• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
Mwanza Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Mwanza

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia ya Mkoa
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti Mkoa
    • Seksheni
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Serikali za Mitaa
      • Afya
      • Elimu
      • Maji
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa Ndani
      • ununuzi na Ugavi
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Kitengo cha Sheria
  • Wilaya
    • Ilemela
    • Nyamagana
    • Magu
    • Misungwi
    • Kwimba
    • Sengerema
    • Ukerewe
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Jiji la Mwanza
    • Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
    • Hamashauri ya Wilaya ya Magu
    • Hamashauri ya Wilaya ya Sengerema
    • Hamashauri ya Wilaya ya Misungwi
    • Hamashauri ya Wilaya ya Kwimba
    • Hamashauri ya Wilaya ya Ukerewe
    • Hamashauri ya Wilaya ya Buchosa
  • Fursa za uwekezaji
    • Miundombinu ya Umwagiliaji na kilimo cha mkataba
    • Kilimo
    • Madini
    • Sekta ya Huduma
  • Huduma zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Watumishi
  • Machapisho
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa Kwa vyombo vya habari
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya video

RAS Mwanza awashauri Wataalamu wa Tiba asili na Tiba mbadala kujiendeleza kielimu ili kutoa huduma bora kwa wananchi

Posted on: October 14th, 2023

RAS Mwanza awashauri Wataalamu wa Tiba asili na Tiba mbadala kujiendeleza kielimu ili kutoa huduma bora kwa wananchi


Kaimu Katibu Tawala Mkoa Mwanza Chagu Nghoma amewashauri Wataalamu wa Tiba asili na Tiba Mbadala kuchangamkia fursa za kujiendeleza kielimu ili kujiaminisha katika kutoa huduma zao,

Akizungumza leo Oktoba 14, 2023 kwenye ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa katika hafla fupi ya kuwakabidhi vyeti vya kuhitimu mafunzo, Chagu amesema bado asilimia kubwa ya Watanzania wanatumia tiba zao hivyo ni wajibu wao kuhakikisha huduma zao zinazingatia miongozo sahihi kutoka Wizara ya afya.

"Naipongeza Wizara ya Afya kwa kutoa mitaala ambayo mmefundishwa,hii itawasaidia kutoa huduma zenu vizuri na kujenga Imani zaidi kwa wananchi," Nghoma.

Amesema huduma za Tiba asili zimekuwa zikitumika kwa miaka mingi hapa nchini tangu enzi za mababu zetu, lakini Serikali kwa kutambua unyeti wa huduma zenu imeona ni vizuri  ziboreshwe kwa kupatiwa mafunzo kama haya.

"Haiwezekani ukatoa huduma kwa mgonjwa bila kwanza kujua anaumwa nini,ni lazima upate vipimo vyake ili ufahamu kiini cha tatizo lake na kuanza kumhudumia,"amesisitiza Nghoma wagonjwa kupata vipimo sahihi kabla ya kupatiwa Tiba mbadala.

Kuhusu wataalamu wa Tiba asili  wanaoibuka kila uchao na kujitangaza ni mabingwa wa magonjwa mbalimbali amewataka kuzingatia miongozo inayotolewa na Wizara ya afya kwani baadhi yao wamechangia vifo kwa wananchi kwa upotoshaji.

"Chuo chetu cha Mwanza Polytechnic kimeanza kutoa mafunzo haya kwa mara ya kwanza,na tunatarajia kutoa mafunzo zaidi kwani Mkoa wa Mwanza una wataalamu wa Tiba asili na mbadala zaidi ya elfu mbili,hivyo mafunzo kama haya ni muhimu kwao",Jerry Nyabululu,Mkurugenzi wa Chuo.

Awali akitoa taarifa ya malengo ya mafunzo hayo  kwa mgeni rasmi,mratibu wa mafunzo Dkt.Sally Giyunga amebainisha Wataalamu hao wamefundishwa namna ya kuandaa dawa mbadala,Sheria ya Tiba asili na mbadala,ukusanyaji wa dawa ghafi na namna ya kuzikausha kupitia nishati ya jua pamoja na namna ya huduma magonjwa yasiyoambukiza na yanayoambukiza.

"Tumekuwa na Moduli 13 kutoka Wizara ya afya na tulikuwa wakufunzi 3 tuliotoa mafunzo haya kwa  wataalamu hawa wapatao 90,"Dkt.Giyunga

"Ndugu mgeni rasmi tunaishukuru Wizara ya afya kwa kuona umuhimu wa sisi kupatiwa mafunzo haya,ombi.letu tunaomba kupunguziwa gharama za vipimo kwa wateja wetu ili tuweze kutoa huduma bora",Kawawa Athumani,Katibu wa Chama cha wataalamu wa Tiba asili Mwanza(CHAWATIATA)

Kauli mbiu ya Wahitimu hao inasema "Waganga kwa afya bora ya Watanzania".

Matangazo

  • Tangazo la kukutana na Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Mwanza kwa shida mbalimbali. January 08, 2025
  • TANGAZO LA NANENANE TAREHE 8.8.2025 January 08, 2025
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • UZALISHAJI ZAO LA PAMBA WAONGEZEKA- MSIGWA

    May 03, 2025
  • DARAJA LA KIGONGO-BUSISI KUANZA KUTUMIKA MUDA WOWOTE KUANZIA SASA.

    May 02, 2025
  • SERIKALI YAANIKA TAKWIMU ZA MAENDELEO YA UTUMISHI YALIYOPATIKANA MWANZA

    May 01, 2025
  • MAKUNDI MAWILI YA MWISHO YALIYOFANYA ZIARA HIFADHI NA JNHPP YAWASILISHA NENO LA SHUKRANI KWA RAS BALANDYA

    April 29, 2025
  • Angalia zote

Video zinazotembea

Siku 365 za Mhe.Rais Samia Suluhu Hassan Mwanza
video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Fomu ya Ugonjwa
  • FFARS User Guidelines
  • Miongozo ya mfumo wa bajeti na Mipango
  • Makusanyo ya Ndani ya Halmashauri za Mkoa wa Mwanza
  • PReM
  • Maswali Yaulizwayo Mara kwa Mara
  • Opras fomu
  • OFISI MTANDAO

Viunganishi Linganishi

  • Tovuti ya Ikulu
  • Utumishi
  • Tamisemi
  • Ofisi ya Taifa ya Takwimu Tanzania
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Kuu ya Serikali

Watembeleaji

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive

    S.L.P: 119, Mwanza.

    Simu: 028-2501037

    Simu ya Mkononi: 028-2501037

    Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.