• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
Mwanza Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Mwanza

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia ya Mkoa
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti Mkoa
    • Seksheni
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Serikali za Mitaa
      • Afya
      • Elimu
      • Maji
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa Ndani
      • ununuzi na Ugavi
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Kitengo cha Sheria
  • Wilaya
    • Ilemela
    • Nyamagana
    • Magu
    • Misungwi
    • Kwimba
    • Sengerema
    • Ukerewe
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Jiji la Mwanza
    • Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
    • Hamashauri ya Wilaya ya Magu
    • Hamashauri ya Wilaya ya Sengerema
    • Hamashauri ya Wilaya ya Misungwi
    • Hamashauri ya Wilaya ya Kwimba
    • Hamashauri ya Wilaya ya Ukerewe
    • Hamashauri ya Wilaya ya Buchosa
  • Fursa za uwekezaji
    • Miundombinu ya Umwagiliaji na kilimo cha mkataba
    • Kilimo
    • Madini
    • Sekta ya Huduma
  • Huduma zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Watumishi
  • Machapisho
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa Kwa vyombo vya habari
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya video

RC MAKALLA AAGIZA KUPATIKANA KWA SULUHU KWENYE USHURU WA VIBANDA STENDI KWIMBA

Posted on: June 27th, 2023

RC MAKALLA AAGIZA KUPATIKANA KWA SULUHU KWENYE USHURU WA VIBANDA STENDI KWIMBA


*Amtaka Mkuu wa Wilaya na Uongozi wa Halmashauri kulitatua suala la ushuru wa vibanda kwa mazungumzo*


*Ahimiza mkazo wa elimu kwa Jamii kuhusu utoro wa wanafunzi shuleni*


*Ataka kutolewa kwa Elimu kuhisu athari za Utoro shuleni*


Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. CPA. Amos Makala amemtaka Mkuu wa Wilaya ya Kwimba na uongozi wa Halmashauri ya Kwimba kutafuta suluhu katika Ukusanyaji wa ushuru kwa wafanyabiashara waliojenga vibanda katika stendi ya Ngudu na Malya.

Mhe. CPA. Makalla amesema hayo leo Juni 26, 2023 kwenye Mkutano wa Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Kwimba kwa ajili ya kujadili hoja za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) za Mwaka 2021/22.

"Niwaombe mkae nao muwaeleze kwamba eneo lile ni la serikali na  wanachotakiwa kufanya na mkuu wa wilaya uongoze kikao hicho, muwabaini wachochezi wa mgogoro ambao hawahusiki na eneo hilo mkae katika majadiliano na watu wanaohusika na vile vibanda, mpate orodha ya watu waliokubali kusaini mikataba na kulipa na mpare orodha ya watu waliogoma kulipa," RC Makalla.

Aidha Mkuu huyo wa Mkoa amewataka viongozi wa Halmashauri hiyo kuhakikisha wanasimamia na kutoa elimu kwa wazazi na jamii kwa ujumla juu ya umuhimu wa elimu kwa watoto ili kutokomeza suala la utoro na kukuza ufaulu shuleni.


"Swala la utoro shuleni, ufaulu na watu kutokumaliza shule niwaombe sana watendaji wetu tutoe elimu hiyo ya umuhimu wa watoto wetu kusoma na kuhakikisha ni ajenda yetu sote na sio afisa elimu tu na jamii nzima ielewe umuhimu wa kuwapeleka watoto shule kwa kuwa Serikali ya awamu ya sita imeboresha mazingira ya elimu hakuna sababu ya watoto kutokwenda shule,"CPA Makalla.

Vilevile, Mhe. Makalla ameipongeza Halmashauri ya Wilaya ya Kwimba kwa kupata Hati Safi kutoka kwa Mdhibiti na  Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) na amewataka Madiwani kufanyia kazi na kuijadili taarifa ya mkaguzi mara kwa mara.


Naye, Mkuu wa Wilaya ya Kwimba Mhe. Ng'wizalubu Ludigija amemuahidi Mkuu wa Mkoa kwa niaba ya watumishi, kamati ya usalama na Kwimba kwa ujumla kwamba watasimamia maelekezo yote aliyo wapa.

Halikadharika, Kaimu Mkaguzi Mkuu wa Nje wa Mkoa wa Mwanza Waziri Shabani kwa niaba ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) amesema Halmashauri ya Wilaya ya Kwimba imepata hati safi inayoridhisha kutokana na ushirikiano alioupata kwa watumishi wa Halmashauri hiyo.

Matangazo

  • Tangazo la kukutana na Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Mwanza kwa shida mbalimbali. January 08, 2025
  • TANGAZO LA NANENANE TAREHE 8.8.2025 January 08, 2025
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • UZALISHAJI ZAO LA PAMBA WAONGEZEKA- MSIGWA

    May 03, 2025
  • DARAJA LA KIGONGO-BUSISI KUANZA KUTUMIKA MUDA WOWOTE KUANZIA SASA.

    May 02, 2025
  • SERIKALI YAANIKA TAKWIMU ZA MAENDELEO YA UTUMISHI YALIYOPATIKANA MWANZA

    May 01, 2025
  • MAKUNDI MAWILI YA MWISHO YALIYOFANYA ZIARA HIFADHI NA JNHPP YAWASILISHA NENO LA SHUKRANI KWA RAS BALANDYA

    April 29, 2025
  • Angalia zote

Video zinazotembea

Siku 365 za Mhe.Rais Samia Suluhu Hassan Mwanza
video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Fomu ya Ugonjwa
  • FFARS User Guidelines
  • Miongozo ya mfumo wa bajeti na Mipango
  • Makusanyo ya Ndani ya Halmashauri za Mkoa wa Mwanza
  • PReM
  • Maswali Yaulizwayo Mara kwa Mara
  • Opras fomu
  • OFISI MTANDAO

Viunganishi Linganishi

  • Tovuti ya Ikulu
  • Utumishi
  • Tamisemi
  • Ofisi ya Taifa ya Takwimu Tanzania
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Kuu ya Serikali

Watembeleaji

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive

    S.L.P: 119, Mwanza.

    Simu: 028-2501037

    Simu ya Mkononi: 028-2501037

    Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.