• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
Mwanza Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Mwanza

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia ya Mkoa
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti Mkoa
    • Seksheni
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Serikali za Mitaa
      • Afya
      • Elimu
      • Maji
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa Ndani
      • ununuzi na Ugavi
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Kitengo cha Sheria
  • Wilaya
    • Ilemela
    • Nyamagana
    • Magu
    • Misungwi
    • Kwimba
    • Sengerema
    • Ukerewe
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Jiji la Mwanza
    • Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
    • Hamashauri ya Wilaya ya Magu
    • Hamashauri ya Wilaya ya Sengerema
    • Hamashauri ya Wilaya ya Misungwi
    • Hamashauri ya Wilaya ya Kwimba
    • Hamashauri ya Wilaya ya Ukerewe
    • Hamashauri ya Wilaya ya Buchosa
  • Fursa za uwekezaji
    • Miundombinu ya Umwagiliaji na kilimo cha mkataba
    • Kilimo
    • Madini
    • Sekta ya Huduma
  • Huduma zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Watumishi
  • Machapisho
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa Kwa vyombo vya habari
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya video

RAS Mwanza ahimiza juhudi zifanyike kutokomeza Uvuvi haramu Ziwa Victoria

Posted on: December 6th, 2023

RAS Mwanza ahimiza juhudi zifanyike kutokomeza Uvuvi Haramu Ziwa Victoria


Katibu Tawala wa Mkoa wa Mwanza Balandya Elikana amezitaka Asasi zisizo za Kiserikali kuendelea kushirikiana na Serikali kutokomeza uvuvi haramu Ziwa Victoria ili sekta hiyo iendelee kuchangia uchumi wa mtu mmoja mmoja na pato la Taifa.

Akifungua leo kikao cha utambulisho wa mradi wa kuzuia kuzama maji Ziwa Victoria unaosimamiwa na Shirika linalojihusisha na mazingira na uvuvi la EMEDO kwenye ukumbi mdogo wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Balandya amebainisha bado kumekuwepo na kesi nyingi za wavuvi zinazotokana na Uvuvi haramu ikiwemo utumiaji wa nyavu zisizo stahili na njia mbaya za ulipuaji kuwapata samaki.

"Nawapongeza Shirika lisilo la Kiserikali la EMEDO  mnao jihusisha na mazingira na Uvuvi kwa kujikita kwenu mradi huu kwenye Wilaya mbili za mkoa huu za Ukerewe na Nyamagana,nina imani malengo yenu ya kuzuia  majanga ya  kuzama maji yatapungua au kumalizika kabisa",amesisitiza Mtendaji huyo wa Mkoa wakati akizungumza na washiriki wa kikao hicho wakiwemo maafisa uvuvi,Tasac,TMA, na Maabara ya Taifa ya samaki.

Balandya amesema sekta ya uvuvi kwa Mkoa wa Mwanza inachangia asilimia 7 ya pato la Mkoa,lakini majanga ya wavuvi kuzama na kupoteza maisha yamekuwa yakitokea mara kwa mara,hivyo mkazo wa elimu hauna budi kutolewa ili wafanye shughuli zao kwa usalama.

Meneja mradi kutoka EMEDO Arthur Mgema amesema mwaka 2021 walianza kufanya utafiti wa sababu za majanga ya kuzama maji kwa Wilaya nne za Ukerewe,Nyamagana,Muleba na Musoma vijijini na kubaini changamoto mbalimbali.

"Miongoni mwa sababu za majanga ya kuzama ni elimu ndogo za wavuvi,uelewa hafifu wa hali ya hewa pamoja na ulevi, na utafiti huu umewalenga makundi manne ambayo ni wavuvi,watoto,wachakataji na bodaboda wanaobeba samaki kutoka kwenye mialo",Mgema.

Mradi huo ulioanza mwaka 2022 utamalizika mwaka 2025 ukijikita kwenye mikoa ya Mwanza,Kagera na Mara yenye shughuli kubwa ya uvuvi.

Matangazo

  • Tangazo la kukutana na Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Mwanza kwa shida mbalimbali. January 08, 2025
  • TANGAZO LA NANENANE TAREHE 8.8.2025 January 08, 2025
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • UZALISHAJI ZAO LA PAMBA WAONGEZEKA- MSIGWA

    May 03, 2025
  • DARAJA LA KIGONGO-BUSISI KUANZA KUTUMIKA MUDA WOWOTE KUANZIA SASA.

    May 02, 2025
  • SERIKALI YAANIKA TAKWIMU ZA MAENDELEO YA UTUMISHI YALIYOPATIKANA MWANZA

    May 01, 2025
  • MAKUNDI MAWILI YA MWISHO YALIYOFANYA ZIARA HIFADHI NA JNHPP YAWASILISHA NENO LA SHUKRANI KWA RAS BALANDYA

    April 29, 2025
  • Angalia zote

Video zinazotembea

Siku 365 za Mhe.Rais Samia Suluhu Hassan Mwanza
video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Fomu ya Ugonjwa
  • FFARS User Guidelines
  • Miongozo ya mfumo wa bajeti na Mipango
  • Makusanyo ya Ndani ya Halmashauri za Mkoa wa Mwanza
  • PReM
  • Maswali Yaulizwayo Mara kwa Mara
  • Opras fomu
  • OFISI MTANDAO

Viunganishi Linganishi

  • Tovuti ya Ikulu
  • Utumishi
  • Tamisemi
  • Ofisi ya Taifa ya Takwimu Tanzania
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Kuu ya Serikali

Watembeleaji

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive

    S.L.P: 119, Mwanza.

    Simu: 028-2501037

    Simu ya Mkononi: 028-2501037

    Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.