• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
Mwanza Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Mwanza

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia ya Mkoa
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti Mkoa
    • Seksheni
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Serikali za Mitaa
      • Afya
      • Elimu
      • Maji
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa Ndani
      • ununuzi na Ugavi
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Kitengo cha Sheria
  • Wilaya
    • Ilemela
    • Nyamagana
    • Magu
    • Misungwi
    • Kwimba
    • Sengerema
    • Ukerewe
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Jiji la Mwanza
    • Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
    • Hamashauri ya Wilaya ya Magu
    • Hamashauri ya Wilaya ya Sengerema
    • Hamashauri ya Wilaya ya Misungwi
    • Hamashauri ya Wilaya ya Kwimba
    • Hamashauri ya Wilaya ya Ukerewe
    • Hamashauri ya Wilaya ya Buchosa
  • Fursa za uwekezaji
    • Miundombinu ya Umwagiliaji na kilimo cha mkataba
    • Kilimo
    • Madini
    • Sekta ya Huduma
  • Huduma zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Watumishi
  • Machapisho
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa Kwa vyombo vya habari
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya video

RC Malima apania kuiinua kiuchumi Wilaya ya Ukerewe

Posted on: August 31st, 2022

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe Adam Malima Jumanne hii ametoa wiki sita kwa Mkandarasi anayejenga barabara ya lami ya kilomita mbili ya Nakutunguru na Nkilizya mjini Nansio kutokana na kusuasua kukamilisha kwa wakati.

Mhe Malima katika ziara yake ya kujitambulisha Wilayani humo na kukagua Miradi ya maendeleo,amesema barabara  hiyo ya zaidi ya Shs milioni mia tisa imeanza kuwa mzigo kwa wananchi ambao wamemlalamikia tangu ameingia Wilayani humo.

"Nasema wazi katika hili sina mzaha huyu Mkandarasi mwezi ujao nitakuja hapa asipokamilisha nitajua la kufanya" Mkuu wa Mkoa

Mhe Malima katika ziara hiyo amefanya ukaguzi wa ujenzi wa Hospitali ya Wilaya mjini Nansio yenye gharama ya zaidi ya Shs Bilioni 2 ambayo sasa imesimama kutokana na utata wa gharama halisi,Chuo cha Veta kilichopo Muhula,Shule ya Sekondari iliyopo Kagunguli na Kituo cha Afya cha Igalla

Aidha Mkuu huyo wa Mkoa katika mazungumzo na Watumishi wa Halmashauri amewahakikishia kuitazama Wilaya ya Ukerewe kwa jicho la tatu akimaanisha kuiinua kimapato hasa kutokana na kuzungukwa na fursa za Uchumi wa bluu.

Mkuu wa Wilaya ya Ukerewe Mhe Dennis Mwila amesema wanaishukuru Serikali ya awamu ya Sita kwa kuleta Miradi  mingi Wilayani humo ikiwemo ya afya,elimu na maji ambayo imekuwa na tija kwa wananchi.

Amemuomba Mkuu wa Mkoa kuingilia kati na kuipatia ufumbuzi  kwa baadhi ya Miradi ambayo imegunikwa na ubabaishaji na kuwa mzigo kwa wananchi.

Mkuu wa Mkoa Mhe Adam Malima amekamilisha ziara za kujitambulisha na kukagua Miradi ya Maendeleo wilaya zote za Mkoa wa Mwanza.

Matangazo

  • Tangazo la kukutana na Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Mwanza kwa shida mbalimbali. January 08, 2025
  • TANGAZO LA NANENANE TAREHE 8.8.2025 January 08, 2025
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • UZALISHAJI ZAO LA PAMBA WAONGEZEKA- MSIGWA

    May 03, 2025
  • DARAJA LA KIGONGO-BUSISI KUANZA KUTUMIKA MUDA WOWOTE KUANZIA SASA.

    May 02, 2025
  • SERIKALI YAANIKA TAKWIMU ZA MAENDELEO YA UTUMISHI YALIYOPATIKANA MWANZA

    May 01, 2025
  • MAKUNDI MAWILI YA MWISHO YALIYOFANYA ZIARA HIFADHI NA JNHPP YAWASILISHA NENO LA SHUKRANI KWA RAS BALANDYA

    April 29, 2025
  • Angalia zote

Video zinazotembea

Siku 365 za Mhe.Rais Samia Suluhu Hassan Mwanza
video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Fomu ya Ugonjwa
  • FFARS User Guidelines
  • Miongozo ya mfumo wa bajeti na Mipango
  • Makusanyo ya Ndani ya Halmashauri za Mkoa wa Mwanza
  • PReM
  • Maswali Yaulizwayo Mara kwa Mara
  • Opras fomu
  • OFISI MTANDAO

Viunganishi Linganishi

  • Tovuti ya Ikulu
  • Utumishi
  • Tamisemi
  • Ofisi ya Taifa ya Takwimu Tanzania
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Kuu ya Serikali

Watembeleaji

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive

    S.L.P: 119, Mwanza.

    Simu: 028-2501037

    Simu ya Mkononi: 028-2501037

    Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.