• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
Mwanza Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Mwanza

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia ya Mkoa
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti Mkoa
    • Seksheni
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Serikali za Mitaa
      • Afya
      • Elimu
      • Maji
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa Ndani
      • ununuzi na Ugavi
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Kitengo cha Sheria
  • Wilaya
    • Ilemela
    • Nyamagana
    • Magu
    • Misungwi
    • Kwimba
    • Sengerema
    • Ukerewe
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Jiji la Mwanza
    • Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
    • Hamashauri ya Wilaya ya Magu
    • Hamashauri ya Wilaya ya Sengerema
    • Hamashauri ya Wilaya ya Misungwi
    • Hamashauri ya Wilaya ya Kwimba
    • Hamashauri ya Wilaya ya Ukerewe
    • Hamashauri ya Wilaya ya Buchosa
  • Fursa za uwekezaji
    • Miundombinu ya Umwagiliaji na kilimo cha mkataba
    • Kilimo
    • Madini
    • Sekta ya Huduma
  • Huduma zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Watumishi
  • Machapisho
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa Kwa vyombo vya habari
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya video

RC Malima ahimiza kutokomeza unyanyasaji wa kijinsia

Posted on: March 27th, 2023


Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe.Adam Malima amewataka washiriki wa mafunzo ya Dawati la Jinsia na Ushauri Nasihi kuhakikisha wanaielewa mada ya Unyanyasaji wa kijinsia na kuhakikisha wanakwenda kuitokomeza katika jamii zao.

Mhe. Malima ameyasema hayo wakati akifungua mafunzo ya Dawati la Jinsia na Ushauri Nasihi yaliyofanyika katika Chuo Kikuu Huria cha Tanzania, Tawi la Mwanza leo Machi 27,2023.

"Kutokomeza unyanyasaji wa kijinsia uanze na mimi,na wewe ili jamii ipate uelewa na ishiriki juhudi za kuondokana na hali hiyo," amesema Mhe.Malima.

Aidha, ametoa wito kwa menejimenti za Vyuo Vikuu na Taasisi za Elimu ya juu Nchini, ambavyo bado hawajaanzisha madawati ya haya na kutoa mafunzo ya Ushauri na jinsi ya kusimamia madawati haya, kufanya hivyo haraka kwani itasaidia sana kutokomeza vitengo vya unyanyasaji wa jinsia na hivyo kuisaidia jamii kwa ujumla.

Hata hivyo,ameongeza kuwa kufanyika kwa mafunzo hayo ndani ya Chuo hicho kumekuja wakati muafaka ambako jamii sasa inaanza kuwa na uelewa mpana wa masuala ya Jinsia na Ushauri Nasihi.

"Kuandaa jambo hili siyo kazi rahisi, hivyo ninaupongeza uongozi wa Chuo Kikuu Huria Tanzania Chini ya Makamu Mkuu wake Profesa Elifas  Bisanda, akisaidiwa na Kurugenzi ya Huduma za Wanafunzi na Mkurugenzi wa kituo cha Mwanza kwa maandalizi yote na kuona umuhimu wa kutoa mafunzo haya ya Ushauri Nasihi kwa jamii yake,"amesema Mhe.Malima.

Kwa upande wake Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania Profesa Elifas Bisanda amesema Chuo hicho kitaendelea kushirikiana na Jeshi la Magereza kwa kuwapa elimu wafungwa  wenye nia ya kujiendeleza ili nao waweze kutimiza ndoto zao.

Naye, Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania huduma za mikoa, Profesa  Alex Makulilo amesema wamekuwa na utaratibu wa kutoa mafunzo hayo ya kuwajengea uwezo wa kumudu changamoto mbalimbali, sababu wafanyakazi wengine wanakwenda kufanya kazi katika Taasisi nyingine pia wengine huwa ni waajiriwa wapya ambao hawajajengewa uwezo hivyo wamekuwa na utaratibu wa kuwajengea uwezo mara kwa mara.

Serikali ilitoa mwongozo wa uanzishwaji wa Dawati la Jinsia katika Taasisi za Elimu ya juu na Elimu ya Kati, hivyo amewapongeza Chuo Kikuu Huria cha Tanzania kwa kutekeleza maelekezo ya Serikali katika kuanzisha madawati hayo.

Akimshuku Mhe.Malima kwa niaba ya washiriki wote Dkt.Regina Malima amesema wamefarijika sana kwa kuwa na mtendaji Mkuu wa Mkoa na hivyo wanaahidi yale yote yatakayofundishwa watakwenda kuyafanyia kazi kwa manufaa ya Umma.

Matangazo

  • Tangazo la kukutana na Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Mwanza kwa shida mbalimbali. January 08, 2025
  • TANGAZO LA NANENANE TAREHE 8.8.2025 January 08, 2025
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • UZALISHAJI ZAO LA PAMBA WAONGEZEKA- MSIGWA

    May 03, 2025
  • DARAJA LA KIGONGO-BUSISI KUANZA KUTUMIKA MUDA WOWOTE KUANZIA SASA.

    May 02, 2025
  • SERIKALI YAANIKA TAKWIMU ZA MAENDELEO YA UTUMISHI YALIYOPATIKANA MWANZA

    May 01, 2025
  • MAKUNDI MAWILI YA MWISHO YALIYOFANYA ZIARA HIFADHI NA JNHPP YAWASILISHA NENO LA SHUKRANI KWA RAS BALANDYA

    April 29, 2025
  • Angalia zote

Video zinazotembea

Siku 365 za Mhe.Rais Samia Suluhu Hassan Mwanza
video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Fomu ya Ugonjwa
  • FFARS User Guidelines
  • Miongozo ya mfumo wa bajeti na Mipango
  • Makusanyo ya Ndani ya Halmashauri za Mkoa wa Mwanza
  • PReM
  • Maswali Yaulizwayo Mara kwa Mara
  • Opras fomu
  • OFISI MTANDAO

Viunganishi Linganishi

  • Tovuti ya Ikulu
  • Utumishi
  • Tamisemi
  • Ofisi ya Taifa ya Takwimu Tanzania
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Kuu ya Serikali

Watembeleaji

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive

    S.L.P: 119, Mwanza.

    Simu: 028-2501037

    Simu ya Mkononi: 028-2501037

    Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.