• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
Mwanza Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Mwanza

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia ya Mkoa
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti Mkoa
    • Seksheni
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Serikali za Mitaa
      • Afya
      • Elimu
      • Maji
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa Ndani
      • ununuzi na Ugavi
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Kitengo cha Sheria
  • Wilaya
    • Ilemela
    • Nyamagana
    • Magu
    • Misungwi
    • Kwimba
    • Sengerema
    • Ukerewe
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Jiji la Mwanza
    • Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
    • Hamashauri ya Wilaya ya Magu
    • Hamashauri ya Wilaya ya Sengerema
    • Hamashauri ya Wilaya ya Misungwi
    • Hamashauri ya Wilaya ya Kwimba
    • Hamashauri ya Wilaya ya Ukerewe
    • Hamashauri ya Wilaya ya Buchosa
  • Fursa za uwekezaji
    • Miundombinu ya Umwagiliaji na kilimo cha mkataba
    • Kilimo
    • Madini
    • Sekta ya Huduma
  • Huduma zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Watumishi
  • Machapisho
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa Kwa vyombo vya habari
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya video

RAS Mwanza awashauri Wadau wa Ushirika kuwa chachu ya kukuza Uchumi nchini

Posted on: October 27th, 2022

Wadau wa Vyama vya Ushirika wanaoendelea kupata mafunzo maalum ya kutoka Analogia na kuingia Kidigitali wamepewa rai elimu hiyo ikalete mageuzi chanya kwenye vituo vyao vya kazi.
Akifungua Mafunzo hayo leo Jijini Mwanza kwa niaba ya Katibu Tawala wa Mkoa wa Mwanza Balandya Elikana, Katibu Tawala msaidizi Uchumi na Uzalishaji  Ndugu Emil Kasagara amebainisha kumekuwa na upotezu wa nyaraka na kazi kuzorota kutokana na kutumia utaratibu uliopitwa na wakati ambao umechangia kurudisha nyuma kasi ya maendeleo kwenye Vyama vya Ushirika.

"Ndugu zangu mliopo hapa kwa haya mafunzo msione aibu katika kujifunza siku zote tatu mtakazo kuwa hapa, mkumbuke kuelimika kwenu kunakwenda kuleta taswira mpya katika majukumu yenu ya kila siku kwenye vituo vyenu vya kazi." Amesema Kasagara.


Kasagara amebainisha kuwepo kwa hati chafu na migogoro isiyokwisha, kutokuwepo kwa uwazi wa uwajibikaji kwenye Vyama vya Ushirika na kwamba muarobaini wake ni matumizi ya TEHAMA katika rahisisha utoaji huduma bora kwa Wananchi.
Mrajisi Msaidizi kutoka Mkoa wa Mara, Kija Maheda amesema baadhi ya Viongozi waliopewa dhamana ya kuongoza vyama hivyo lakini hawakuwa na nia njema wametumia udhaifu huo wa mfumo duni kujinufaisha, lakini sasa kwa hatua hii mpya wanaoingia na jinsi Serikali hii ya awamu ya Sita ilivyonuia kuviinua Vyama vya Ushirika watasimama imara kuleta tija ya Maendeleo.
"Vyama vya Ushirika vinachangia ukuaji wa Uchumi wa Taifa letu, na  Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe Adam Malima ametuahidi kutupigania kuwa na Benki yetu ya Taifa ya Ushirika hivyo tuna kila sababu sisi Viongozi kuwa chachu ya Maendeleo," amesisitiza Maheda.
Mafunzo hayo yanasimamiwa na kutolewa na Tume  ya Maendeleo ya Ushirika Makao Makuu kwa kuwashirisha wenyeviti na Mameneja, warajisi wasaidizi, na Maafisa Ushirika kutoka Mikoa ya Mwanza, Geita, Kagera, Shinyanga pamoja na Mara.

Matangazo

  • Tangazo la kukutana na Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Mwanza kwa shida mbalimbali. January 08, 2025
  • TANGAZO LA NANENANE TAREHE 8.8.2025 January 08, 2025
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • UZALISHAJI ZAO LA PAMBA WAONGEZEKA- MSIGWA

    May 03, 2025
  • DARAJA LA KIGONGO-BUSISI KUANZA KUTUMIKA MUDA WOWOTE KUANZIA SASA.

    May 02, 2025
  • SERIKALI YAANIKA TAKWIMU ZA MAENDELEO YA UTUMISHI YALIYOPATIKANA MWANZA

    May 01, 2025
  • MAKUNDI MAWILI YA MWISHO YALIYOFANYA ZIARA HIFADHI NA JNHPP YAWASILISHA NENO LA SHUKRANI KWA RAS BALANDYA

    April 29, 2025
  • Angalia zote

Video zinazotembea

Siku 365 za Mhe.Rais Samia Suluhu Hassan Mwanza
video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Fomu ya Ugonjwa
  • FFARS User Guidelines
  • Miongozo ya mfumo wa bajeti na Mipango
  • Makusanyo ya Ndani ya Halmashauri za Mkoa wa Mwanza
  • PReM
  • Maswali Yaulizwayo Mara kwa Mara
  • Opras fomu
  • OFISI MTANDAO

Viunganishi Linganishi

  • Tovuti ya Ikulu
  • Utumishi
  • Tamisemi
  • Ofisi ya Taifa ya Takwimu Tanzania
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Kuu ya Serikali

Watembeleaji

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive

    S.L.P: 119, Mwanza.

    Simu: 028-2501037

    Simu ya Mkononi: 028-2501037

    Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.