Swahili
  • English
  • Swahili
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
Mwanza Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Mwanza

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia ya Mkoa
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti Mkoa
    • Seksheni
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Serikali za Mitaa
      • Afya
      • Elimu
      • Maji
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa Ndani
      • ununuzi na Ugavi
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Kitengo cha Sheria
  • Wilaya
    • Ilemela
    • Nyamagana
    • Magu
    • Misungwi
    • Kwimba
    • Sengerema
    • Ukerewe
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Jiji la Mwanza
    • Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
    • Hamashauri ya Wilaya ya Magu
    • Hamashauri ya Wilaya ya Sengerema
    • Hamashauri ya Wilaya ya Misungwi
    • Hamashauri ya Wilaya ya Kwimba
    • Hamashauri ya Wilaya ya Ukerewe
    • Hamashauri ya Wilaya ya Buchosa
  • Fursa za uwekezaji
    • Miundombinu ya Umwagiliaji na kilimo cha mkataba
    • Kilimo
    • Madini
    • Sekta ya Huduma
  • Huduma zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Watumishi
  • Machapisho
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa Kwa vyombo vya habari
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya video

RC MAKALLA : USIKILIZZAJI KERO ZA ARDHI BILA UTATUZI NI KAZI BURE

Posted on: March 7th, 2024

RC MAKALLA : USIKILIZZAJI KERO ZA ARDHI BILA UTATUZI  NI KAZI BURE


*Asema Maafisa Ardhi wanafeli kwenye Mambo Matano*


*Awataka Maamuzi ya utatuzi migogoro ardhi yafanyiwe kazi*


*Awataka maafisa ardhi kusimamia sheria za ardhi ili kutenda haki kwa wananchi*


*Aagiza maafisa ardhi kutoa maamuzi ya maandishi kwa rejea ya baadae*


*Awataka maafisa hao kutowazungusha wananchi wanapohitaji huduma*


*Aagiza ulipaji wa fidia ili kuondoa migogoro kwenye maeneo yaliyotwaliwa*


*Atangaza ziara ya 2 kusikiliza Jimbo kwa Jimbo, awali amesikiliza kero 926*


Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. CPA Amos Makalla amewataka watumishi wa sekta ya ardhi mkoani humo kufuata sheria na miiko ya kazi yao ili kutenda haki kwa wananchi pamoja na kuepusha migogoro ya ardhi ikiwa ni pamoja na kumaliza migogoro iliyobainika kwa kufikia maamuzi.

Ametoa agizo hilo leo  07 Machi 7, 2024 wakati akifungua kikao kazi cha watumishi wa sekta ya ardhi kinachowakutanisha wataalamu hao kutoka kwenye Halmashauri za mkoa huo katika ukumbi wa halmashauri ya Manispaa ya Ilemela.


"Nawaomba twendeni tukafanye kazi kwa mujibu wa sheria, ipo mifano ya kutolewa hati kwenye ardhi juu ya hati ingine yaani hata ukisikia unajiuliza huyu afisa aliyetoa hati hii ni wa aina gani jamani, nendeni mkafanye kazi kwa kufuata taratibu kwa weledi mkubwa," amesisitiza  Mkuu wa Mkoa.

Katika kutatua kero za wananchi, Makalla amewataka kutoa maamuzi kwa maandishi ili kupata rejea ya kudumu kwenye hatua zilizopitia hadi kutatua kero ikiwemo utoaji fidia kwa maeneo yaliyotwaliwa kwa ajili ya kumbukumbu kwa miaka ya baadae na akawataka kuacha urasimu kwenye utoaji huduma.

Kamishna Msaidizi wa ardhi Mkoa wa Mwanza Bi. Happyness Mtutwa amebainisha kuwa kikao kazi hicho ni mahususi kwa ajili ya kukumbushana misingi ya utoaji huduma kwa wananchi kupitia sekta ya ardhi na kwamba watumishi 126 walioajiriwa na 146 wa mkataba wamekutana.


"Mhe. Mkuu wa Mkoa huu ni muendelezo wa utatuzi wa kero za ardhi kwa watumishi wa ardhi na tumeitana kwa ajili ya kukumbushana miiko, taratibu na misingi ya utendaji kazi kwenye sekta yetu na kuepuka rushwa na kuwa na weledi wakati wote." Amesema Kamishna Msaidizi.

Bi. Mtutwa amefafanua kuwa kupitia zoezi la usikilizaji wa kero za wananchi lililofanywa na Mhe. Mkuu wa Mkoa mwishoni mwa mwaka jana na kuagiza utatuzi wa haraka tayari wamemaliza migogoro 86 na kwamba hati 4206 zimetolewa ndani ya muda huo mfupi kwa wananchi.


Aidha, amebainisha kuwa wananchi 570 wamesikilizwa kupitia kliniki ya Jijini Mwanza, 132 Usagara-Misungwi na 262 Ilemela na kwamba kupitia maduhuli wamekusanya Bilioni 5.6 ndani ya muda huo wa takribani miezi sita ya uendeshaju wa kliniki za kusukiliza kero.

Matangazo

  • Tangazo la kukutana na Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Mwanza kwa shida mbalimbali. January 08, 2025
  • TANGAZO LA NANENANE TAREHE 8.8.2025 January 08, 2025
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • BARAZA LA RAIS LA USHAURI WA KILIMO NA CHAKULA LAKUTANA NA WADAU WA KILIMO KANDA YA ZIWA

    June 04, 2025
  • MWANZA, SIMIYU ZANG'ARA UTAMILIFU DARASA LA SABA KANDA YA ZIWA

    May 30, 2025
  • RAS MWANZA AZINDUA RASMI MRADI WA KUPAMBANA NA UGONJWA WA SELI MUNDU

    May 30, 2025
  • WAANDISHI WA HABARI MWANZA WAPIGWA MSASA MIKAKATI YA KUTOKOMEZA WATOTO WA MITAANI

    May 29, 2025
  • Angalia zote

Video zinazotembea

Siku 365 za Mhe.Rais Samia Suluhu Hassan Mwanza
video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Fomu ya Ugonjwa
  • FFARS User Guidelines
  • Miongozo ya mfumo wa bajeti na Mipango
  • Makusanyo ya Ndani ya Halmashauri za Mkoa wa Mwanza
  • PReM
  • Maswali Yaulizwayo Mara kwa Mara
  • Opras fomu
  • OFISI MTANDAO

Viunganishi Linganishi

  • Tovuti ya Ikulu
  • Utumishi
  • Tamisemi
  • Ofisi ya Taifa ya Takwimu Tanzania
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Kuu ya Serikali

Watembeleaji

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive

    S.L.P: 119, Mwanza.

    Simu: 028-2501037

    Simu ya Mkononi: 028-2501037

    Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.