• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
Mwanza Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Mwanza

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia ya Mkoa
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti Mkoa
    • Seksheni
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Serikali za Mitaa
      • Afya
      • Elimu
      • Maji
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa Ndani
      • ununuzi na Ugavi
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Kitengo cha Sheria
  • Wilaya
    • Ilemela
    • Nyamagana
    • Magu
    • Misungwi
    • Kwimba
    • Sengerema
    • Ukerewe
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Jiji la Mwanza
    • Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
    • Hamashauri ya Wilaya ya Magu
    • Hamashauri ya Wilaya ya Sengerema
    • Hamashauri ya Wilaya ya Misungwi
    • Hamashauri ya Wilaya ya Kwimba
    • Hamashauri ya Wilaya ya Ukerewe
    • Hamashauri ya Wilaya ya Buchosa
  • Fursa za uwekezaji
    • Miundombinu ya Umwagiliaji na kilimo cha mkataba
    • Kilimo
    • Madini
    • Sekta ya Huduma
  • Huduma zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Watumishi
  • Machapisho
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa Kwa vyombo vya habari
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya video

RC MAKALLA AAGIZA KUUNDWA KWA KAMATI KUFUATILIA WIZI WA VIFAA TIBA BUCHOSA

Posted on: June 5th, 2023

RC MAKALLA AAGIZA KUUNDWA KWA KAMATI KUFUATILIA WIZI WA VIFAA TIBA BUCHOSA.


*Akemea matumizi ya fedha mbichi, ataka sheria za fedha kufuatwa*


*Aonya wanaoeneza imani potofu zinazopeleka hadi kusababisha vifo*


*Barabara ya Sengerema- Buchosa kujengwa kiwango cha lami Mwezi Agosti 2023*


*Anamini Usalama kwa wananchi kuchagiza Maendeleo*


*Ana imani kubwa na nidhamu kazini kama dira ya Maendeleo*


Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. CPA Amos Makalla amemuagiza Katibu Tawala Mkoa kuunda Kamati itakayofuatilia Vifaa Tiba kwenye Vituo vya kutolea huduma za Afya Buchosa kufuatia tuhuma za kupotea na kurejeshwa kwa 'Ultrasound' kwenye hospitali ya Halmashauri hiyo.

Mhe. Makala ametoa agizo hilo mapema leo Juni 05, 2023 katika nyakati tofauti wakati akizungumza na Viongozi na Watendaji wa Halmashauri za Buchosa na Sengerema akiwa ziarani kujitambulisha wilayani humo na akamtaka Mkuu wa Wilaya kuwachukulia hatua watakaobainika kuhusika na wizi wa kifaa hicho kinachogharimu takribani Milioni 80.


Aidha, CPA Makalla amekemea tabia ya watendaji kukaa na fedha za mapato bila kupeleka benki na kusababisha matumizi ya fedha mbichi jambo ambalo linaitia doa halmashauri za Wilaya hiyo hadi kupelekea kupata hoja wakati qa ukaguzi wa hesabu za Serikali kama alivyobainisha kuwa kwa mwaka 2022/23 kumekua na hoja 30 Buchosa.


"Pelekeni fedha Benki msikae nazo ndani baada ya kukusanya nami kwa kutumia mfumo wa mapato wa Tausi nitawaona mnakusanyaje kila siku na nani ana pesa hajapeleka Bank na nitalirekebisha hili hivyo ni lazima mbadilike na ndio maana kwenye ripoti ya CAG mmetajwa kwa kutopeleka Bank fedha zaidi ya milioni 30 ndani ya mwaka uliopita" Amesema.


Vilevile, amewataka watendaji kusimamia miradi ya Maendeleo vizuri kwa kushirikiana na waheshimiwa Madiwani na kuhakikisha wanajibu hoja za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Serikali (CAG) kwa wakati na kufanya kazi kwa uadilifu ili kulinda rasilimali za nchi zisipotee.

 Aidha, ametoa onyo kwa tabia ya baadhi ya viongozi wa Dini wanaowahubiria wananchi kuamini Imani kali ambazo hazina uhalisia ambapo ametolea mfano kwa tukio la hivi karibuni la vifo vya Watoto wawili pamoja na wengine 13 kutotibiwa kutokana na kutofikishwa hospitali kupata matibabu ya Ugonjwa wa Surua huku wakiaminishwa kupona kwa maombi.


"Tuepuke imani kali za namna hii tutaangamia, tutumie wataalamu wetu wa afya kwenye Zahanati na vituo vya Afya vilivyo kwenye maeneo yetu tunayoishi na sio kuwasikiliza watu wengine wenye nia ya kujinufaisha kwa namna yoyote" Amesisitiza Mhe Makalla


Kwa upande mwingine, Mhe. Makalla amebainisha kuwa ifikapo mwezi Agosti mwaka huu Serikali inakwenda kujenga barabara yenye urefu wa Kilomita 56 ya Sengerema- Buchosa  kwa kiwango cha lami kwa zaidi ya Bilioni 70 ikiwa ni Muendelezo wa hatua za Mhe. Rais Samia katika kuwahudumia wananchi.


"Nataka niwahakikishie  kwamba barabara ya kutoka sengerema  kuja Buchosa  itaanza kujengwa rasmi niwaombe viongozi wote wa kata zote mtoe ushirikiano mtakapopitiwa katika maeneo yenu ili mwezi wa  nane mkandarasi aanze ujenzi rasmi." Mhe. Makalla.

Akizungumzana viongozi na watendaji wa Sengerema, Mhe. Makalla ametoa wito kqa Viongozi wa Siasa, Viongozi wengine na watendaji kushirikiana katika kufanya kazi kwani anaamini kuwa Maendeleo thabiti hupatikana pahala kwenye mahusiano thabiti.


Mkuu wa Wilaya ya Sengerema Mhe. Senyi Ngaga amesema kwa Mwaka wa fedha 2022/23 Halmashauri ya Buchosa imekusanya jumla ya Bilioni 2.2 kati ya Bilioni 3.1 inayokusudiwa ambayo ni sawa na asilimia 76 na kwamba wamekuja na mikakati kabambe ya kuhakikisha wanafikia lengo katika ukusanyaji mapato. Ameongeza kuwa kwa  upande wa kodi kupitia Mamlaka ya Mapato nchini (TRA) wamevuka lengo kwa kukusanya kwa zaidi ya asilimia 100.


"Sisi tunamshukuru sana Mhe. Rais, tuna miradi mingi ambayo inakwenda kuifungua Sengerema kama vile mradi wa Daraja la Kigongo-Busisi ambalo kukamilika kwake kutaiweka Sengerema kwenye sehemu ya juu sana na tutahakikisha tunahimarisha makusanyo ya Mapato ya ndani ambayo hadi sasa kwa Halmashauri ya Sengerema tumekusanya kwa asilimia 85." Mhe. Ngaga.

"Kwa upande wa shule za msingi, tunahitaji vyumba vya madarasa Elfu 2 na tunavyo 800 na kufanya kwa Halmashauri ya Buchosa kuwa na upungufu wa vyumba elfu 16 ila tunamshukuru Mhe. Rais kwa kutuletea fedha kujenga Miundombinu ya Madarasa, Shule Mpya pamoja na ukarabati wa madarasa na kwa upande wa Sekondari hatuna upungufu." Mhe. Ngaga.


Aidha, Mhe. Mkuu wa Wilaya amebainisha kuwa Wilaya hiyo inatarajia kuvuna zaidi ya Tani 5146 za Pamba na kwamba tayari Makampuni Saba yameonesha nia ya kununua na kwenye Sekta ya Uvuvi amemhakikishia Mhe. Mkuu wa Mkoa kuwa wataendelea kukusanya Mapato kwa zaidi ya 35% ikiwa ndio tegemeo kubwa.

"Kwenye Halmashauri yetu ya Buchosa tunatekeleza miradi kwa mfumo wa 'force acct' ila kamati za ujenzi hazifanyi vema na inatoa ishara ya miradi kutekelezwa vibaya sasa tunaomba kama miongozo ya kusimamia miradi umebadirika basi tupewe taarifa ili tusimamie ipasavyo". Amesema Mhe. Augustine Makoye, Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Sengerema.

Matangazo

  • Tangazo la kukutana na Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Mwanza kwa shida mbalimbali. January 08, 2025
  • TANGAZO LA NANENANE TAREHE 8.8.2025 January 08, 2025
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • UZALISHAJI ZAO LA PAMBA WAONGEZEKA- MSIGWA

    May 03, 2025
  • DARAJA LA KIGONGO-BUSISI KUANZA KUTUMIKA MUDA WOWOTE KUANZIA SASA.

    May 02, 2025
  • SERIKALI YAANIKA TAKWIMU ZA MAENDELEO YA UTUMISHI YALIYOPATIKANA MWANZA

    May 01, 2025
  • MAKUNDI MAWILI YA MWISHO YALIYOFANYA ZIARA HIFADHI NA JNHPP YAWASILISHA NENO LA SHUKRANI KWA RAS BALANDYA

    April 29, 2025
  • Angalia zote

Video zinazotembea

Siku 365 za Mhe.Rais Samia Suluhu Hassan Mwanza
video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Fomu ya Ugonjwa
  • FFARS User Guidelines
  • Miongozo ya mfumo wa bajeti na Mipango
  • Makusanyo ya Ndani ya Halmashauri za Mkoa wa Mwanza
  • PReM
  • Maswali Yaulizwayo Mara kwa Mara
  • Opras fomu
  • OFISI MTANDAO

Viunganishi Linganishi

  • Tovuti ya Ikulu
  • Utumishi
  • Tamisemi
  • Ofisi ya Taifa ya Takwimu Tanzania
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Kuu ya Serikali

Watembeleaji

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive

    S.L.P: 119, Mwanza.

    Simu: 028-2501037

    Simu ya Mkononi: 028-2501037

    Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.