Halmashauri za Mkoa wa Mwanza
  • PReM
  • Maswali Yaulizwayo Mara kwa Mara
  • Opras fomu
  • OFISI MTANDAO

Viunganishi Linganishi

  • Tovuti ya Ikulu
  • Utumishi
  • Tamisemi
  • Ofisi ya Taifa ya Takwimu Tanzania
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Kuu ya Serikali

Watembeleaji

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive

    S.L.P: 119, Mwanza.

    Simu: 028-2501037

    Simu ya Mkononi: 028-2501037

    Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.