• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
Mwanza Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Mwanza

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia ya Mkoa
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti Mkoa
    • Seksheni
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Serikali za Mitaa
      • Afya
      • Elimu
      • Maji
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa Ndani
      • ununuzi na Ugavi
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Kitengo cha Sheria
  • Wilaya
    • Ilemela
    • Nyamagana
    • Magu
    • Misungwi
    • Kwimba
    • Sengerema
    • Ukerewe
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Jiji la Mwanza
    • Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
    • Hamashauri ya Wilaya ya Magu
    • Hamashauri ya Wilaya ya Sengerema
    • Hamashauri ya Wilaya ya Misungwi
    • Hamashauri ya Wilaya ya Kwimba
    • Hamashauri ya Wilaya ya Ukerewe
    • Hamashauri ya Wilaya ya Buchosa
  • Fursa za uwekezaji
    • Miundombinu ya Umwagiliaji na kilimo cha mkataba
    • Kilimo
    • Madini
    • Sekta ya Huduma
  • Huduma zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Watumishi
  • Machapisho
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa Kwa vyombo vya habari
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya video

RC MAKALLA AMEZIAGIZA HALMASHAURI KUPANGA NA KUTOA FEDHA ZA UTEKELEZAJI WA MASUALA YA LISHE KWA WATOTO.

Posted on: August 17th, 2023

RC MAKALLA AMEZIAGIZA HALMASHAURI KUPANGA NA KUTOA FEDHA ZA UTEKELEZAJI WA MASUALA YA LISHE KWA WATOTO.


*Ameagiza Wakurugenzi kuwawezesha Maafisa Lishe wa Halmashauri ili watimize majukumu yao*


*Ameziagiza Halmashauri kuweka Agenda ya Lishe kwenye Vikao*


Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. CPA Amos Makalla amezipongeza halmashauri   za Ilemela, Magu, Kwimba na Jiji la Mwanza kwa kupanga na kutoa fedha kulingana na idadi ya watoto wenye umri chini ya miaka mitano na amewataka Misungwi, Buchosa na Ukerewe kuhakikisha wanatekeleza Matakwa ya Mkataba wa Lishe ipasavyo.

Ametoa agizo hilo leo Agosti 17,2023 katika kikao cha tathmini ya Utekelezaji wa Mkataba wa Lishe kwa kipindi cha Julai 2022 hadi Juni 2023 kilichofanyika kwenye Ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa ambapo ameagiza halmashauri hizo kuiga mfano kwa wenzao na kuchukua hatua kabla au ifikapo tarehe 20 Agosti, 2023.

Vilevile, amezitaka halmashauri kuhakikisha wanatoa Elimu ya Lishe kupitia Vikao vyote vya kitendaji ili kila mmoja apate uelewa ili taaluma hiyo isambae na kusaidia kufanikisha adhma ya Serikali ya kuondoa udumavu kwenye jamii.

"Maafisa Lishe wasiwe kimbilio la kazi za dharula hususani kama kupokea wageni wakija kwenye halmashauri, wana majukumu makubwa ya kufuatilia utekelezaji na kutoa Elimu hivyo basi hakikisheni wanapewa usafiri na vitendeo kazi vingine ili wafike malengo." CPA Makalla.

Mhe. Makalla amesema Serikali inaweka msukumo wa kipekee kwenye masuala ya lishe na kwamba Wakuu wa Mikoa wamesaini Mkataba na Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuhusu maeneo maalum ya kuwekea mkazo katika Suala la lishe na kwamba Mhe. Rais alitoa viashiria maalum vya kupima utekelezaji wa mkataba huo.

"Lishe duni kwa wanawake wajawazito ni miongoni mwa sababu zinazowaweka katika mazingira hatarishi zaidi yanayoweza kusababisha kujifungua watoto njiti au wafu, watoto wenye utindio wa ubongo au hata mimba kuharibika kabisa." Mkuu wa Mkoa.

Akizungumzia utekelezaji wa maazimio ya kikao cha Mwezi februari mwaka huu kwa niaba ya Mganga Mkuu wa Mkoa, Muuguzi Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Claudia Kaluli amesema jumla ya Shilingi Milioni 855.6 zimetumika kwa watoto zaidi ya 846 ambayo ni sawa na Shilingi 1010 kwa kila mtoto ambayo ni sawa na asilimia 110 ya lengo.

Vilevile, Bi Claudia amefafanua kuwa halmashauri  za mkoa huo zimeanzisha Klabu za Lishe kwenye Shule za msingi na sekondari kwa asilimia 80% na kwamba kila halmashauri imehakikisha kumekuwepo Madini joto katika chumvi

kutokana na upimaji wa sampuli 4146  uliofanyika.

"Mkoa wetu umepata asilimia 69 kwenye kadi alama ya utekelezaji wa afya za lishe katika kipengele cha Hali ya utoaji wa chakula chenye Lishe kwenye Shule za Msingi na Sekondari katika kipindi cha Julai 2022 hadi Juni 2023." Amesema Afisa Lishe Mkoa, Bi. Sofia Lazaro.

Vilevile amefafanua kuwa muongozo unazitaka halmashauri kutoa Shilingi Elfu Moja kwa kila mtoto kuanzia umri wa miaka 0 hadi 5 lakini halmashauri  hazijafanya vizuri na kwamba zoezi la utoaji wa chanjo ya matone ya Vitamini A halmashauri  zimefanya vizuri.

Matangazo

  • Tangazo la kukutana na Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Mwanza kwa shida mbalimbali. January 08, 2025
  • TANGAZO LA NANENANE TAREHE 8.8.2025 January 08, 2025
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • UZALISHAJI ZAO LA PAMBA WAONGEZEKA- MSIGWA

    May 03, 2025
  • DARAJA LA KIGONGO-BUSISI KUANZA KUTUMIKA MUDA WOWOTE KUANZIA SASA.

    May 02, 2025
  • SERIKALI YAANIKA TAKWIMU ZA MAENDELEO YA UTUMISHI YALIYOPATIKANA MWANZA

    May 01, 2025
  • MAKUNDI MAWILI YA MWISHO YALIYOFANYA ZIARA HIFADHI NA JNHPP YAWASILISHA NENO LA SHUKRANI KWA RAS BALANDYA

    April 29, 2025
  • Angalia zote

Video zinazotembea

Siku 365 za Mhe.Rais Samia Suluhu Hassan Mwanza
video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Fomu ya Ugonjwa
  • FFARS User Guidelines
  • Miongozo ya mfumo wa bajeti na Mipango
  • Makusanyo ya Ndani ya Halmashauri za Mkoa wa Mwanza
  • PReM
  • Maswali Yaulizwayo Mara kwa Mara
  • Opras fomu
  • OFISI MTANDAO

Viunganishi Linganishi

  • Tovuti ya Ikulu
  • Utumishi
  • Tamisemi
  • Ofisi ya Taifa ya Takwimu Tanzania
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Kuu ya Serikali

Watembeleaji

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive

    S.L.P: 119, Mwanza.

    Simu: 028-2501037

    Simu ya Mkononi: 028-2501037

    Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.